Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Tukio la kuzaliwa kwa mbuzi mwenye viungo vya jinsia zote mbili (kike na kiume), limeibua mshangao na taharuki kwa wakazi wa Mtaa wa Nyantorotoro B, Kata ya Nyankumbu, Manispaa ya Geita, huku mmiliki wa mbuzi huyo akimtelekeza kwa balozi wa shina ili apatiwe maombi, akiamini huenda angeweza kubadilika na kuwa na jinsia moja.
Mmiliki wa mbuzi huyo, Catherine Kachwele, mkazi wa eneo hilo, amesema alijikuta katika hali ya sintofahamu baada ya kugundua kuwa mbuzi aliyopewa kama zawadi ana jinsia mbili.
Akizungumza na East Afica Radio, Kachwele, ambaye ni mtaalamu wa tiba asili, amesema kuwa alipata mbuzi huyo mkoani Kigoma kama sehemu ya malipo ya huduma ya matibabu aliyotoa kwa mgonjwa aliyekuwa hana fedha za kutosha.
Akitoa ufafanuzi wa kitaalamu, daktari wa mifugo wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Jackson Mutayaba, amesema hali hiyo inajulikana kama hitilafu ya kuzaliwa (congenital anomaly), ambapo viungo vya mwili hujitokeza tofauti na mpangilio wa kawaida.
Ameeleza kuwa moja ya sababu zinazoweza kuchangia ni pamoja na kuzaliana kwa wanyama wa ukoo mmoja (inbreeding), hali inayoweza kusababisha mabadiliko yasiyo ya kawaida katika maumbile ya wanyama.