Mbwana Samatta aanza kusugua benchi KRC Genk

Mbwana Samatta aanza kusugua benchi KRC Genk

Hata hapa huwa tuna shangaana hivi Fulani imekuwaje ameachwa... Fulani amepataje namba....

Samatta huyu aliye enda ulaya sio sawa na yule aliye kuwa winga teleza pale simba yule alikuwa kama singano, kama ngasa wawakati huo... Ana mbio ana chenga... Kapelekwa kati basi amekuwa mvivu amekuwa wa kusubiria vya kutenga...

Nazani ndio maana hata timu ya taifa watanzania wengi nao wamemlalamikia, hivyo sio uchawi mchawi ni yeye mwenyewe

Hata hasheem alifika level kama yake sasa alivyo polomoka yeye mwenyewe ana fahamu...

Ukilegeza tu basi umekwisha... Afanyekazi ajitume...

Wakina Paulsens walio wahi kuwa makocha wa timu yetu ya taifa walimuacha sababu yakuwa ni mzigo katika timu...

Mara mia pale Genk angekuwepo Msuva sio huyu Samatta wa sasa...
Naanza kuamini Kati ya watanzania 10 , 9 ni wachawi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana kocha mpya....anatafuta kikosi....alipofika Samatta aliendelea kuanza kikosini lakini hakuwa na kiwango kizuri...sasa anaingia dakika za mwisho lakini bado kiwango hakiko vizuri...Mna-geria anaeanzishwa amejitahidi lakini kiwango Chake cha kawaida tu...Samatta bado ana-nafasi. Naamini England anapaweza kwani ni mzuri kwa Timu inayocheza kitimu...Genk ya mwaka huu kidogo nayo haiko vizuri .
 
Mshambuliaji na Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta hali imeanza kuwa tete katika klabu yake ya KRC Genk. Hii ni kufuatia kupigwa benchi mara mbili mfululizo katika mechi za ligi.

Mechi ya kwanza ilikuwa nyumbani pale KRC Genk walipo ikalibisha Waasland Beveren, katika mechi hiyo Samatta alianzia benchi kisha dakika ya 74 akaingia.

Mechi ya pili ni hapo jana tarehe 22. RSC Anderlecht waliikalibisha KRC Genk katika uwanja wao wa nyumbani. Kama kawaida Samatta alianzia benchi Kisha kupata nafasi ya kucheza dakika ya 63. RSC Anderlecht ilishinda kwa magoli wawili kwa bila.

Nafasi ya Mbwana Samatta imechukuliwa na Mnigeria Poul Onuachu.

Je, kwa hatua ni kuonyesha kwamba kiwango cha Mbwana Samatta kimeshuka ama ni mbinu za Mwalimu.?

Binafsi huyo Samatta sijawahi kumkubali...anyway ila kama Mtz namuombea mafanikio...
 
Juzi kaingia dk ya 85...mnaigeria kaendelea kuaminiwa na ametupia tena goli....Samatta kiwango hakiko sawa mzima huu.
 
Back
Top Bottom