Consigliere,
Hata makanisani wanapiga vita ndoa za mbwembwe. Inaonekana umekaririshwa mambo, wafunga ndoa za kikristu wengu tu huchukuana na kwenda kufungishwa ndoa ma Padre bila ya kuwepo mikusanyiko ya watu kama mnavyoona.
Katoliki zinafungwa sana ndoa hizo. Wanaotaka ndoa zenye mbwembwe siyo makanisa bali ni wanafamilia. Usichanganye mambo.
Umemaliza kila kitu nilichotaka kuzungumza. Watu wengi huchanganya sana kati ya ndoa na harusi, Ndoa ni tendo la kuunganisha watu wawili wapendanao kiimani tu tukiamini chini ya watumishi wa Mungu waliokasimishwa mamlaka hayo yaani Sheikh au Padre au Mchungaji wakati harusi ni sherehe baada ya tukio zima la ndoa kufungwa. Sasa hapa jinsi ya kuifanya hiyo sherehe ya ndoa ni familia zenu Zaidi zitaamua, kwa upande wa dini hakuna dini hata moja inayo-complicate the whole process.