Hongera zake sana.
Ni anajituma kufanya kilichompeleka ...tumpe pongezi.
Leo ni mechi yake ya nne,akitokea benchi baada ya dakika 60 ya mchezo...yaani aliingia dakika ya 72,77,60 na leo kaingia ya 79 na kufunga goli ktk dk ya 81...thus kwa wastani ya dakika alizocheza uwanjani na kupata goli tumpe Hongera zake.
Inaonekana pattern bado,uaminifu wa kocha kwake upo kwani siku zote nne anampa sub ya kumtoa mchezaji mmoja(mshambuliaji mwenzake)....ambaye siku waliyoshinda 6 huyo jamaa alikua katupia 2,ila ndiye aliyetoka na Samata kuingia dakika ya 77.....kwa hiyo inaonyesha kuna kitu anakionyesha na tayari anashindanishwa....
Na kwa mara ya kwanza pia,leo amepata Yellow Card.
Aina ya Sub anayopewa,kama Mungu atamjalia wepesi siku zijazo ni rahisi kwake kuanza ktk first eleven....na kupiga HATUA zaidi.