Mbwana Samatta aifungia bao la kwanza Genk

Mbwana Samatta aifungia bao la kwanza Genk

Nilikuwa naangalia game, kapewa dakika chache kazitumia vizuri. Hivi ndio inavyotakiwa maana pale ni kugombania namba asipofanya kweli anaenda loan. Leo kaweka kambani goli muhimu Sana maana ngoma ilikuwa inaenda droo ya 2-2. Kuingia tu kabadilisha game. Goli la kwanza na yellow card ya kwanza. Big up wa nyumbani
 
maskini kumbe wnampigaga sub dah but io siku atakua lulu ulaya

Man, game yenyewe hii ndio kwanza ya tatu. Hata mwezi hajamaliza mazoezini kwahiyo subira uvuta heri. Kama hivi next game anaweza kupewa 45 minutes mpaka wamkubali kwanza maana kuwa kwnye first eleven kwenye mpira wa kulipwa sio mchezo
 
Alipata team nje akaenda akachemsha,alitaka maisha ya bongo kutwa kuwepo mawela bar sinza
 
Mie nikajua yale magoli yetu ya kuongeza idadi ya viumbe duniani. Basi sawa.
 
Hongera zake sana.
Ni anajituma kufanya kilichompeleka ...tumpe pongezi.
Leo ni mechi yake ya nne,akitokea benchi baada ya dakika 60 ya mchezo...yaani aliingia dakika ya 72,77,60 na leo kaingia ya 79 na kufunga goli ktk dk ya 81...thus kwa wastani ya dakika alizocheza uwanjani na kupata goli tumpe Hongera zake.
Inaonekana pattern bado,uaminifu wa kocha kwake upo kwani siku zote nne anampa sub ya kumtoa mchezaji mmoja(mshambuliaji mwenzake)....ambaye siku waliyoshinda 6 huyo jamaa alikua katupia 2,ila ndiye aliyetoka na Samata kuingia dakika ya 77.....kwa hiyo inaonyesha kuna kitu anakionyesha na tayari anashindanishwa....
Na kwa mara ya kwanza pia,leo amepata Yellow Card.
Aina ya Sub anayopewa,kama Mungu atamjalia wepesi siku zijazo ni rahisi kwake kuanza ktk first eleven....na kupiga HATUA zaidi.
 
Back
Top Bottom