Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Mshambuliaji wa kimataifa wa taifa Stars na KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta yumo kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa na timu ya Middlesbrough ya Uingereza mwezi ujao.
Meneja wa timu hiyo ya mhimili wa pili wa ligi kuu ya Uingereza au Tier two iliyo na makazi na uwanja wake wa Riverside Tony Pulis, amevutiwa na mshambuliaji huyo ambae mpaka sasa amefunga magoli 75 kwenye mechi zote alizocheza.
Timu ya KRC Genk imeweka thamani ya pauni za Uingereza milioni kati ya 7 hadi 8 ili kumwachia mchezaji huyo aende nchiniu Uingereza.
Samatta ameonyesha umahiri mkubwa katika kufunga magoli ambapo mpaka sasa amefunga magoli 12 katika mechi 18 ambazo timu yake KRC Genk imecheza katika ligi ya Ubelgiji ya Belgian Jupiler Pro League.
Samatta alitengeneza jina lake katika timu ya TP Mazembe ya Congo DRC tangu mwaka 2011 hadi 2016 ambapo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alifunga magoli 160 katika mechi 103 alizochezea timu hiyo.
Alijiunga na KRC Genk mwaka 2016 ambapo mwaka huohuo alitwaa taji la mwanasoka bora wa Afrika akifunga magoli 55, usaidizi assists mara 14 katika mechi 151 alizochezea Genk.
Meneja Tony Pulis anaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji huyo katika kuboresha safu yake ya ushambuliaji wa timu hiyo katika duru la pili la mzunguko wa ligi hiyo ngumu ya daraja la pili ijulikanayo kama Championship.
Samatta huenda akaziba nafasi ya mshambuliaji Rudy Gestede ambae huenda nae akasajiliwa na timu ya Celtic ya Scotland baada ya kushindwa kuonyesha makucha yake kwa Middlesbrough.
Hata hivyo pia timu za ligi kuu ya Uingereza nazo zimekuwa zikiwatuma maskauti wao kwenda kumuangalia Samatta akicheza mechi mbalimbali za hivi karibuni.
Timu za Everton, West Ham United, Burnley na Brighton & Hove Albion zote zinaangalia kujiimarisha katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo ambao umeanza katika kipindi hiki cha siku kuu ya Christmas.
Endapo Genk watakuwa tayari kumwachia mchezaji huyo kupitia kifungu maalum kiitwacho "release clause" ambacho huwekwa kwenye mkataba, basi Samatta ataingia Uingereza mwezi ujao wa January.
Mwezi January dirisha la usajili hufunguliwa tena kwa usajili mdogo ambapo timu mbalimbali hujaribu kusajili wachezaji wengi wa gharama nafuu kulingana na mahitaji.