Wadau wa JF,
Habari ndugu zangu, kwanza kabisa nawapongeza taifa kwa kwenda kushiriki afcon 2019 nchini Misri japo kimazabe.
Leo nimemsikia Samatta akisema wanaenda kucheza michuano hiyo kwa lengo la kuleta heshima kwa Tanzania na Awamu ya tano ya uongozi huu.
Kama ni kwa ajili ya Tanzania, nampa big up. Lakini kaniboa kuitaja wanaenda kucheza kwa ajili ya serikali ya awamu hii ya tano.
Hivi Samatta hajajifunza kuzungumza kwenye media au na yeye anaupata ukichaa, maana pembeni yake alikuwepo Juliana Shonza.
Huyu dada ni Naibu Waziri Wa Michezo sijui, au ndiyo naye ameamua kumuambia azungumze hivyo?
Basi Taifa Stars itarudi mapema sana nyumbani na haitafika mbali kwa sababu kapteni wao kashaanza kuwagawa Watanzania.