Mbwana Samatta: Nina wazo kwanini Dar isibadilishwe jina ikaitwa Kolomije

Mbwana Samatta: Nina wazo kwanini Dar isibadilishwe jina ikaitwa Kolomije

Samatta angalia jamaa asije akakufilisi maana hachelewi. Kupiga mnada nyumba kwa gear ya kodi ya ardhi
 
Duuh, kumbe koromije imekua maarufu hadi ulaya[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kaajiri Management na mwanasheria
Mkuu huyo huyo Tindikali unadhani anajua hilo ulilomwambia? Nafikiri upeo wake ni kukumbuka kuwafungulia kuku asubuhi na kuangakia mkewe anachati na nani kwenye simu. Suala la mchezaji mkubwa wa kimataifa kwamba ni taasisi yenye management na mwanasheri; na kwamba kila mwnadamu ana uhuru wa kujieleza ni ngumu sana kwake kuelewa. Anadhani ukishakuwa mchezaji basi utazame mpira tu na dunia nyingine yote inayokuhusu unai - switch off! Pretty vile!
 
Niliahidi kukuletea sababu mkuu soma hapo chini:

Mbwana Samatta alipofikia ni kama Entity ya kibiashara, anahitaji kila aina ya support toka kwa kila mtu na kila taasisi. Mbwana anaweza kuja kuwekeza kibiashara hapa nyumbani TZ hasa DSM, huku anahitaji ardhi,leseni za kibiashara, na kusajiri kampuni na kuhitaji endorsement ya serikali na ya taasisi binafsi kama za kanisa la Gwajima na Clouds FM. Atahitaji hizo leseni na ardhi toka serikalini na atatakiwa alipe kodi serikalini. unadhani atakuwa na mazingira rafiki ya kibiashara kama ataingia utata(kuchukiwa) na wenye dhamana huko serikalini wale ambao wako nyuma ya Makonda? Hata akifungua academy ya michezo au hospital kama wenzake akina Kanu, Adebayor, Etoo na Drogba anahitaji usajiri/vibali vya serikali. hawezi kuingiza container la vifaa vya biashara zake au academy bila kufanya tax clearance serikalini na hukomhujui nani yupo nyuma ya Bashite. Haya machache lakini yapo mengi wengine watakuja kuchangia. unafikiri kwanini IPP media hawashabikii sana hizi habari za Bashite? Unafikiri hawataki kuuza sana magazeti yao au wanampenda sana Bashite? je wewe una akili sana ya Biashara kuliko Mzee Mengi na washauri wake? Au Mzee Bhakresa? au Mo? Umemuona Manji au umemuona Mbowe na yanayowakuta unayajua? Sio lazima ukosoe kila kitu bila tafakari!! Kuna mengine yamewazidi upeo wenu wa kufikri na uelewa kuhusu biashara na kufanya vuta na Jamii au media au na Kaisari mwenye dola.
Mkuu Titicomb sikufahamu, lakini ulichoandika hapo umekosea SANA na sijui lengo lako ni nini. Naomba nibainishe machache ya makosa yako hayo:
  1. Kwanza mantiki ya bandila la huyo anayejiita Samata (sina hakika kama ni huyu tunayemzungumzia) siioni kwa vyovyote kwamba ni negative. Yeye amependekeza tu Dar iitwe "Kolomije!", basi! Kolomije ni nini? Ni wazi kwa upepo unaozunguka sasa hivi mitandaoni ukisikia neno Kolomije lazima uwafikirie watu wawili MAARUFU Dar na wanaorumbana kwa sasa. Wote ni watu maarufu positively na ni viongozi wa ngazi ya juu na wanaoheshimika sana. Sasa kuna tatizo gani hapo?
  2. Pili, kwa wewe kuweka hadharani hizo shughuli za kibiashara za mwenye hayo maneno usiyoyapenda (japo huna hakika kama kweli ni yeye aliyetoa ujumbe huo uliotumia jina lake) ni kuonyesha una nia ya wazi kwamba kwa sababu unazoziona wewe huyu bwana anyimwe ushirikiano wa taasisi za serikali na za kidini eti tu kwa sababu wewe umemwelewa unavyotaka.
  3. Tatu, ambalo ni muhimu zaidi na ni baya sana kwa upande wako, kwa kuandika hadharani kwamba huyu mwenye maoni hayo anajiweka katika mazingira ya kunyimwa uhalali wa kuungwa mkono na serikali (wa kupewa vibali vya kisheria) kufanya shughuli yoyote halali huko Tanzania eti tu kwa sababu unadhani anawaudhi wenye mamlaka wa sasa hata kama hakuvunja sheria! Fikra za namna hii ni fikra za ovyo na ndizo zinazolea utawala wa ovyo wa watu kudhani wakipata dhamana serikalini basi wana haki ya kufanya wanachojisikia na wananchi (kama wewe) wataona wana haki ya kufanya hivyo!
  4. Nne, japo wameshalisema wengi; kila mtu ana haki ya kutoa maoni, kama wewe ulivyofanya. Kuwa mchezaji maarufu haina maana dunia nyingine inayokuzunguka haikuhusu. Bahati mbaya huyu (kama ni yeye kweli) alitoa maoni yake kwa utambulisho wake. Na wewe unadhani anapashwa kucheza mpira tu na atie ganzi katika masuala mengine ya kijamii. Wewe umejificha ktk kivuli cha Titicomb. Ungekuwa certified user wa JF tungekuheshimu.
Namalizia kwa kuandika kwamba, hata ungempeleka mahakamani leo huyo anayejiita Mbwana Samata angekushinda vibaya kwa hoja mbili nyepesi:
  1. Mimi ninawapenda sana watu wanaotoka Kolomije, hasa wanaishi Dar kwani ni watu wachapakazi sana.
  2. Nina uhuru wa kutoa maoni yangu ambayo hayavunji sheria.
 
Mtu akifanya juhudi binafsi akafanikiwa kimaisha na kuwa maarufu, wabongo wengi wanapata dhana kuwa ni wao ndo wamemfikisha hapo na inabidi afuate matakwa yao asije kuwaudhi
 
Mbwana ni Entity kubwa ya kibiashara kuliko "wauza duka wa mtaani".
Wauza duka wa mtaani hawawezi kuingia mkataba mkubwa na makampuni makubwa ulimwenguni kama Nike, Adidas, AIG n.k lakini Mbwana anaweza. Mbwana anaweza kuingia partinership ya mradi wowote mkubwa na serikali na akapiga mabilioni ya pesa. Kueni vijana mjue ulimwengu wa kibiashara.
Kwa hiyo Diamond ni Entity ndogo?
 
Yaani Pepsi diet wametoka povu hao.
Samatta wala hataathirika lolote na post yake. Mkimpiga ban bongo ataomba ukazi london na mambo yataendelea kama kawaida.
 
Umeongea ikweli sana mkuu.je mbona huyo Bashite ni mshabiki wa simba ilihali yeye mwanasiasa?
Ndio ushangae hapo. Watu huwa tunajisahau sana, kwamba sisi tuna uhuru wa kutoa maoni yetu na wengine hawana eti kwa kuwa wao ni wasanii au wachezaji mpira. Huo ni unafki.
 
Nakushauri usijiingize ktk siasa utapotea Sasa hiv
Kwani nyie mnao post humu ni wana siasa? Suala la elimu fuatilieni elimu ya Ronaldo wa Madrid ndio mtajijua kinacho wasumbua ni wivu.
 
Lakini bahati mbaya na yeye mwenyewe kuandika hajui. Sijui anawezaje kusoma mikataba anayosainishwa.

"Isibadirishwe"!
Ww mwenyewe kiswahili hujui isibadilishwe unaandika isibadirishwe sijui wawapi ww
 
Ww mwenyewe kiswahili hujui isibadilishwe unaandika isibadirishwe sijui wawapi ww

Mwingine huyu hajui kusoma na kuandika.

Alama za nukuu maana yake nimechukua maneno ya Mbwana Samatta kuonyesha jinsi asivyojua kuandika. Daaah... nchi yetu masikini weee!

Huo sasa wivu,yeye c mtaalami wa sheria wenye fani yao watafanya kwa niaba yake


Hapana, huwezi kuwa mwajiri wa accountant, management na mwanasheria wakati wewe mwenyewe hujui kusoma na kuandika jamani, watakutumia kama kitambaa cha kupangusia jiko.

Wachezaji karibia wote wa michezo mikubwa duniani, NBA, NFL, n.k. wanatokea vyuoni.

Kumbe wenzetu walijua aisee!
 
ndo mmezoea kuminya freedom of speech,Kwan yy si mtanzania?
Bosi wangu ngoja nikueleze ukweli, kuna faida kubwa sana kiuchumi na kijamii kwa Mbwana Samatta kukwepa kujiingiza ktk mgogoro huu. Akinyamaza nahisi hatapungukiwa kitu kikubwa kama kuliko ikatokea kuchukiwa na upande wowote wa wanaopambana. Sio lazima uamini maneno yangu. Silence is wisdom kwa wakati flani.
 
Back
Top Bottom