Mkuu
Titicomb sikufahamu, lakini ulichoandika hapo umekosea SANA na sijui lengo lako ni nini. Naomba nibainishe machache ya makosa yako hayo:
- Kwanza mantiki ya bandila la huyo anayejiita Samata (sina hakika kama ni huyu tunayemzungumzia) siioni kwa vyovyote kwamba ni negative. Yeye amependekeza tu Dar iitwe "Kolomije!", basi! Kolomije ni nini? Ni wazi kwa upepo unaozunguka sasa hivi mitandaoni ukisikia neno Kolomije lazima uwafikirie watu wawili MAARUFU Dar na wanaorumbana kwa sasa. Wote ni watu maarufu positively na ni viongozi wa ngazi ya juu na wanaoheshimika sana. Sasa kuna tatizo gani hapo?
- Pili, kwa wewe kuweka hadharani hizo shughuli za kibiashara na mwenye hayo maneno usiyoyapenda (japo huna hakika kama kweli ni yeye aliyetoa ujumbe huo uliotumia jina lake) ni kuonyesha una nia ya wazi kwamba kwa sababu unazoziona wewe huyu bwana anyimwe ushirikiano wa taasisi za serikali na za kidini eti tu kwa sababu wewe umemwelewa unavyotaka.
- Tatu, ambalo ni muhimu zaidi na ni baya sana kwa upande wako, kwa kuandia hadharani kwamba huyu mwenye maoni hayo anajiweka katika mazingira ya kunyimwa uhalali wa kuungwa mkono na serikali (wa kupewa vibali vya kisheria) kufanya shughuli yoyote halali huko Tanzania eti tu kwa sababu unadhani anawaudhi wenye mamlaka wa sasa hata kama hakuvunja sheria! Fikra za namna hii ni fikra za ovyo na ndizo zinazolea utawala wa ovyo wa watu kudhani wakipata dhamana serikalini basi wana haki ya kufanya wanachojisikia na wananchi (kama wewe) wataona wana haki ya kufanya hivyo!
- Nne, japo wameshalisema wengi; kila mtu ana haki ya kutoa maoni, kama wewe ulivyofanya. Kuwa mchezaji maarufu haina maana dunia nyingine inayokuzunguka haikuhusu. Bahati mbaya huyu (kama ni yeye kweli) alitoa maoni yake kwa utambulisho wake. Na wewe unadhani anapashwa kucheza mpira tu na atie ganzi katika masuala mengine ya kijamii. Wewe umejificha ktk kivuli cha Titicomb. Ungekuwa certified user wa JF tungekuheshimu.
Namalizia kwa kuandika kwamba, hata ungempeleka mahakamani leo huyo anayejiita Mbwana Samata angekushinda vibaya kwa hoja mbili nyepesi:
- Mimi ninawapenda sana watu wanaotoka Kolomije, hasa wanaishi Dar kwani ni watu wachapakazi sana.
- Nina uhuru wa kutoa maoni yangu ambayo hayavunji sheria.