MC Pilipili acha kutafuta kiki kupitia Marehemu Seth(Bikira wa kisukuma)

MC Pilipili acha kutafuta kiki kupitia Marehemu Seth(Bikira wa kisukuma)

simba jike

Senior Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
182
Reaction score
537
Tangu juzi kulipotokea msiba wa marehemu seth pilipili amekuwa akipost qoutes mbalimbali kuhusu marehemu, si kitu kibaya ila baada ya hapo ameendelea kupost picha mbalimbali za matukio ya msiba huo zinaoonesha amepigwa kwa simu huku akijinasibu kuwa amehuzunishwa,ameumia na kusikitishwa sana na kifo cha Seth.

Jamani kweli kabisa mtu una huzuni unaweza kupose na kupigwa picha kiasi kile!? Kulikuwa na bunches of media photographers kwanini asingetulia kama wengine akapigwa picha kulingana na matukio!?

**Nilimshangaa zaidi alipoandaa makala ya wasifu wa marehemu na kutaja mpaka ugonjwa uliomuua siku hiyo hiyo ambayo seth alifariki as if alikuwa msemaji wa familia**

Hata mwajiri wake (E-FM) hakudiriki kutoa hiyo taarifa japo kwa sehemu kubwa anahusika katika utoaji wa taarifa za mwajiriwa wake.

Pilipili humpendi Seth hata kidogo coz urafiki ni kustiriana na kujaliana why uanike ugonjwa wa Seth tena mapema kabisa wakati watu bado wapo kwenye taharuki kubwa baada kupokea taarifa ya kifo tena bila haya wala aibu ukaiwahisha hiyo makala you tube ili Seth aadhirike vizuri

Rafiki wa hivi simuhitaji katika maisha yangu.

Pilipili sina chuki binafsi na wewe ila unabore kiki za kijinga kwenye mambo ya msingi hazitakusaidia na zitakupoteza.
R. I. P SETH

Mdau JF

Sent from my Phantom6 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli hii tabia sio nzuri na hata kisheria na maadili haikubaliki. Mambo ya kupiga picha marehemu ama kusema ugonjwa uliosababisha kifo chake ni jukumu la familia kama kuna mtu mwingine anafanya hivyo ni sharti apewe kibali na familia

Hata week kadhaa zilizopita kuna mdau mmoja alituletea taarifa ya msiba wa mwana JF mwenzetu tulishukuru kwa taarifa ila cha kusikitisha mkuu yule aliweka hadi vipimo alivyofanya na majibu+ ugonjwa uliomuua as if yeye ndio alikuwa msemaji wa familia ingawa alijiyambulisha kama ni rafiki yake tu
 
Skuhiz,misiba ya watu
Imekua jukwaa kujinasibu

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Nadhani ataona kama yupo hum lakin pia kama ataona kilichosemwa ni sahihi basi atachenge na kama ataona sio sahihi basi hatochange maamuz ni yake jukum lako muandish ushakamilisha
 
Alienichefua ni Mpoki eti leo kampost marehemu akiwa anaumwa kalazwa kitandani akiwa mkondefu kabisa,ila binadamu wengine hawana utu kabisa,Pilipili nae anapost tena video za selfie kabisa,hivi mtu una maumivu kweli utajiselfisha video?Popularity inatafutwa at any cost.
 
Screenshot_2017-07-12-22-27-33.png


Hivi ndivyo Huyu jamaa alivyokwenda kutalii kwenye mazishi ya Seth katende
 
Swaswa,kijiji kimoja Dodoma majirani zao na kile kijiji cha Zuzu
Wanakula sana viwavi jeshi kama mboga sbb ya ukame,na hutegemea mahikwii na mamung'unya kama mbadala wa maboga...Ni walaji wazuri sana wa sesetya na udawi pori
Daaah....muwaha chitetelaje che wayago
 
Back
Top Bottom