Mc Pilipili utanisamehee kwa ukweli huu "huna kipaji cha kuchekesha"

Mc Pilipili utanisamehee kwa ukweli huu "huna kipaji cha kuchekesha"

Kuna mambo ya kupeana support na kuna mambo pia ya kuelezana ukweli, siko hapa kumkatisha mtu tamaa ila My Brother Mc Pilipili sanaa ya Uchekeshaji imekupiga Kanzu.
Speed ya standup comedy ilipo na ww unachokifanya ni Kigoma na London.

"Wapaka mafuta kwa mgongo wa chupa hamtakosekana kussuport comedy ya huyu mtu kinafiki,ila kwa mm binafsi,
Lazima tuiite beleshi beleshi na sio kijiko kikubwa. !"

Mc pilipili Ukumbuke tu,si kila anayepiga makofi basi anakupongeza , ukitaka uhakika muulize "Mbu".

WEWE SI MCHEKESHAJI.

AHSANTENI.
UKO SAHIHI BADO KIJANA AANGALIE FURSA NYINGINE, TUTAMUUNGA MKONO.
 
Hata kazi ya kuwa Mc anaforce tu, haiwezi!
Yote kwa yote Tz hamna stand up comedy..
Tz Mpoki kidogo anajtahid akiamua kufanya serious.
Kinachowa cost hawa ma celeb wa kibongo ubunifu ni sifuri ni watu wa kucopy copy sana hawajui ili ukubalike unabidi uwe mbunifu lakini pia ushamba mzigo pilipili ni bonge la mshamba ukiangalia video zake akiwa uko usA mpaka aibu
 
Kuna mambo ya kupeana support na kuna mambo pia ya kuelezana ukweli, siko hapa kumkatisha mtu tamaa ila My Brother Mc Pilipili sanaa ya Uchekeshaji imekupiga Kanzu.
Speed ya standup comedy ilipo na ww unachokifanya ni Kigoma na London.

"Wapaka mafuta kwa mgongo wa chupa hamtakosekana kussuport comedy ya huyu mtu kinafiki,ila kwa mm binafsi,
Lazima tuiite beleshi beleshi na sio kijiko kikubwa. !"

Mc pilipili Ukumbuke tu,si kila anayepiga makofi basi anakupongeza , ukitaka uhakika muulize "Mbu".

WEWE SI MCHEKESHAJI.

AHSANTENI.
Kiukweli nilishawahi kuhudhuria harusi moja hv jamaa alikuwa ndo mshehereshaji...kwakweli ukumbi mzima ulikuwa hauna mbavu kwa vituko vyake....naheshimu mawazo yako ila ilikupasa ujiangalie wewe kwanza una hobby na hvyo vitu...coz kuna watu wanasema Mr bean ni mkali wa vichekesho ila kuna wengine hawamkubali...mf mm huwa siwezi kukaa hata dk 5 kuangalia bongo movie..lkn kuna watu ndo movie wanazozipenda...so inawezekana pilipili kuna vitu anavifanya au kuongea lakini wewe huelewi...ila wanaomwelewa wanaona wanapata burudani...km ameweza kupata mialiko hadi ughaibuni basi jamaa mkali...
 
watanzania wanafiki tu.. kwa mfano ukitoa post kwamba Diamond hajui kuimba watu watajaa na kushadadia..wabongo wivu tu unawasumbua kwa ufupi ni umasikini
 
Nchi hii comedian naturally ni Mpoki, joti, Bambo na kingwendu tu..wengne cjui wanachofanya
bambo ana kingwendu?? uko serious kweli mkuu?? hao wanabana pua hawabadiliki commedy hawajui
 
Pilipili kwa stand up comedy bado yuko nyuma kwa kweli. Ajaribu kuangalia jirani zetu Kenya na Uganda, watu kama Salvador, Professor Hamo, YY, Njoroge, Mc Jesse ajifunze kitu. Aache kuhamisha vichekesho watu wanavyotumiana kwenye groups za whatsApp na kuzileta stage.
 
Mkuu futa kauli kabisa ,Kiukweli MC pilipili kwenye show ya Leo amevunja watu mbavu,Jamaa yupo vizuri sana kwenye stand-up comedy show ya Leo ameitendea Haji....Wasaka Tonge.....Wasanii wa bongo wapo vizuri,tuwatie moyo wanaweza.
 
Mara nyingi huwa anachukua stuff kutoka kwa Nigerian Comedians (Buchi, Gordons etc) na anazitasfiri kwa Kiswahili. Kiukweli hata mimi ninaona kabisa vichekesho vyake havichekeshi. Naona hata Joti anamzidi and you can now imagine level aliyopo.
 
Huyo idriss nae kafulia mpaka huruma yaani mtu upewe 600 millions na fame alafu mwishowe ugange njaa kwa kubaka talent za watu na kutangaza viredio vya vichochoroni?
Da Mkuu umenena sana million 600 awe mtangazaji?
 
Mkuu futa kauli kabisa ,Kiukweli MC pilipili kwenye show ya Leo amevunja watu mbavu,Jamaa yupo vizuri sana kwenye stand-up comedy show ya Leo ameitendea Haji....Wasaka Tonge.....Wasanii wa bongo wapo vizuri,tuwatie moyo wanaweza.
Kuna mdogo alikua wa tatu ku perform yuko vizuri sana
 
Afadhali umemwambia maana ni kituko kitupu. Analazimisha lakini wapi
 
Hhuyh jamaa si mchekeshaji na si msanii anaforce kabisi, bongo sijaona coedians kama MPOKI &JOTI
 
Watanzania hatujawahi kuwa na mawazo ya kujenga hasa kwenye suala linalomhusisha Mtanzania mwenzake........siku zote tunapambana kuwarudisha nyuma wale waliotuacha hatua kadhaa mbele......na hii mindset inaanzia ngazi ya familia mpaka taifa kwa ujumla.....

Anachokifanya huyo bwana mdogo sio kila mtu anaweza kukifanya na sio kila mtu atafurahishwa nacho.......

Katika ulimwengu wa burudani kuna vitu vya kufurahisha...kama wewe hufurahishwi na comedy yake.....basi tafuta comedian wengine....acha wanaofurahishwa na comedy yake wampe sapoti.....

Kumbuka anachokifanya ndio kinachomwingizia kipato na kumuendeshea maisha yake....sasa kwanini uharibu maisha ya mtu kwa kuwa tu hupendi anachokifanya....!??

Hiyo kwa rugha nyepes ni ROHO MBAYA.....

b78628632914d310267e78d26907ae50.jpg
 
Back
Top Bottom