Mc Pilipili utanisamehee kwa ukweli huu "huna kipaji cha kuchekesha"

Mc Pilipili utanisamehee kwa ukweli huu "huna kipaji cha kuchekesha"

hivi kumbe huwa ni mchekeshaji?? Dooh mi nkajua mshereheshaji tu.
Kwa kweli kuchekesha hajui bora hata Kanjunju John
 
Ukimlinganisha na stand up comedians wa.Uganda na Nigeria kweli mc pilipili ni Bashite haswaa! Zero!
 
Kuna mambo ya kupeana support na kuna mambo pia ya kuelezana ukweli, siko hapa kumkatisha mtu tamaa ila My Brother Mc Pilipili sanaa ya Uchekeshaji imekupiga Kanzu.
Speed ya standup comedy ilipo na ww unachokifanya ni Kigoma na London.

"Wapaka mafuta kwa mgongo wa chupa hamtakosekana kussuport comedy ya huyu mtu kinafiki,ila kwa mm binafsi,
Lazima tuiite beleshi beleshi na sio kijiko kikubwa. !"

Mc pilipili Ukumbuke tu,si kila anayepiga makofi basi anakupongeza , ukitaka uhakika muulize "Mbu".

WEWE SI MCHEKESHAJI.

AHSANTENI.
Naungamkono 100%binafsi nimejitahidi kumfuatilia sijaona kama mchekeshaji"kifupi mvamia fani..yaani sijuagi hata anawachekesha nini...hata tuseme kweli binadam huwezi pendwa na wote lkn kiukweli pilipili sio mchakeshaji..
 
Wabongo saa ingine wanang'ang'aniza vipaji wasivyokuwa navyo ilmradi tu watengeneze pesa. Kipaji na deal ya kutengeneza pesa haviingiliani. Sana sana badala ya kuchekesha wewe ndiyo utakuwa unajichoresha kwa comedy zisizochekesha.
 
Sijawahi Kumkubali na nadhani nitakuwa wa mwisho kabisa Kumkubali tena kishingo upande. Tanzania nzima ina Wachekeshaji hawa tu....
  1. Mzee King Majuto
  2. Lucas Mhavile a.k.a Joti
  3. Masanja
  4. Kingwendu
  5. Bambo
  6. Mtanga
  7. Mkwere
Waliobaki ' wanajaribu ' tu.
..mpoki
 
Anajaribu tu ila hao Saba ( 7 ) niliowataja hapo juu ndiyo ' Mafundi ' watupu wa ' Uchekeshaji '.
Mkuu kama hata "Mboto, mpoki na "anko K" wa futuhi kwenye list yako hawapo ila kingwendu na bambo wapo basi list yako ni feki!
 
Kuchekesha anajua.Anachotakiwa kufanya ni kubadili vichekesho mara kwa mara.Asirudie hicho hicho mara tatu kwa sababu huwa vinakuwemo kwenye mitandao.
 
Ni kweli ila kuna watu washampokea na vijipesa anajiingizia ivyo ivyo,sasa mpk hapo alipofikia then unataka aache inabidi umpe ajira sio kusema hajui kuchekesha while mfuko unatuna na muda si mrefu ataanza kulipa kodi na kuchangia kijipato cha nchi hii
 
Tanzania ni Nchi ya tatu kwa kutokuwa na furaha duniani kama sijakosea. Hivyo basi sishangai kuona raia hapa wakimponda kila comedian.

Stress + ugumu wa maisha+ serikali ya matukio ni lazima uwe sawa na mtu alietolewa na bandama.
 
Back
Top Bottom