TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

Nimeisoma naomba orodhesha makosa ya Mch Mtikila. Je Lowasa ni magonjwa au sio mgonjwa??? USICHANGANYE ushirikina na neno la Mungu.

Queen Esther
acha kutuletea habari zako za ushambenga hapa! akina magufuli walienda loliondo kwa babu kunywa vikombe vya nini?
 
Jana nilikuwa narudia kuangalia mkanda wa Air Force One nikamkumbuka rais wangu lowasa
 
RIP Mtikila. Saa ya ukombozi ni sasa!
 
Ndiyo maana mimi huwa nina adabu sana. hata mode wanapo delete post zangu huwa siwajibu, namuachiaga Mungu tu.
 
Kwani Mtikila alimuombea nini Lowasa? Acheni hizo. Mtikila alikuwa anasema kweli tupu kuhusu Lowasa. Ndo maana wameamua kumuua

Ukiambiwa uthibitishe hiyo sentensi yako ya mwisho utakua na la kujibu?

Mimi siwezi kufurahia kifo hata kama ni cha adui yangu(isipokua majeshi tena yakiwa vitani).

Ninamuombea Mungu amrehemu ila kama baadhi ya wachangiaji wengine wanavyosema Tusimdhihaki Mungu.

Marehemu alikua ni Mtumishi wa Mungu mwenye cheo cha Uchungaji lakini kwa kauli alizokua anatoa hivi karibuni alipokua akihojiwa kwenye kipindi cha Tuongee asubuhi cha StarTv kuhusu Afya ya EL kiukweli sikuipenda na nilishangaa sana kauli kama zile kutolewa na yeye ijapokua alikua ashazoeleka kwa kauli zake zenye utata tangu kipindi cha Mkapa.

Hivyo basi wito wangu kwa Nape, Mwigulu, Msukuma na wengine wengi tu mnaodhihaki wagonjwa Mungu anaweza kuwapa pigo ambalo hamtalisahau maishani mwenu.

Kifo cha Mtikila ndicho alichokua amepangiwa, kwa bahati mbaya kimetokea mara baada tu ya kauli zake ndio maana wengi humu jamvini wanaona kimetokea kutokana na kweli zake.
 
Afya ni neema na baraka toka kwa Mungu, uhai wa binadam ni siri kubwa Sana ambayo Mungu pekee ndo anajua lini uhai wa mtu utaisha!! Tusimsemee Mungu!!
 
Kama ndivyo.. Mungu ametenda kazi yake poleni sana Watanganyika..

mkuu ajali zote zinaletwa na shetani , analeta ajali halafu anakuchukua.
MUNGU akiweka mkono wake kukulinda basi unapona ndiyo watu wanasema amepona kwa nguvu za MUNGU.
Mimi na mwenzangu tulipata ajali kama hii gari ilipinduka Mara kadhaa mbele iliharibika Sana na upande wa juu kwa abiria.Masaa mawili kabla ya ajali mwenzangu alinikumbusha kufunga mkanda hivyo wakati gari inapinduka mkanda ulitushikilia ikaja kutua kiubavu tukafungua mikanda tukatoka salama bila hata mchubuko wowote.
 
Ivi ajali hiyo haichunguziki???maana aliwai kusema kuna wanyarwand kibao wameingizwa na ka.....,ila Mungu awatie nguvu family yake..japo nae alisema maneno ambayo yaliwakwaz family ya lowasa.siasa si matusi
 
Mtikila rip tangulia tutafata kazi ya mungu haina makosa. Na mungu akusamehe ulioyatenda na kuyasema kwa kukusudia au kwa kutokusudia
 
Hahahahaha mm nacheka tu....Komba alimtukana Warioba akaenda...Mtikila alimtukana Lowassa ameenda...huwezi kujitapa na afya inayotolewa na mungu...Faizafoxxy are u watching
 
Kama wapanga mikakati wakubwa wa Mheshimiwa kwenda ikulu ni aina ya Kina Gwaji.......Mhuuu.!!!
 
Pumzika kwa amani ya Bwana wetu Mchungaji!


Lowasa alipoulizwa kuhusu afya yake na wanaombeza, alijibu kwa huruma na upole, afya yangu mwenyezi MUNGU ndiye anayeijua maana sijui nitafia wapi au kwa njia gani, niwapongeze hao walio wazima milele maana aliyewajalia afya njema ndiye alinipa mimi maradhi, maana wao wataishi milele na mimi nitakufa tuu, ila bado nikiwa na pumzi na uhai huu hata kama nimelala kitandani naugua ugonjwa nitaendelea kuipigania Tanzania. Ikumbukwe mimi nilikuwa nina hii ndoto ya kuwaongoza Watanzania na kuwaondolea umaskini toka Mwaka 1990 na bado ninaamini naweza kuitimiza, cha muhimu sasa ni kila mtu anatafuta kick ya kuaminika zaidi na Wananchi ili wampe kura, tatizo linakuja pale tuu ni njia gani wanaiyoitumia kuomba kura, either kwa kumdhihaki mwingine au wananchi au kwa kutumia sera makini. Kabla ya kampeni na wakati tukifungua kampeni zetu Jangwani nilishasema tutaendesha kampeni swafi zisizo na maneno machafu ya kumdhihaki mtuu.. Kwa hilo nafikiri mpaka sasa nalisimamia vizuri, sikuwahi kumtaja mtu mwingine kwa kumchafua toka nianze kampeni maana ninaamini hao hao tunaopingana nao majukwaani wengine lazima tufanye nao kazi ofisi moja ili kuleta maendeleo kwa Watanzania...



Touch me deeply.... always WISDOM is a good career in Leadership
 
Katika suala la afya ya mtu, naheshimu sana kauli ya busara ya Mhesh. Zitto.Yakwamba hatueezi zungumzia afya ya mtu ktk majukwaa ya kisiasa. Kwasababu afya ni majaliwa ya MUNGU.

Zitto alikuwa anamwambia Habibu mchange maana alimsema vibaya sana kuhusu afya ya Lowassa siku ya uzibduzi hapo ndio Zitto alipokuja kuweka sawa kwamba bwana mdogo amepitiwa.
 
Last edited by a moderator:
Duuuh Mungu anasingiziwa mengi basi tu.
 
Chacha Wangwe
Grace Mbowe
Regia Mtema
Mohammed Mtoi
Christopher Mtikila
??????????????? Loading

The same Modus Operandi. Kweli usishindane na wakaskazini

R.I.P


Akili yako fupi sana!!!!

Hatutarajii kuona ujinga kama huu humu ila kwa kuwa mpo humu lazima mlete!

Pole sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…