Pumzika kwa amani ya Bwana wetu Mchungaji!
Lowasa alipoulizwa kuhusu afya yake na wanaombeza, alijibu kwa huruma na upole, afya yangu mwenyezi MUNGU ndiye anayeijua maana sijui nitafia wapi au kwa njia gani, niwapongeze hao walio wazima milele maana aliyewajalia afya njema ndiye alinipa mimi maradhi, maana wao wataishi milele na mimi nitakufa tuu, ila bado nikiwa na pumzi na uhai huu hata kama nimelala kitandani naugua ugonjwa nitaendelea kuipigania Tanzania. Ikumbukwe mimi nilikuwa nina hii ndoto ya kuwaongoza Watanzania na kuwaondolea umaskini toka Mwaka 1990 na bado ninaamini naweza kuitimiza, cha muhimu sasa ni kila mtu anatafuta kick ya kuaminika zaidi na Wananchi ili wampe kura, tatizo linakuja pale tuu ni njia gani wanaiyoitumia kuomba kura, either kwa kumdhihaki mwingine au wananchi au kwa kutumia sera makini. Kabla ya kampeni na wakati tukifungua kampeni zetu Jangwani nilishasema tutaendesha kampeni swafi zisizo na maneno machafu ya kumdhihaki mtuu.. Kwa hilo nafikiri mpaka sasa nalisimamia vizuri, sikuwahi kumtaja mtu mwingine kwa kumchafua toka nianze kampeni maana ninaamini hao hao tunaopingana nao majukwaani wengine lazima tufanye nao kazi ofisi moja ili kuleta maendeleo kwa Watanzania...
Touch me deeply.... always WISDOM is a good career in Leadership