Clueless14
JF-Expert Member
- Aug 27, 2014
- 3,108
- 4,751
katika Vitabu vitakatifu Mungu amekuwa akitoa ishara nyingi nyingi sana. Na hii leo anasema na Watanzania kwa namna tofauti kabisa ya kuondokewa na mwanasiasa mwenye chachu kabisa katika Siasa za Vyama vingi. Hebu kaa dakika moja mkumbuke Mch.Mtikila, Kumbuka siasa za Mtanganyika, Kumbuka siasa za --------- na mengine mengi.
Mungu anasema kwa ishara mabalimbali kipindi hiki cha uchaguzi, matukio mengi sana yametokea hapa Tanzania na duniani yakitukumbusha sisi ni mavumbi tu. Nikipindi ambacho Tunakumbushwa kurudi Miskitini na makanisani kusiliza sauti ya Mungu na kuzitambua ishara hizi kwa unyeyekevu mkubwa. Mungu anatukumbusha kujali maskini,Watu wenye njaa, na wagonjwa mbalimbali. Mungu anatukumbusha si kwa akili zetu tumepata dhamana kuliongoza taifa hili bali yeye mwenyewe ndio kafanya yote haya.
Mungu anatukumbusha Gas Mafuta na madini ni mali yake na vitumie kwa utukufu wake kwa kuhudumia watu wenye mahitaji zaidi. Mungu anatukumbusha Mikataba ya madini/Gas iwekwe wazi ili iwafikie walengwa wake. Mungu anatukumbushaTuache rushwa na ufisadi,Tutubu zambi zetu na Tujenge taifa kwa kizazi kijacho.
Mungu ameota ishara hizi ila kila mwanadamu apate kumjua yeye ndie Mungu Muumba wa Taifa hli.
1.Lowassa Kuhama CCM
2.Magufuri kuwa Mgombea Urais
3.Lipumba Kuacha siasa
4.Dr Slaa kuacha Siasa
5.Halima mdee na Mbatia kwenye Jukwaa moja.
6.Tanzania kuwa giza wakati wa uchaguzi
7.Vyama vinne kusimamisha mgombea
8.Rais kupiga campaign
9.Hotuba za Nyerere kutamba katika jukwaa la upinzani.
10.Kwa mara ya kwanza Watanzania hawajui nani atashinda uchaguzi.
11.Campaign bila kept.Komba.
ukiangalia kwa mbali utaona ni vitu vidogo sana lakini ukirudi utakuta mabadiliko makubwa sana katika radha ya siasa za Tanzania. kwa ujumla kifo cha mtikila ni pigo zito sana katika radha ya siasa ya vyama vingi. R.I.P
Halafu wee kama nakufahamu vile...
Arusha member? Umesoma arusha sec?
