TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

Kweli Lowassa Mungu anamlinda sana. Wansomdhihaki kuhusu afya yake ndo wanatangulia. Mungu ni mwema!

Hivi akili gani hizi? Yaani Mchungaji Mtikila kauwawa na Mungu gani huyu wa ajabu? Kweli mnahitaji reality check! Mnapoandika ujinga kama huu ndo mnazidi kupoteza mvuto! Eti Mungu!
 
Wataalam wa mambo ya uchaguzi, katiba inasemaje endapo mgombea wa kiti cha urais ATAFARIKI siku chache kabla ya uchaguzi?
 
Wakuu,

Kuna taarifa kwamba Mchungaji Christopher Mtikila amepata ajali ya gari mkoani Pwani alfajiri ya leo, taarifa zaidi tunasubiria kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani humo.

=====
UPDATE:

JamiiForums imeongea na Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema amefariki saa 12 kasorobo asubuhi katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.

Amesema gari lililokuwa limempakia lilikuwa linatokea Morogoro na kwamba walikuwa watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya.

Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya Tumbi.

picha yake hiyo chini
 
Kumbuka enzi za wana wa israel ktk safari yao kutoka misiri,,,, waliokuwa wakienda kinyume na mapenzi ya Mungu walipewa adhabu papo, hapo.... Kwa hiyo ,,,, na hili usilishangae Mungu wetu hadhihakiwi hata kidogo
chinembe ni mungu yupi huyo????? Mungu ni wa rehema na hataki hata mmoja apotee.

Kama huyo mungu wa lowasa anaua kila atakayemsema basi atauwa watu wengi sana. Lile kusudi la kazi ya msalaba litakuwa limefitinika.

Bwana wetu yesu kristo alifanyiwa kila namna ya uovu akasema baba wasamehe hawajui wafanyalo. Huyo mungu wa kulipiza papo kwa papo !!!!!!! Mh!!!!! Wapi kazi ya msalaba???

Damu zilizomwagika hata sasa kama ni mapenzi ya mungu zitaenda kwa amani. Kama ni umafya na ushirikina basi tegemeeni kisasi cha bwana.

Queen esther
 
kama ni hivyo watadondoka wengi maana wengi wamemtukana sana Bw Lowassa.

Tutashuhudia mengi. Mungi hadhihakiwi na ameshaanza kuthibitisha hilo...

Haha,duh...kafa kabla ya Lowassa?Mungu hadhihakiwi

Mungu hapendi mzaha kwani yeye ndiye humpa mja wake afya na maradhi kwa hiyo basi kifo chake ni fundisho kwa wengine km akina Mwigulu et el.

Mungu ni mkubwa kuliko mmbuyu!

Duh...kafa kabla ya Lowassa?Mungu hadhihakiwi

Kweli Mungu hadhihakiwi kama kuna Ukweli katka hili.

Hivi huwa mnaandika kwa kufikiria? au mhimeko?

Mungu angekuwa anawaadhibu watu kutokana na dhambi zao hapo hapo nani angepona??

au huyu wenu ni Mungu yupi?
 
Kwa kuua wengine? Mungu wa Lowassa yuko hivo?
Mwanzo 38:7. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; na BWANA akamwua.

Uwe unasoma maandiko wewe, BWANA MUNGU anaweza kuuwa na anaweza kuhuisha.
 
Mhuuuuu jamani hata kama aliwah kukukosea MTU akifa tofauti zetu tunaweka pembeni[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] mhuuuu
 
Ndio Muache kumtukana Mungu akimtukana mgonjwa mmoja umewatukana wagonjwa wote. Na hao wagonjwa kila siku wanapiga goti kwa Mungu ambaye ndio.mtoa afya na uzima kwa wote so jamani chungeni midomo yenu
 
Chinembe ni Mungu yupi huyo????? Mungu ni wa rehema na hataki hata mmoja apotee.

Kama huyo Mungu wa Lowasa anaua kila atakayemsema basi atauwa watu wengi sana. Lile kusudi la kazi ya msalaba litakuwa limefitinika.

Bwana wetu Yesu Kristo alifanyiwa kila namna ya uovu akasema Baba wasamehe hawajui wafanyalo. Huyo Mungu wa kulipiza papo kwa papo !!!!!!! Mh!!!!! Wapi kazi ya MSALABA???

Damu zilizomwagika hata sasa kama ni mapenzi ya Mungu zitaenda kwa AMANI. Kama ni umafya na ushirikina basi tegemeeni KISASI cha Bwana.

Queen Esther

Kumbe wafahamu kuhusu Kisasi cha Bwana halafu unauliza ni Mungu yupi huyo? Unasahau kuwa Uzima ama Mauti uu Mikononi mwa Mungu Muumba Mbingu na Nchi? Umesahau kwamba Kile Apandacho Mtu ndicho atakachovuna? Umesahau neno linalosema Usihukumu usije Ukahukumiwa? Uhai ni wa Mungu na Si wa Kina Komba, Cellina Kombani, Mtikila, et al kiasi kwamba Wamuite Mwenzao Marehemu ilihali hata Sekunde Moja mbele yao hawajui kitakachotokea? Je! Huoni kuwa kuna la kujifunza katika hili? Muogopeni Mungu, licha ya kuwa ni Mwingi wa Rehema, lakini pia Hadhihakiwi kamwe!
 
hakuna aijuaye kesho yake yule aliyesema ni mgonjwa bado yu hai. hakika mungu ni wa wote.
Mungu ni mkuu kuliko kitu chochote hapa duniani.

Hamshangai huyu wanayemwita mgonjwa anaendelea kudunda na kila siku anafanya mikutano ya kampeni isiyopungua mitatu.

Hata hivyo mbona hawashangai Rais tuliye naye ambaye alidondoka jukwaani wakati anamalizia kampeni zake mwaka 2005?

Lakini pamoja na ugonjwa wake wa 'kudondoka' mara kwa mara majukwaani, Mungu wetu mkuu amemuwezesha kumaliza salama vipindi vyake vyote viwili vya utawala vya miaka 10.
 
Back
Top Bottom