Ghosryder
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 10,403
- 4,373
Ukiambiwa uthibitishe hiyo sentensi yako ya mwisho utakua na la kujibu?
Mimi siwezi kufurahia kifo hata kama ni cha adui yangu(isipokua majeshi tena yakiwa vitani).
Ninamuombea Mungu amrehemu ila kama baadhi ya wachangiaji wengine wanavyosema Tusimdhihaki Mungu.
Marehemu alikua ni Mtumishi wa Mungu mwenye cheo cha Uchungaji lakini kwa kauli alizokua anatoa hivi karibuni alipokua akihojiwa kwenye kipindi cha Tuongee asubuhi cha StarTv kuhusu Afya ya EL kiukweli sikuipenda na nilishangaa sana kauli kama zile kutolewa na yeye ijapokua alikua ashazoeleka kwa kauli zake zenye utata tangu kipindi cha Mkapa.
Hivyo basi wito wangu kwa Nape, Mwigulu, Msukuma na wengine wengi tu mnaodhihaki wagonjwa Mungu anaweza kuwapa pigo ambalo hamtalisahau maishani mwenu.
Kifo cha Mtikila ndicho alichokua amepangiwa, kwa bahati mbaya kimetokea mara baada tu ya kauli zake ndio maana wengi humu jamvini wanaona kimetokea kutokana na kweli zake.
Kabla hujachangia uliona comments za wana UKAWA humu walivyopokea taarifa za kifo cha Mch Mtikila kwa furaha? hilo lazima lilete shaka na maswali.