Mch. Kenan Mwasomola umeongea kweli suala la muziki Kanisani

Sisi wazee wa masebene Huwa tunasikiliza sawa tu nyimbo za werrason,wenge,fellegola.
 
Bora warudi tu kwenye tenzi za rohoni huku kwenye secular music Wakristo wamechemka
 
Yah sure man.
mimi nilikuaga sijui inakuaje mtu anasali analia machoz kabisa.wanaita kuabudu.

siku moja niliingia kanisa moja hiv la kilokole kwa mazabe tu nikakutana na ibada yenye utulivu wa kiwango sana.

sasa hapo huo muda kuabudu, wanaimba taratiibuu kwa kumaanisha sana nikajikuta kama nakosa controll ya akil yangu kuhusu nini ninafikiri. Nikajikuta akil inanipitisha kwenye matukio ya maisha yangu ambayo kiuhalisia niliponyoka kwenye hatar kadha wa kadha katika namna ya ajab ajab sana. Nikajikuta hayo matukio yanapita yanapita kwa kas sana na kujirudia halaf ni kama ndio nikawa najua sasa kuwa kulikua na third part intervention nyuma yake..

Hata sikujua what was happening, nilikuja shtuka nimepiga magoti nalia machozi naongea lugha ambayo hata sielewi nahis ndio huko kunena kwa lugha sijui. Basi bwana ile experience ikanipa utulivuuuu sana wa nafsi but sikujua what was happening.

So mimi mpaka leo huwa nakaa kimyaa nikiona watu wanawatukana walokole kuwa wanalia lia.😂😂.
Heb Donatila njoo nipe majibu mkuu
 
Aliyeanzisha music wa rap ndie aliyeanzisha haya makanisa ya kufokafoka
 
Angalau Wakatoliki na wasabato waliona haya wakaamua kusimamia kwenye tunes na codes zao za uimbaji.
Kuepukaa kuingiza disco kanisan.
ajabu yake sasa, hata hao nao hawamwabudu Mungu wa kweli, kwasababu wanamwabudu kimwili. kutulia tunakosema sio kule kwa kunyenyekea kimwiliiiii, kama umemwagiwa maji. ni kutulia kulikochanganywa na Roho Mtakatifu. abudu yako yote wewe ni bure kabisa kama haijahusisha Rogo Mtakatifu, omba yako ni bure, hubiri yako ni bure na chochote unachofanya ni bure kwenye ibada kama hauhusishi Roho na umwone kabisa uwepo wake. hao uliowataja hawana imani ya kujazwa na kuishi na Roho Mtakatifu na hapo ibada zao zooote zinakuwa makosa, wanapoteza muda ndio maana hawawezi hata kuweka mkono juu ya mtu akapata afya kama Yesu alivyoelekeza tufanye. manake hawana nguvu hizo, muwezeshaji wa nguvu kwao hayupo (Roho Mtakatifu), wamemkataa na wanamwita kunena kwa lugha ni fujo na ni ushetani, kumbe wamekosa kitu cha maana kuliko vyote kwenye Ukristo. bila yeye hatuwezi kufanya lolote, hata kwenye maombi ni yeye anatuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, akilia aba yaani baba. waliowahi kufikwa na hayo wanajua ninachoongea.

usabato ulianzishwa na elen white aliyeleta predictions nyingi sana za uongo kuhusu siku za mwisho, na kuwafanya watu waabudu kimwili wakiamini wanaweza kushinda dhambi kwa kufuata sheria ambayo Yesu Kristo alikuja kuitimiliza kwa uwepo wa moyoni wa kuishinda dhambi. tunaishinda dhambi sio kwa kusoma kitabu cha sheria wala kukikariri, dhambi tunaishinda kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu ambaye ndiye anatakiwa kutuongoza kututia kwenye kweli yote. ndio maana hata Yesu alisema huyo msaidizi atakapo kuja, ...atawatia kwenye kweli yote, ..., n.k.

ukija kwa wakatoliki, wamepotea kabisa. kanisa katoliki lile la mitume, sio hili la sasa. hapo katikati lilishachakachuliwa, shetani alifanikiwa kulichakachua wamebaki tu wanaabudu dini na masanamu. nasema hivi kwasababu Kanisa la kwanza la mitume, hawajawahi kuabudu maria wala kumkuza. pia, Neno la Mungu linasema, Yesu Kristo alikuwepo tangu mwanzo, hata kabla maria hajakuwepo Yesu alikuwepo, alishuka tu hapa kama reincanation ya kufanyika mwili ili atukomboe. na alitoa maagizo kwamba, tuombe kwa kutumia Jina lake Yesu, hata kuokoka tunaokoka kwa Jina lake, bila hivyo unapoteza muda. wakatoliki wanaomba na kumwabudu maria na wafu wengine. wanaamini wafu waliokufa wanaweza kuwaombea huko waliko. pia wanaamini wanaweza kuomba kwaajili ya mtu aliyekufa katika dhambi akatakasika huko aliko. huo ni uongo. baada ya kifo ni hukumu. ndio maana unatakiwa kuokoka na kutengeneza maisha sasa, Mungu atusaidie.

chukua maisha ya Petro yule wa kitabu cha Matendo, stephano, Paulo na mitume wote, linganisha na kanisa hili la kina Pengo, halafu sema kama hili ni kanisa la mitume au mnapoteza tu muda. Biblia inasema pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo, mmepata bure toeni bure. enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili, aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa, na ishara hizi (alizozifanya Yesu) zitaambatana na hao waaminio, kwa Jina langu watatoa pepo, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya, watasema kwa lugha mpya (kunena kwa lugha ambako wasabato na wakatoliko wanapinga).

kwa mistari hiyo hapo juu, chukua padre au askofu mmoja tu au hata kadinari au hata Papa mwenyewe, mwambie, Yesu alisema tuweke mikono juu ya mgonjwa naye atapata afya, au tutoe pepo. naomba papa au padre fanya kama Yesu alivyoagiza tuone inatokea nini. nakuhakikishia atakimbia na hiyo sio imani yake.
 
Mbona wanatoa mapepo tembelea vituo vya Emmaus,au kwa wakatecumen.
 
mtu kusali analia kuna mambo mengi. kwanza, anaweza kuwa analia kwa uchungu, pili anakuwa kama anadeka mbele za Mungu, ila Tatu, anaweza kuwa analia kwa Roho Mtakatifu. Ukiokoka, Mungu atakupatia nguvu zake yaani Roho wake Mtakatifu akae ndani yako, huyo kama ndio anaomba kwa kunena kwa lugha, hata hautajipendea utajikuta tu umetoa machozi. hata mimi huwa natoa machozi, na sio dhambi, na nikimaliza najisikia amaniiii, furahaaa, nguvuuu za Mungu na mambo mengi yanakuwa yamejibiwa. hilo wala lisikutie shaka. usishindwe kwenda church nzuri kwa kuogopa kulia, kwa Roho huwa tunalia. Neno la Mungu linasema,

Rum 8:26-30 SUV​

Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.

Wagalatia 4:6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.
 
Mambo yote ni TEC tu.
 
Ulitarajia nn ,makanisa ambayo mahubiri yake yanamtaja shetani kuliko Malaika wezake ,kama yesu na mungu

Shetani /lusifa apewe Maua yake
 
Nashukuru tupo pamoja kwenye hoja ya Mwanzo ya Mch Kenan Mwasomola kuhusu makelele ya muziki na uimbaji wa fujo ndani ya kanisa. Kuhusu hiyo ya wanaohubiri barabarani nikujibu kama hivi:-
1. Je ni haki au sio haki kuwaondoa wamachinga waliopanga bidhaa zao mabarabarani? Maana naona wanafukuzwa
2. Je ni kwanini wamachinga wafukuzwe barabarani na ndani ya stand.
3. Iwapo kila mtu atapata uamsho na kuamua kununua spika na kuweka popote iwe barabarani au stand nk , je waachwe tu kwakuwa wanafanya kazi ya bwana.
4. Je lengo la hao wanaohubiri barabarani na stand ni la kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mbinguni au ni KUKUSANYA MAOKOTO? Najua hapa utakimbilia kusema nisihukuma lakini niseme tu kuwa hata Biblia imesema Mtawatambua tu kwa matendo yao na mwenye macho anaona.
5. Je ni kwanini nchi nyingi duniani zimeweka utaratibu na unafuatwa , kama ni mahubiri basi yanafanyika lakini sio kiholela kama huku kwetu ambapo hata mtu aje kuweka spika getini kwako unaona ni sawa tu.

TUMEKUWA WAJINGA SANA KATIKA KUITAFSIRI IMANI NA KUYATAFSIRI MAANDIKO NA NDIO MAANA KUMEKUWA NA UHOLELA KWA KILA KITU.
 
Mbona wanatoa mapepo tembelea vituo vya Emmaus,au kwa wakatecumen.
Halafu hii hoja ya kutoa mapepo ndio walokole wameikamatia sana. Yaani watu wanaamini kuwa watu wana mapepo na yanatolewa, KWAKWELI SISI NI MBUMBUMBU SANA. Ni nani anyeweza kuthibitisha kuwa fulani alikuwa na pepo, huyo pepo yukoje. Yaani NI SANAA TU ZINAENDELEA na sababu ya umaskini na taabu tulizonazo katika maisha, familia, kazini, ndoa, magonjwa basi mtu akiambiwa ana mapepo naye anakubali.
Leo hii ni matukio ya uponyaji yasiyokuwa na ushahidi ndio yanatangazwa, utasikia fulani alikuwa na viwembe tumboni, chupa mgongoni . Lakini kipindi cha kina Elia na Elisha na kipindi cha Yesu ukiambiwa fulani kaombewa na kuponywa basi jamii nzima inakuwa haina shaka KWASABABU ALIYEPONYWA NI MTU ALIYEKUWA ANAJULIKANA NA JAMII NZIMA KUWA NI KIZIWI AU KIPOFU AU KICHAA WA MIAKA NA MIAKA.
Leo hii tunapewa ushuhuda na mtu mwenyewe ambaye hakuna anayejua kama kweli alikuwa na shida au ugonjwa.

Waafrika tumekuwa maskini wakubwa SANA wa FIKRA
 
Lutherani na Anglikana ni suala tu la muda, na wenyewe watakuwa wanacheza Ndombolo ya solo kwenye Makanisa yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…