nakubaliana na wewe, style ya miziki ya kidunia makanisani katikati yake huwa kuna kashetani wanacheza pamoja. wao huwa wanachukulia ile kwamba hata Daudi alicheza hadi nguo zikamdondoka lakini hawafikirii kwamba Daudi alipocheza alikuwa anaonyesha hisia za furaha tu haikua kumwabudu Mungu kwa kucheza vile. research imeonyesha Mungu hawawahi kuonekana mahali penye makelele ya aina hiyo, mara huku limdundo la ajabu ajabu, mara huku mtu anaomba kwa kupayukaaaaa tena kwa maneno ya kiswahili kabisa (yangekuwa maneno ya kunena kwa lugha tungeongea mengine), mpo kwenye uwepo mara mwingine analeta linyimbo la ajabuajabu, shida tupu.
Mungu huwa anapatikana kwenye utulivu, hata abudu yako inatakiwa kuwa ya utulivu, ya ndaniii ya moyo wako, kwenye kilindi cha moyo wako. Yesu aliwaambia kuwa, usalipo ingia ndani, funga mlango, sali kwa moyo wako toka kilindini na Mungu wako atakusikia. labda uwe uanfanya maombezi ndio uanwez akupayuka payuka kwasababu unakuwa unaamuru, though hata kuamuru nako sio lazima upayuke kama una nguvu za Mungu hata uwepo wako tu sehemu ni threat kwa shetani vya kutosha.
nisiongee mengi sana, naomba nikujibu suala la watu kuhubiri ovyo mitaani. hapo umekosea, hao watu wanafanya la maana sana, ninyi mlioko makanisani sio tu ndio mliotumwa kuhubiri. ofcourse tunatakiwa kuhubiri kila mahali as long as you have a breath, hubiri. mitandaoni hubiri badala ya kuleta critics kama hizi, ulitakiwa uhubiri. Mungu akukipatia speaker nenda barabarani kahubiri, hata akiokoka mtu mmoja tu ni wa thamani kwa Mungu. tangu umekalisha mwili wako kwenye kiti hauhubiri unajua ni wangapi wamepotea kwa uvivu wako na kujifanya mstaarabu ati usihubiri mitaani na mabarabarani? unasema uhuru umekuwa mwingi ungependa watu wazuiwe kuhubiri mitaani? hujui unachokisema na Mungu akusaidie.