Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kila kitu mnacholetewa hata kikiwa chema mtataka muongeze chumvi. Hata suala la Demokrasia mlipoletewa na watu wa Ulaya basi nyie mkaamua kuongeza chumvi kwa kisingizio cha democracy, NDIO MAANA HATA WANAOPANGA BIASHARA BARABARANI WANAPOONDOLEWA MNAWATETEA, Nakumbuka hata wale wakazi wa jangwani kwenye mafuriko mliwatetea kuwa wasiondolewe.Kila watu wanamuimbia Mungu kulingana na tamaduni zao. Unataka Waafrika waimbe kama waitaliano? Unafikiri wayahudi walipokuwa wanamuimbia Mungu walikuwa wanaimba kama wakazi wa Roma? Tuachwe kushikwa akili.
Hao sio wakristo ,wapinga Ukristo.Ni kikundi cha Shetani kupotosha Ukristo.Wanasema Yesu hakufa ,yule aliyekufa ni mwingine.Yesu Mungu alimtwaa hivyo Yesu hakufufuka maana hakufa.Wanakataa kiini wa wokovuMimi pia Lutheran ila daima nitawapenda mashahidi wa yehova
Zinaamsha mori na kuongeza ari kwa waumini wamsifu bwana kwa nguvu pia kuwavutia wasiopenda kuabudu waweze kuhudhuria kwa wingi.Hakuna mziki, mdundo au melody rasmi ya asili ya kanisani. Mitindo, midundo au melody zote za nyimbo ni ni vionjo vya kitamaduni, kiasili na mitindo ya kijamii. Wanajamii husika ndio huvileta kanisani.
Melody za nyimbo za kiroma ni matokeo ya melody za kitamaduni za asili kule Roma, ndio kitu hicho hicho kipo Lutheran ambapo ni melody za kitamaduni za kijerumani nk.
Wakristo wa India wataimba na kucheza kwa style za kitamaduni za kihindi.....
Wakristo wa China wataimba na kucheza kwa style za kitamaduni za kichina.....
Tatizo sio style kuanzia duniani na kuzikuta kanisani, tatizo hizo style zinamrudishiaje Mungu utukufu huko makanisani zikiimbwa na kuchezwa.
Ukitaka kumuabudu Mungu kihalisia uimbe na kusali Kiebrania. Achana na magitaa na vinanda, piaga Tari/dufu. Waroma au Wasabato wa Marekani wana uhalisia gani?Kila kitu mnacholetewa hata kikiwa chema mtataka muongeze chumvi. Hata suala la Demokrasia mlipoletewa na watu wa Ulaya basi nyie mkaamua kuongeza chumvi kwa kisingizio cha democracy, NDIO MAANA HATA WANAOPANGA BIASHARA BARABARANI WANAPOONDOLEWA MNAWATETEA, Nakumbuka hata wale wakazi wa jangwani kwenye mafuriko mliwatetea kuwa wasiondolewe.
SISI NI WAJINGA SANA NA LIMBUKENI.
Ndio maana mnaina ni sawa mtu kuhubiri popote eti anafanya kazi ya bwana. Nakumbuka hata Arusha kuna kanisa walifunga barabara sababu ya kutembea wakiwa wamevaa magunia ya kujutia Zambia zao. Ilikuwa kutoka njia ya mbauda hadi Kibo.
Hivi mnajua huko duniani kwa wenzetu wanaojielewa huwezi kukuta uholela kama huu. Wao wanamuabudu sana Mungu lakini wameweka utaratibu na mipaka na sio tu aamue kukaa service road au stand na spika nakuanza kuhubiri.
Tufanyeni kazi ya Bwana katika uhalisia na utaratibu
Hata wazungu Wanaombewa mapepo.Halafu hii hoja ya kutoa mapepo ndio walokole wameikamatia sana. Yaani watu wanaamini kuwa watu wana mapepo na yanatolewa, KWAKWELI SISI NI MBUMBUMBU SANA. Ni nani anyeweza kuthibitisha kuwa fulani alikuwa na pepo, huyo pepo yukoje. Yaani NI SANAA TU ZINAENDELEA na sababu ya umaskini na taabu tulizonazo katika maisha, familia, kazini, ndoa, magonjwa basi mtu akiambiwa ana mapepo naye anakubali.
Leo hii ni matukio ya uponyaji yasiyokuwa na ushahidi ndio yanatangazwa, utasikia fulani alikuwa na viwembe tumboni, chupa mgongoni . Lakini kipindi cha kina Elia na Elisha na kipindi cha Yesu ukiambiwa fulani kaombewa na kuponywa basi jamii nzima inakuwa haina shaka KWASABABU ALIYEPONYWA NI MTU ALIYEKUWA ANAJULIKANA NA JAMII NZIMA KUWA NI KIZIWI AU KIPOFU AU KICHAA WA MIAKA NA MIAKA.
Leo hii tunapewa ushuhuda na mtu mwenyewe ambaye hakuna anayejua kama kweli alikuwa na shida au ugonjwa.
Waafrika tumekuwa maskini wakubwa SANA wa FIKRA
Nyie ndio Mungu,mbona mnamsemea!?Tukiimba katika Roho na kweli hapo hamna kelele.Kelele ni kupuyanga pasi na Roho wa Mungu hivyo hata nyie mnaojinasibu kuimba kwa codes gani sijui...kama moyo sio safi ni makekele tu.sahihi kabisa. hata Mungu hawezi kuongea na wewe kwenye makelele na unarukaruka kama bongo fleva. ni heshima gani unasogea nayo kwa Mungu? lazima uende kwa kutulia, kwa unyenyekevu na kwa kutoka kilindini cha moyo wako. kweli utakuwa kilindini cha moyo kwa kuruka kama hamonize? sebene sijui disco la yesu hata sijui ni yesu gani wanamsema huyo.
mashahidi wa yehova sio wakristo, ni wapagani kabisa na hawatafika mbinguni, ni motoni moja kwa moja.
binafsi sio mhusika wa kuimba kwa codes. ninachosema, uimbaji wa vurugu sawa tu na manyimbo hayo ya dunia, haupo kwenye abudu yeyote kwenye historia ya Biblia. hakuna mtu aliwahi kuabudu Mungu kwa namna hiyo. hata Daudi alivyocheza kwa kuvua nguo na kuruka mbele za watu, hakuwa anafanya hivyo kuabudu, alikuwa ana express feelings za furaha yake tu. tutajie mtu mwingine aliyewahi kumwendea Mungu akiabudu kwa namna hiyo mnayoifanya ninyi. hayupo. mnapenda sana kuifuatisha namna ya dunia hii, mnacopy vitu vya dunia ili kuvifanya kwa Mungu as if Mungu hawezi kuanzisha cha kwake. Huwezi kumwendea Mungu bila unyenyekevu na utulivu. you should always be still and know that he is God. hapo ndipo atajidhihirisha kwako. tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, mnapoteza muda na hiyo sio abudu ambayo Mungu anaihitaji. Mungu sio binamu yenu.Nyie ndio Mungu,mbona mnamsemea!?Tukiimba katika Roho na kweli hapo hamna kelele.Kelele ni kupuyanga pasi na Roho wa Mungu hivyo hata nyie mnaojinasibu kuimba kwa codes gani sijui...kama moyo sio safi ni makekele tu.
Ustaarabu ni kutokosoa imani usiyoishiriki.Hukubaliani lkn kuwa na staha fanya yako.
shida ninayoiona kwako sio utaratibu wa machinga au mahubiri. shida yako wewe ni wokovu, hutaki kuhubiriwa, una kashetani ndani yako kanakokerwa na Mahubiri. kimbia haraka upone, nafasi bado ipo kabla mlango haujafungwa.Nashukuru tupo pamoja kwenye hoja ya Mwanzo ya Mch Kenan Mwasomola kuhusu makelele ya muziki na uimbaji wa fujo ndani ya kanisa. Kuhusu hiyo ya wanaohubiri barabarani nikujibu kama hivi:-
1. Je ni haki au sio haki kuwaondoa wamachinga waliopanga bidhaa zao mabarabarani? Maana naona wanafukuzwa
2. Je ni kwanini wamachinga wafukuzwe barabarani na ndani ya stand.
3. Iwapo kila mtu atapata uamsho na kuamua kununua spika na kuweka popote iwe barabarani au stand nk , je waachwe tu kwakuwa wanafanya kazi ya bwana.
4. Je lengo la hao wanaohubiri barabarani na stand ni la kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mbinguni au ni KUKUSANYA MAOKOTO? Najua hapa utakimbilia kusema nisihukuma lakini niseme tu kuwa hata Biblia imesema Mtawatambua tu kwa matendo yao na mwenye macho anaona.
5. Je ni kwanini nchi nyingi duniani zimeweka utaratibu na unafuatwa , kama ni mahubiri basi yanafanyika lakini sio kiholela kama huku kwetu ambapo hata mtu aje kuweka spika getini kwako unaona ni sawa tu.
TUMEKUWA WAJINGA SANA KATIKA KUITAFSIRI IMANI NA KUYATAFSIRI MAANDIKO NA NDIO MAANA KUMEKUWA NA UHOLELA KWA KILA KITU.
Shida sio hivyo vyombo, hapo tatizo ni wapigaji. Kila aliyeshika chombo anataka kisikike zaidi ya mwezie ndio maana badala ya kupata mziki uliopangiliwa unasikia makelele tu.Sina sababu ya kuelezea ila mimi moyoni nilikataaa yale ma drum na mangoma ngoma kuwepo kanisani.