Mch. Kenan Mwasomola umeongea kweli suala la muziki Kanisani

Wakiambiwa kweli wanakimbilia kutukana waislam
 
La kuhusu wahubiri wa mitaani nakuunga mkono.. imeandikwa siku za mwisho injili itahubiriwa KILA pahala... "Ili siku ya hukumu ikifika, usiseme sikusikia.. maana Mungu atakukumbusha.. ulivyo kuwa pale stand nyegezi au jamatini au Makumbusho hukumuona yule mtu alikuwa napayuka na ukamcheka au unaona aibu?" Hapo mwanadamu atakosa majibu na ataanza kuhaha!......
 
ameshindwa kuhubiria waamini wake kanisani kwakwe anahubiri makanisa ya wenzake
 
Maadili yamebaki kwa wakatoliki na wasabato
 
To each their Own...,

Unaweza kuwaambia kina Robert Nesta Marley na Peter Tosh kwamba Reggae ni Mziki wa Kidunia ?

Tusianze kupangiana maisha hata hizo dini / imani ukiongea na Mababu zetu watakwambia ni za kidunia...
 
Siku hizi wamegawanyika eti! Kuna High Church na Low Church. Hao High Church nadhani ndiyo hao Walokole mamboleo.
High church wapo na taratibu kam za katoliki kwa mbaaali ila low ndo wenye amsha amsha ambayo ndo mambo leo
 
High church wapo na taratibu kam za katoliki kwa mbaaali ila low ndo wenye amsha amsha ambayo ndo mambo leo
Ok!! Basi hao low church ni majanga kweli kweli. Wanakoelekea ni kutoka kabisa kwenye ule utaratibu wa zamani wa Kanisa.
 
Kila watu wanamuimbia Mungu kulingana na tamaduni zao. Unataka Waafrika waimbe kama waitaliano? Unafikiri wayahudi walipokuwa wanamuimbia Mungu walikuwa wanaimba kama wakazi wa Roma? Tuachwe kushikwa akili.
 
Hakuna mziki, mdundo au melody rasmi ya asili ya kanisani. Mitindo, midundo au melody zote za nyimbo ni ni vionjo vya kitamaduni, kiasili na mitindo ya kijamii. Wanajamii husika ndio huvileta kanisani.

Melody za nyimbo za kiroma ni matokeo ya melody za kitamaduni za asili kule Roma, ndio kitu hicho hicho kipo Lutheran ambapo ni melody za kitamaduni za kijerumani nk.

Wakristo wa India wataimba na kucheza kwa style za kitamaduni za kihindi.....
Wakristo wa China wataimba na kucheza kwa style za kitamaduni za kichina.....


Tatizo sio style kuanzia duniani na kuzikuta kanisani, tatizo hizo style zinamrudishiaje Mungu utukufu huko makanisani zikiimbwa na kuchezwa.
 
Umejieleza kwa hisia sana mkuu, inaonyesha ni kwanamna gani umekereka.
waumini wengi hivi sasa wamefanya mahubiri (neno la Mungu)kuwa ajira yakuwaingizia kipato hivyo wanachozingatia ni namna ile itakayowaingizia pesa na sio namna watu watakavyolipokea neno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…