Mch. Kenan Mwasomola umeongea kweli suala la muziki Kanisani

Ukisema utaambiwa mbona Daudi alicheza mpaka mavazi yakaanguka...

Ikumbukwe Shetani alikuwa ni Malaika Mkuu wa Sifa...

Hivyo si ajabu akawateka waimbaji wa kusifu na kuabudu wakaifanya kazi yake ..
 
Kila watu wanamuimbia Mungu kulingana na tamaduni zao. Unataka Waafrika waimbe kama waitaliano? Unafikiri wayahudi walipokuwa wanamuimbia Mungu walikuwa wanaimba kama wakazi wa Roma? Tuachwe kushikwa akili.
Kila kitu mnacholetewa hata kikiwa chema mtataka muongeze chumvi. Hata suala la Demokrasia mlipoletewa na watu wa Ulaya basi nyie mkaamua kuongeza chumvi kwa kisingizio cha democracy, NDIO MAANA HATA WANAOPANGA BIASHARA BARABARANI WANAPOONDOLEWA MNAWATETEA, Nakumbuka hata wale wakazi wa jangwani kwenye mafuriko mliwatetea kuwa wasiondolewe.

SISI NI WAJINGA SANA NA LIMBUKENI.

Ndio maana mnaona ni sawa mtu kuhubiri popote eti anafanya kazi ya bwana. Nakumbuka hata Arusha kuna kanisa walifunga barabara sababu ya kutembea wakiwa wamevaa magunia ya kujutia Zambi zao. Ilikuwa kutoka njia ya mbauda hadi Kibo.

Hivi mnajua huko duniani kwa wenzetu wanaojielewa huwezi kukuta uholela kama huu. Wao wanamuabudu sana Mungu lakini wameweka utaratibu na mipaka na sio tu aamue kukaa service road au stand na spika nakuanza kuhubiri.

Tufanyeni kazi ya Bwana katika uhalisia na utaratibu
 
Mimi pia Lutheran ila daima nitawapenda mashahidi wa yehova
Hao sio wakristo ,wapinga Ukristo.Ni kikundi cha Shetani kupotosha Ukristo.Wanasema Yesu hakufa ,yule aliyekufa ni mwingine.Yesu Mungu alimtwaa hivyo Yesu hakufufuka maana hakufa.Wanakataa kiini wa wokovu

1 Wakorintho 15:14-17
[14]tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.
[15]Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
[16]Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.
[17]Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.
 
Zinaamsha mori na kuongeza ari kwa waumini wamsifu bwana kwa nguvu pia kuwavutia wasiopenda kuabudu waweze kuhudhuria kwa wingi.
 
Ukitaka kumuabudu Mungu kihalisia uimbe na kusali Kiebrania. Achana na magitaa na vinanda, piaga Tari/dufu. Waroma au Wasabato wa Marekani wana uhalisia gani?
 
Hata wazungu Wanaombewa mapepo.
Dini inaponya magonjwa ya kiroho yanayoonekana kupitia Tabia mfano, umalaya,uteja,ulevi,wizi,ushoga, hasira,laana na mikosi, hofu na mashaka na Tabia zote chafu.
Hospital Haina uwezo wa kuponya magonjwa ya tabia tajwa ambae chanzo chake ni mchafuko wa roho na nafsi.
Uthibitisho wa uponyaji ni baada ya watu kuacha Tabia hizo na kuwa watu wema.
Pepo ni nguvu ya kiroho yenye uvuvio wa shetani imuingiayo mwanadamu ili kuvuruga kuharibu saikolojia yake.
 
Duhh mbona Leo mnasemana wenyewe kwa wenyewe?
 
Nyie ndio Mungu,mbona mnamsemea!?Tukiimba katika Roho na kweli hapo hamna kelele.Kelele ni kupuyanga pasi na Roho wa Mungu hivyo hata nyie mnaojinasibu kuimba kwa codes gani sijui...kama moyo sio safi ni makekele tu.
Ustaarabu ni kutokosoa imani usiyoishiriki.Hukubaliani lkn kuwa na staha fanya yako.
 
binafsi sio mhusika wa kuimba kwa codes. ninachosema, uimbaji wa vurugu sawa tu na manyimbo hayo ya dunia, haupo kwenye abudu yeyote kwenye historia ya Biblia. hakuna mtu aliwahi kuabudu Mungu kwa namna hiyo. hata Daudi alivyocheza kwa kuvua nguo na kuruka mbele za watu, hakuwa anafanya hivyo kuabudu, alikuwa ana express feelings za furaha yake tu. tutajie mtu mwingine aliyewahi kumwendea Mungu akiabudu kwa namna hiyo mnayoifanya ninyi. hayupo. mnapenda sana kuifuatisha namna ya dunia hii, mnacopy vitu vya dunia ili kuvifanya kwa Mungu as if Mungu hawezi kuanzisha cha kwake. Huwezi kumwendea Mungu bila unyenyekevu na utulivu. you should always be still and know that he is God. hapo ndipo atajidhihirisha kwako. tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, mnapoteza muda na hiyo sio abudu ambayo Mungu anaihitaji. Mungu sio binamu yenu.
 
shida ninayoiona kwako sio utaratibu wa machinga au mahubiri. shida yako wewe ni wokovu, hutaki kuhubiriwa, una kashetani ndani yako kanakokerwa na Mahubiri. kimbia haraka upone, nafasi bado ipo kabla mlango haujafungwa.
 
Hongera kw Wasabato na Wakatoliki....
Ukisikiliza nyimbo unaguswa kabisa...Kwingine vijana wanaenda kufuata kipindi cha kuimba ili waruke majoka...
Tunakoelekea watu wataanza kutumia style ya regge kuimba kanisani, tukimaliza tunaingia na melody ya taarabu....then tunamalizia na singeli
 
dah inasikitisha sana,wanawake wanakatika laivu huku matako ya kutikisika ni mwendo wa kudinda dinda tu makanisana, kuna ya le mahubiri yao utasikia .nyuma kuna shimo na mbele kuna shimo ukitumbukia nyuma ni balaa huwezi kutoka,nyimbo zao sasa nimekiona kiti kimesimama haja ya moyo wangu umusifu bwana .kwakweli huwa hii inanitoa kwenye uwepo kabisa
 
Sina sababu ya kuelezea ila mimi moyoni nilikataaa yale ma drum na mangoma ngoma kuwepo kanisani.
Shida sio hivyo vyombo, hapo tatizo ni wapigaji. Kila aliyeshika chombo anataka kisikike zaidi ya mwezie ndio maana badala ya kupata mziki uliopangiliwa unasikia makelele tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…