Pre GE2025 Mch Msigwa: Mbowe na CHADEMA hawana tena ujumbe kwa Watanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Bila shaka umenielewa vizuri Mkuu, kule alikuwa anakosa hoja Kwa kuwa alikuwa anajicontradict mwenyewe,Kwa Sasa amesikiliza sauti ya ndani kutoko moyoni mwake na kuutambua ukweli,asikilizwe Sasa.
Kwahiyo hoja ni kumshambulia Mbowe?
 
Mna wabunge wangapi ukilinganisha na 2015-2020?
2020 hakukuwa na uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Sasa nakupe idadi kwa uchaguzi gani kwa mfano?
 
Kwa hiyo Msigwa ni msemaji wa Watanzania kwa sasa?
Msigwa asipotaja Chadema au ccm lazima wamtimue
 
Jamaa uliichukia sana chadema kwa sababu ya Padre Silaa. Sasa hivi nadhani baada ya Silaa kurudi CCM, umepunguza chuki….siasa zako ni za kidini mnooooooo.
Kumbe Slaa karudi CCM?

Nashukuru Kwa taarifa Mkuu
 
Msigwa tapeli tu Hilo la kisiasa linatafuta udc kwa mgongo wa mbowe na cdm. Na chama chama changu CCM ntawashangaa kumpa cheo huyo tapeli.
Kama mtaendelea na mentality kama hiyo basi kuwakomboa makamanda itakuwa ni vigumu sana.
 
Nafurahi kuona SISIEMU wamempa Msingi msigwa na sasa amefungua biashara ya mayai.

Ningemshauri Msigwa ajikite kutafuta ABCs za biashara yek mpya ya mayai ,amtafute Bon Yai ,aache mambo ya kumsema Mbowe kila muda.
 
Wangekuwa hawana ujumbbe mngehangaika na kuwateka na kuwaua?
 
2020 hakukuwa na uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Sasa nakupe idadi kwa uchaguzi gani kwa mfano?
Sasa kama mlikuwa na wabunge 89 na sasa mko na Mbunye 01 ina maana mnashuka(kufa kisiasa). Kwamba mnafikiri kuna siku CCM itawapa tu Chenye mnataka kwenye sahani? Mliporwq uchaguzi, mlifanya nini?
 
Sasa kama mlikuwa na wabunge 89 na sasa mko na Mbunye 01 ina maana mnashuka(kufa kisiasa). Kwamba mnafikiri kuna siku CCM itawapa tu Chenye mnataka kwenye sahani? Mliporwq uchaguzi, mlifanya nini?
Wabunge 89 hatukupata kwa hisani. Hatuhitaji hisani ya ccm, lakini hatuko tayari kuendelea kushiriki chaguzi za kipuuzi tena. Tumeporwa uchaguzi tunataka mazingira sahihi ya ushindani. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi yatarejesha heshima ya box la kura, sio kwenda kupotezeana muda tena kwenye mstari wa kura.
 
CHADEMA Wana sera Gani mbadala au Bora Zaid kuliko CCM kias Cha kuwaamini uwape Dola waongoze?
 
Umehama chama una miezi kibao badala ya kuuza sera za ulikohamia, unabaki kuleta nogwa. Toka lini nogwa ikawa hoja?
Ili kuwazindua wengine ambao Bado mpo kwenye Mbowe's captivity ni lazima awaeleze why alihama huko,na Yale ambayo aliwaaminisha kipindi yuko kule awaeleze kuwa hayakuwa ya kweli.
 
CHADEMA ndiyo imeleta umaskini wa watanzania?
 
Bila shaka,hata yeye hoja yake kaweka wazi kuwa CHADEMA kama. Chama kinaangamia Kwa kukosa maarifa mapya,na kwamba Mwenyekiti amehodhi chama na kukiweka mfukoni.

..mambo aliyokuwa akisema ni mabaya ktk Ccm bado yapo, sasa unawezaje kwenda hukohuko alikokuwa akisema ni kubaya?

..mimi nadhani Msigwa angeeleweka kama angehamia ktk chama kingine cha upinzani, halafu akaendelea kuwapiga spana Ccm, na Chadema.

..Ni vigumu kufuta hoja, na mashambulizi ya Msigwa, dhidi ya Ccm, toka ktk kumbukumbu za watu wengi.

..Naamini hata Ccm na kwenyewe watakuwa wanamuona Msigwa, ni kituko, na hayuko sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…