Mchaichai (Lemon Grass) na faida zake kwa matumizi ya mwanadamu

Mchaichai (Lemon Grass) na faida zake kwa matumizi ya mwanadamu

1.KUSAFISHA FIGO NA MKOJO

Mchaichai una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu katika mwili, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa na kemikali za viwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa na baadaye kusasababisha magonjwa mbalimbali.Figo inapokuwa safi na imara,hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo zinafanyika

kirahisi


2.HUSAIDIA UMENGENYWAJI WA CHAKULA MWILINI

Mchaichai husifika kusaidia urahisishaji wa mmengenyo wa chakula mwilini na kutibu maumivu ya tumbo kama vile hali ya tumbo kujaa gesi.


3.KUZUIA HALI YA KUHARISHA MARA KWA MARA

Mchaichai pia ni dawa nzuri kwa wale wanaosumbuliwa na hali ya kuarisha mara kwa mara,kwani inauwezo wa kupambana na mdudu aina ya protozoa anayesababisha ugonjwa huu.


4.HUSAIDIA KUSAFISHA DAMU

Faida nyingine ya mchaichai ni kusafisha damu mwilini hasa kwa watu ambao wamekuwa na tabia ya kupata magonjwa ya ngozi kama mapele na kutoka majipu.


5.HUUPA MWILI KINGA DHIDI YA UGONJWA WA SARATANI.

Mchaichai umegundulika pia unauwezo wa kuua seli zinazoweza kusababisha ugonjwa wa saratani.Kwani kwenye gila gram 100 ya mchaichai kuna virutumbisho ambayo vinaweza kuondoa na kuukinga mwili dhidi ya sumu ambayo inasababisha ugonjwa wa saratani.


6.KUONDOA MLUNDIKANO WA MAFUTA KATIKA MISHIPA YA DAMU

Mchaichai husaidia kuondoa mafuta katika mishipa ya damu hivyo kuruhusu damu kupita vizuri katika sehemu mbalimbali za mwili na kuifanya mishipa hiyo kuwa na afya njema.Pia kusaidia mapigo ya moyo kuwa katika hali nzuri wakati wote.


JINSI YA KUTUMIA MCHAICHAI

Kupata faida hizi unashauriwa majani ya mchaichai yalowekwe katika maji ya moto kiasi cha vikombe vitatu vya chai, weka majani ya mchaichai kisha kunywa maji hayo kiasi cha kikombe kimoja cha chai kabla ya kula chochote asubuhi, mchana, nusu saa kabla ya mlo, na jioni kabla ya chakula cha jioni.Pia unaweza kutia sukari kwa kiasi kidogo mno. Unaweza fanya jambo hili kuwa endelevu kwa kutumia chai ambayo imepikwa kwa majani ya mchaichai mara kwa mara.

[https://4]


Kumbuka faida zilizo tajwa hapo juu ni chache tu ambazo nimekuletea siku ya leo na ni matumaini yangu utanza kutumia mchaichai kuwa sehemu ya lishe yako ili kupata virutubisho mbalimbali na kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchaichai ni dawa ya kushusha presha pia. Usage kwa mkono utie ndani ya maji ya kawaida uwache kwa muda ikisha unywe
 
Mchaichai una faida nyingi zaidi ya kufukuza wadudu za kutia harufu nzuri ( kwenye vyakula na vipodozi).

Mchaichai ukichumwa na kuchemshwa waweza kunywewa kama tiba ya kuua cells za cancer.

Madaktari hushauri wagonjwa wanaopata tiba ya mionzi kunywa chai hii kwanza kabla ya tiba!

SOMA HAPA CHINI:

Lemongrass is a perennial, aromatic tall grass with a light lemon scent used for culinary and medicinal purposes. For centuries, herbalists have used the herb as an effective digestive tonic and nervous system relaxant.

Lemon grass oil is used to help clear blemishes and maintain balanced skin tone. Lemon grass is also used as an insect and mosquito repellent.

Now, according to Israeli scientists, they can add cancer prevention to the list of attributes associated with lemon grass
Hapo kwenye kansa inabidi watu wa mwanza washauriwe kutumia,maana idadi ya watu wanaopata kansa kutoka kanda ya ziwa inazidi kuongezeka.
 
Hapo kwenye kansa inabidi watu wa mwanza washauriwe kutumia,maana idadi ya watu wanaopata kansa kutoka kanda ya ziwa inazidi kuongezeka.
Ninahisi matumizi holela ya kemikali kama zebaki za kusafishia madini migodini au wachimbaji wadogo wa madini huchafua mazingira mashambani, mitoni na ziwani inachangia hii.

Ningeshauri serikali iwafanyie tafiti samaki toka ziwa Victoria unaweza kukuta jambo la kushitua.

Angalizo: Sijasema samaki wa ziwa Victoria wana tatizo.
 
je ni kweli inasaidia kwenye tatizo la nguvu za kiume?
 
Back
Top Bottom