Christina Kamili(Jukwaa la Katiba): Katiba ya Warioba ilibeba maslahi mapana ya wananchi hasa mgawanyo wa mihimili 3 ya Serikali
[HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG]
Mchakato wa marekebisho ya Katiba ulipitia awamu 3. Awamu ya kwanza ilikuwa ya kuundwa Tume ya marekebisho chini ya Jaji Warioba
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
Miongoni mwa mambo yaliyopendekezwa ktk rasimu hii ni kubadilisha muundo wa sasa wa Serikali 2 na kuanzisha muundo wa Serikali 3
[HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG]
Bunge Maalumu la [HASHTAG]#Katiba[/HASHTAG] lilipitisha rasimu hii Oktoba 2014, pasipo kujali kujiondoa kwa wajumbe waliounda umoja uliojulikana kama UKAWA
93% ya Watanzania wameshawahi kusikia kuhusu Katiba, lakini kati yao 58% hawafahamu Katiba ni nini
[HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG] [HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
22% - Ni mkusanyiko wa kanuni zitumikazo kuongoza nchi
12% - Ni azimio la kisheria litumikalo kuongoza nchi
1% - Azimio la haki za wananchi
Uelewa wa Katiba ni mkubwa miongoni mwa wenye elimu ya Sekondari na ya juu(49%) kuliko ambao hawajahitimu elimu ya msingi(22%)
Uelewa wa Katiba ni mkubwa miongoni mwa wenye umri > miaka 50(45%) kuliko wenye < miaka 30(29%) - Matajiri(40%); masikini (28%)
Uelewa wa Katiba kati ya wanaume na wanawake: 47% ya wanaume waliweza kueleza maana ya Katiba, ukilinganisha na 22% ya wanawake
44% wanasema [HASHTAG]#Katiba[/HASHTAG] iliyopo inatekelezwa ipasavyo, 46% wanasema inatekelezwa “kwa kiwango fulani”. 4% tu wanasema “haitekelezwi ipasavyo”
Waliosema [HASHTAG]#Katiba[/HASHTAG] inatekelezwa ipasavyo walisema ni kwa sababu sheria zinafuatwa (22%) au kutokana na kwamba uongozi ni mzuri (12%)
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
Waliosema “inatekelezwa kwa kiwango fulani” walieleza kuwa kuna baadhi ya vipengele vya Katiba(15%) au Sheria(12%) ambavyo havifuatwi
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
71% ya wananchi wanafahamu kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa [HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG] ilianzisha mchakato wa mabadiliko ya [HASHTAG]#Katiba[/HASHTAG] yake
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
Uelewa wa mchakato wa [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG] ni mkubwa miongoni mwa wanaume (81%) ukilinganisha na wanawake (61%) [HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
Uelewa wa mchakato wa [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG] ni mkubwa miongoni mwa wenye miaka zaidi ya 50 (81%) kuliko wenye umri chini ya miaka 30 (63%)
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
Wananchi 2 kati ya 3(67%) wanasema maoni ya wananchi hayajatokea kwenye rasimu ya [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG] iliyoandaliwa na Bunge Maalum la Katiba [HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
23% ya wananchi wanasema mchakato wa [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG] kwa kiasi kikubwa ulikuwa ni
kuwapa taarifa kuliko kuruhusu wananchi kutoa maoni yao
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
44% ya wananchi waliona mchakato huo uliwapa fursa wananchi kutoa maoni yao, lakini hayakutumika kwenye rasimu ya [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG]
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
59% ya wananchi wanasema Bunge Maalumu la [HASHTAG]#Katiba[/HASHTAG] liliwawakilisha vema watanzania ktk mchakato huo
- 38% hawakubaliani na kauli hiyo
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
Mwananchi mmoja kati ya wanne(23%) wanaunga mkono UKAWA kususia Bunge Maalumu la Katiba na kugomea mchakato wa kupitia [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG]
[HASHTAG]#szw[/HASHTAG]
56% ya wananchi wanasema kutoka nje kwa UKAWA hakubatilishi mchakato wa [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG] ; 41% wanasema kitendo hicho kinabatilisha mchakato
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
48% ya wananchi wanasema njia nzuri ya kufufua mchakato wa mabadiliko ya Katiba ni kuanza mchakato huo upya na tume mpya
[HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG] [HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
Wananchi hawakubaliani na mabadiliko mengi yaliyofanywa na Bunge la katiba chini ya M/Kiti kamati ya uandishi [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG], Ndugu Chenge
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
79% hawakubaliani na kuondolewa kifungu kinachotaka mawaziri kupitishwa/kukataliwa kwa kura bungeni baada ya kuteuliwa na Rais
[HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG]
Ado Shaibu kutoka Chama cha ACT-Wazalendo: Kwa Ripoti hii ya Sauti za Wananchi iliyotolewa na TWAWEZA ni dhahiri kuwa wananchi wanahitaji [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG]
Ado Shaibu(ACT): Rais Magufuli hakusema mchakato wa [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG] haufai bali alionesha wazi kuwa si kipaumbele cha Serikali Awamu ya 5
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
Ado Shaibu: Utafiti huu umebainisha kuwa kuna pengo kubwa kati ya Wanawake na Wanaume katika uelewa wa mambo nchini
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG] [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG]
Ado Shaibu: Mchakato mzima wa [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG] unaonesha [HASHTAG]#SautiZaWananchi[/HASHTAG] zimezimwa
- Wananchi wametaja vipengele walivyopendekeza na vikatolewa
Ado Shaibu: Wapinzani tunafanya makosa ktk kujifungamanisha na Wadau wakuu ambao ni wananchi
-Wananchi wengi hawaijui UKAWA
[HASHTAG]#SzW[/HASHTAG] [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG]
Polepole(CCM): Watanzania kwa takwimu hizi za Twaweza wanataka kuona Ukatiba(constitutionalism) kuliko Katiba(constitution) nchini
Polepole: Watu wa kawaida wanataka viongozi waadilifu, wasiokula rushwa, wanaojua cheo ni dhamana; huo ndio Ukatiba [HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG]
Polepole: Ukatiba ni kuwekeana mifumo hata kama haikuandikwa mahali. Kila mtu akielewa hii mifumo hakutokuwa na tatizo
[HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG] [HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]
Polepole: Tunaweza kuandaa Katiba na kuiweka kwenye kitabu lakini bila Ukatiba hakuna atakayeifuata
[HASHTAG]#KatibaMpya[/HASHTAG] [HASHTAG]#SzW[/HASHTAG]