Mchakato Katiba Mpya: 44% wanasema maoni yao hayakuwekwa kwenye Katiba iliyopendekezwa

Hilo bunge lilikuwa mkusanyiko wa taasisi na mafisadi wa CCM, wakitetea wizi wao kina Chenge.
Polepole leta mezani rasimu bora ya Mzee Warioba.
Tengeneza katiba bora ya Watanzania.
Hila mbinu chafuu
hazitatusaidia!!
Sawa kabis unavyosema lakini hiyo ndio mshahara wa watu wanaosusa susa kama watoto wakike au wadogo. Waliosusiwa wameamua kufanya vile kutokana na mawazo yao na kile wanachokitaka. Hata ingekuwa wewe.
Wale wana haki ya kutoa maoni yao hata kama wengine hawayakubari, sababu mchakato ule ulikuwa unawapa uhuru huo na kumbuka haikusemwa mawazo ya wananchi yatakuwa ya mwisho.
So, hao unao washutumu wewe naona wapo sahihi kwa upeo wao ulipoishia kuliko wale walio susa na kutoka nje.
 
Kama ni kuendelea pale bunge la katiba lilipoishia, yaani kupigia kura katiba iliyopendekezwa na bunge la katiba, bora kuachana na kitu kicho kabisa,
Kinachotakiwa ni kurudi nyuma kabisa:
Kwanza tufute mabadiliko ya sheria ya mchakato wa mabadiliko ya katiba - mabadiliko ambayo yaliiondoa tume ya Warioba kusimamia kura ya maoni na kuipa tume ya uchaguzi madaraka hayo (mabadiliko hayo yalilenga kuficha matokeo halisi ya kura za wananchi kwa kuwa tume ya uchaguzi si tume huru)
Pili, katika sheria ya mwanzo ilikuwa kama wananchi wataikataa katiba waliyopelekewa kuipigia kura, basi tume ya Warioba ilitakiwa irudi tena kwa wananchi kuwauliza ni kwanini wameikataa katiba hiyo na marekebisho gani wanayataka, Hivyo marekebisho yaliyofanywa kuwa wananchi wakiikataa katiba watakayokuwa wapelekewa waipigie kura basi Katiba ya zamani iendelee, yafutwe (Mabadikliko haya yalilenga kuwalazimisha wananchi kuikubali katiba mpya hata kama ina mapungufu mengi, vinginevyo wataendelea na katiba ya zamani, Hiki ndicho kiini cha kuchomeka vipengele visivyofaa katika katiba pendekezwa!)
Tatu, bunge la katiba lisihusishe wabunge wa bunge la kawaida maana hao wamechaguliwa kwa utashi wa vyama vyao na hivyo wanatumiwa kulinda maslahi ya vyama badala ya maslahi mapana ya wananchi.
Nne, wajumbe wa bunge la katiba wawekewe masharti magumu ya kugombea uongozi wa kikatiba baada ya kupatikana katiba mpya, hii itasaidia wabunge hao kutopitisha katiba kwa maslahi binafsi, Nakumbuka kuna nchi wajumbe wa bunge la katiba na familia zao na ndugu wa karibu walizuiwa kugombea nafasi za kikatiba kwa muda fulani
 
kasome tena mchakato wakatiba ulivyo!

hiyo iliyopendekezwa ikikataliwa, bunge linaitishw atena then wanakwenda kukubaliana, then kura tena, ikkataliwa basi tunarudi ya zamani.
Na hapo ndipo upuuzi ulipo,wananchi wakiikataa siyo kurudishwa tena bungeni, Inabidi wananchi waulizwe sababu za kuikataa na wapendekeze marekebisho wanayohitaji; baada ya hapo irudishwe kwa wananchi kwa kura.
Kuna mantiki gani eti wakiikataa katiba mpya basi warudi ya zamani - kwani maoni yao walitoa ya nini? Hapa ndipo kuwachezea wananchi yaani wanatuletea katiba pendekezwa mbovu iliyochakachua maoni yetu ili tukiikataa wabaki na ya zamani - shame kwa wote waliobadilisha sheria
 


Mpoka ikataliwe mara mbili na wananchi.
 
Mchakato wa katiba uko na hatua tatu:
1. Kukusanya maoni na kuandaa rasimu;
2. Rasimu kujadiliwa na Bunge la Katiba na;
3. Kaiba Pendekezwa kupigiwa kura na wananchi wapiga kura.
Sijui ni kwa nini baadhi ya watu wanataka tuanze moja! Je, ni kwa sababu UKAWA walisusia mjadala kwenye Bunge La Katiba? Je, ni kwa sababu kipengele cha ulaji na kuwagawa Watanzania kwa kuwa na serikali tatu kiliondolewa? Je, ni kwa sababu wasaka tonge walikwamishwa kwa kipengele cha ghiriba na fitina cha kuwaondoa wabunge, eti kwa sababu ya kutokuwatumikia wananchi vyema ndani ya muhula wa utumishi wao?
Kama alivyosema Ndugu Polepole, cha msingi ni namna ya kuwa na viongozi wenye sifa zilizotukuka za kutumikia wananchi hata bila ya Katiba. Hebu tafakari kwa mfano, tunazo sheria nzuri dhidi ya uhalifu wa ulaji rushwa au uhujumu uchumi, je, ni kwa namna gani zimezuia watu kutoa na kupokea rushwa au kuhujumu uchumi wa nchi?
Kimsingi, nadhani ni vyema mchakato ukaendelea ulikoishia. Kumbukeni kwamba, kuna kipindi cha miaka minne ya matazamio baada ya kupitishwa ambacho kinaweza kutumika kutathmini mapungufu na kuifanyia maboresho!
 
Mimi nimeshangaa sana kuhusu kujua na kueleza maana ya katiba kati ya wanaume na wanawake, kumbe wanawake uelewa wao uko chini hivyo. Pia, wale wenye elimu ya darasa la saba, uelewa ni mdogo MNO wa katiba. Nilichofurahi ni kuwa WETU wengi kama 67% wanasema mambo mengi yaliachwa kwenye
 
Maoni ya TWAWEZA huwa yanachkuliwa toka kwa watu gani maana sijawahi sikia mtu mtaani kahojiwa na na hao watu ila kila siku wanatoa tafiti zao
 
Tunahitaji Katiba Mpya, hapa tulipokwama hakuna kiongozi au mtu mmoja anaweza kutukwamua.

Rais Magufuli ni mtawala mwenye nguvu katika mfumo dhaifu....na hilo litaweza kupata suluhu kwenye Katiba.
 
Katiba mpya inahitajika japo siyo leo jiulize nani wenye akili ya kimungu wa kutengenezea katiba itakayo lipeleka taifa mbele kwa karne nyingi? Leo ukitaka maoni ya wanaoitwa wananchi utakuta siyo wananchi bali akili zao ziko kivyama.
 
Usomeshe wanao wa kike mkuu. Gepu kati ya gender mbili ni kubwa sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…