Binafsi naona mchakato wa katiba ulianza kupotezwa na jaji warioba mwenyewe kwa kuto heshimu maoni ya wengine. Mchakato ulikuwa na vipengele muhimu kadhaa, baadhi ni ukusanyaji wa maoni ya wananchi, kuyachambua, na lililokuwa la mwisho, ambalo ni muhimu kabla ya kupiga kura, ni bunge la katiba. Hapa ndipo babu alipotuyumbisha. Kazi kubwa ya bunge la katiba ilikuwa kuijadili rasimu ya katiba na SI KUIPITISHA. Sasa mzee Warioba na ukawa walitaka ipitishwe, jambo ambalo lilikuwa halileti maana ya kuwa na bunge la katiba. Ninavyojua mimi, majadiliano yanaweza kupunguza, kuongeza au kuondoa baadhi ya vitu. Hivi mnawezaje watu zaidi ya 300 kujadili kitu kimoja mkawa na mawazo sawa?
Kweli tunahitaji katiba mpya, ila kama mchakato utakuwa ni uleule wa kuwa na bunge, basi ni lazima tuheshimu mawazo ya bunge sababu kupeleka maoni yetu kule ina maanisha mawazo ya wananchi sio ya mwisho ila ya bunge la katiba.
Kwahiyo tusijitoe ufahamu wakujifanya kutokujua nafasi ya bunge la katiba.
NARUDIA TENA, KAMA TUNATAKA KATIBA YENYE MAWAZO YA WANANCHI PEKE YAO, BASI KUSIWEPO NA BUNGE LA KATIBA.