Katika kipindi cha TBC1 cha Mchakato Majimboni, mgombea Ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ametia fora na kuwapiku wagombea wenzake huku akishangiliwa na watu waliofurika kwenye ukumbi ambapo kipindi hicho kilirekodiwa na kurushwa hewani, kuanzia saa 3 usiku, Jumamosi, Oktoba 2, 2010.
Kabwe alijieleza vema kuliko kila mgombea na kudhihirisha kwamba CHADEMA bado inakubalika, na ina mipango dhahiri ya kuliendeleza jimbo hilo, mojawapo ya mipango hiyo ukiwa ni ule wa kuileta kampuni inayosimamia masuala ya reli nchini Ujerumani, kuja kusimamia uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania, kwa msaada, kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani, kwa muda wa miaka miwili.
Zitto alisema: Sio kwamba tutafanya nini, ni kwamba, tunafanya nini. Tupendi nafasi tuweze kuendelea kutekeleza mipango yetu ambayo tayari imeonekana.
CCM na vyama vingine vitapaswa kufanya KAZI YA ZIADA kumwondoa Zitto kwenye jimbo hilo! Ama kweli, ni KAZI NZITO kumwondoa ZITTO kwenye jimbo hilo!
-> Mwana wa Haki