Elections 2010 Mchakato majimboni TBC1 Jimbo la Kigoma Kaskazini

Elections 2010 Mchakato majimboni TBC1 Jimbo la Kigoma Kaskazini

huyu mgombe wa CUF anadharau sana, anasema masikini, hawezi kumsaidia masikini mwezake, anasema wampe yeye ili awasaidie
jeuri ya tajiri wa kijijini hiyo..umeiona?.......kama issue ni utajiri, basi asigombee, akawasaidie wananchi kimya kimya.

Katika kipindi cha TBC1 cha Mchakato Majimboni, mgombea Ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ametia fora na kuwapiku wagombea wenzake huku akishangiliwa na watu waliofurika kwenye ukumbi ambapo kipindi hicho kilirekodiwa na kurushwa hewani, kuanzia saa 3 usiku, Jumamosi, Oktoba 2, 2010.

Kabwe alijieleza vema kuliko kila mgombea na kudhihirisha kwamba CHADEMA bado inakubalika, na ina mipango dhahiri ya kuliendeleza jimbo hilo, mojawapo ya mipango hiyo ukiwa ni ule wa kuileta kampuni inayosimamia masuala ya reli nchini Ujerumani, kuja kusimamia uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania, kwa msaada, kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani, kwa muda wa miaka miwili.

Zitto alisema: Sio kwamba tutafanya nini, ni kwamba, tunafanya nini. Tupendi nafasi tuweze kuendelea kutekeleza mipango yetu ambayo tayari imeonekana.

CCM na vyama vingine vitapaswa kufanya KAZI YA ZIADA kumwondoa Zitto kwenye jimbo hilo! Ama kweli, ni KAZI NZITO kumwondoa ZITTO kwenye jimbo hilo!

-> Mwana wa Haki

Hiki ndicho ninachokiongelea kila mara kwa wagombea hususan wa upinzani. Zitto,kutaja tu reli ya kati umegusa eneo lote la Tanzania magharibi na kati,na umegusa asilimia 90 ya watu. Wagombea ni lazima wajue shida za wananchi na waeleze ufumbuzi.Shida ya kigoma si airport au kuwa Dubai ni usafiri unaoathiri asilimia 98 ya wakazi wa huko kijamii na kihuduma. Hapa umekula TANO za juu Zitto.
Kafulila anaongelea Milenia [2015 milleniumn devel.goal], mungu wangu! huyu mtu anayekusikiliza hajui asafirishe vipi dagaa, hajui afike vipi muhimbili, hajui mtoto aende vipi shule kule minaki, hajui mafuta ya taa yatafika lini ni mpaka aende burundi, halafu unamtajia MDG si anaona unaongea mazingaombwe!
Kule sumbawanga,mazao yanaoza shambani halafu watu wanasema kilimo kwanza,kwanini wapinzani wasiongelee kusafirisha na kutoa bei nzuri za mazao ambalo ni tatizo la wakulima wa sumbawanga.
Wapinzani chambueni Ilani zenu za uchaguzi na mu-simplify kwa mwananchi wa kawaida kuelewa.

zitto jibu maswali ya wana jf tafadhali,kukaa kwako kimya kunafanya watu wasikufikirie vizuri..
Kwa nini hauonekan kwenye kampen za dr slaa ilhal wew ni mmoja wa wa vijana wa chadema wenye ushawishi katika jamii?

zito hasubutu kumfanyia kampeni slaa kwani kashfa ya ngono ya huyu padri imemsikitisha sana zito!!!

Kama Zitto hukutumia nafasi ile adhimu kumnadi, au kumfagilia dr Slaa mbele ya wananchi wanaokutazama basi ujue kwamba umepoteza nzafasi adhimu sana ya kukisaidia chama chako kuongeza nguvu katika Uchaguzi.

Hata kama kuna tofauti zozote, au mkwaruzano wowote katika kambi yenu(sijui ukweli wa hili) lakini fahamu kwamba,sisi wananchi wa Tanzania wapenda mabadiriko, tunatamani kuona Upinzani unachukua hatamu za nchi hii!. Tunafanya hivyo siyo kwamba hatufahamu mapungufu ya Dr, bali tunafanya hivyo huku tukifahamu kwamba mapungufu ya CCM ni makubwa zaidi.

Pengine unajiamini kwamba you can make it "ON YOUR OWN". lakini huku ni kujidanganya, mpiga kura wa leo huenda akawa mpiga kura wa chaguzi nyingine zijazo!. Wanamageuzi tupo tunaangalia kwa makini, ni nani yupo on our side wakati huu Muhimu. kumbuka John McCain pamoja na kufanyiwa kitu mbaya na Mpinzani wake George Bush katika primaries za Republican mwaka 2000 , aliamua kusimama na kumu endorse Bush katika kinyang'anyiro cha mwaka 2004 walipokuwa wanapambana na John Kerry. pamoja na kambi ya Kerry kumuahidi umakamu wa Raisi kama angekubali kusimama nao. unaona sasa wana Siasa waliobobea, McCain huyuhuyu akaja kupata Support ya nguvu kutoka kwa Gerge Bush mwaka 2008.

Zitto you cannot make it on your own, believe me!. Siasa siku zote zina evolve, you need alliances. wakati mwingine unahitaji kujishusha, hata kama unadhani umeonewa katika ishu fulani, "EGOISM" need be controlled. you cannot go on your own and think you are making a service to your party!.

Kwa sasa Dr Slaa yupo on the Prime Time, na Watanzania wana mreward kwa heshima ya kusimama on their side on many issues continously. hata wewe kuna wakati Watanzania walikutreat atleast the same wanavyomtreat Slaa baada ya ile issue ya Buzwagi. Sasa na wewe tunahitaji Support yako this time.

Ila kama unadhani, you are "YOUR OWN MAN" then wananchi wanajua vizuri kweli kuchambua pumba na mchele, Hebu angalia, Mrema yuko wapi?

Ahaa heee! Jamaa wa APPT MAENDELEO Kweli ana vituko sana, mbona kama alikuwa amekariri tu na bado anababaika? Sera za chama anajimix, kigugumizi kingi dah! Ndio ugombea huo wa wasiwasi mmh! Watu ilibidi wamshamgilie tu kwani anachekesha jinsi alivyokuwa akijiuma uma. ... About Zito no comment... Mayowe, makofi, nderemo na vifijo vinasadifu kupendwa kwake... Kila la kheri...

Hajamtaja hata chembe Slaa? You don't tell me...!

Sio tuu hajamtaja hata kidogo Dr. Slaa, bali pia hajazungumzio lolote kuhusu Chadema kama chama wala madiwani wake. zitto amedorminate debate kama Zitto.
Siamini hkumtajaDr. Slaa kwa bahati mbaya, Zitto ni researcher makini hivyo siasa za Kigoma anazijua fika. Kumkampenia Dr. kigoma ni sawa na Dr. Kwenda kukampeni Pemba, au Lipumba kwenda kupiga kambi Karatu!. Kwa vile ameshalijua chaguo la WanaKigoma kwenye kura za urais, nadhani aliamua kumuepuka Slaa asije akapunguza kura zake za ubunge. Kigoma ni moja ya maeneo yenye siasa kali za fundamentalism.

Ukiwa na muda fuatilia kipindi hiki leo

Nimekiangalia kipindi chako. Hii ni tathmini yangu ya awali.
1.Umefanya vizuri, umedorminate ni hakika utashinda bila mashaka ukishashinda, mshike mkono huyo jamaa wa CUF, mleteni Chadema msafishie njia kwa 2015.
2.Host Shabani Kissu, alikubeba kiaina or it was just a coincidence kwamba wewe ulipewa nafasi ya kuwa mzungumzaji wa mwisho kila wakati tangu mwanzo hadi mwisho, hivyo kuwafunika wapinzani wako wote.
3.Umeonysha sana ile elementi ya Umimi zaidi kuliko team work spirit, kuna maeneo mengi tuu ungeweza kujibu sisi Chadema au hata kuinadi tuu sera yenu na wagombea wenu. Nasubiri ratiba ya Dr. Kigoma niondoe mashaka ya kinachoendelea chini kwa chini huko uvunguni kwenu.
4. Nakupongeza, hongera sana.

Alimtaja Said Arfi tu na jinsi chadema ilivyokwishaanza kushughulikia swala la TRL. Naona kama lengo lake pale ni kujinad tena ilitakiwa uwe mhafidhina. Naona tajiri wa CUF alimchanganya ndio maana ikabidi aongeze nguvu zake. Ngoja tusubirie siku zinavyokwenda tutathibitishawacwac wa wana JF juu ya umimi wa Zitto

Alimtaja Said Arfi tu na jinsi chadema ilivyokwishaanza kushughulikia swala la TRL. Na
ona kama lengo lake pale ni kujinad tena ilitakiwa uwe mhafidhina. Naona tajiri wa CUF alimchanganya ndio maana ikabidi aongeze nguvu zake. Ngoja tusubirie siku zinavyokwenda tutathibitishawacwac wa wana JF juu ya umimi wa Zitto

Umimi wa Zittohauhitaji JF kuuthibitisha, kipimo kidogo ni kule tuu kutostand crticisim. Alikuwa mchangiaji mzuri tuu humu ndani, alipokwaana na macritic humu alitukimbia na kuhamia kule kwa wana bidii, huko nako yalipomtokea jamaa kajifunika kwenye ile shell yake 'mimi'.
Kwa vile yeye ndie thread starter wa hii thread sio ameiazisha ili kubadilishana mawazi nasi, bali kaileta ili kutuambia niangaieni, tumeangalia tukitegemea atakuwa nasi kwenye michango au kujibu hoja, kumbe no! Ilikua nioneneni. Sasa si mmeshaniona, inaosha!.

Zitto nakuomba come back hata kusema tuu "thanks for your observations and comments" tutatosheka, huku kukaa kimya ni dharau, kiburi, jeuri na kujisikia!
Please!.

Zitto ni mbinafsi sana nakumbuka hata pale UDSM wakati tunasoma aliendesha mgomo na baadae akatusaliti wana DARUSO. He is a very strong politician na inaonyesha anakubalika sana ila team work ni muhimu sana hasa kwa yeye anayetaka kugombea uraisi mwaka 2015 kwa tikiti ya CHADEMA. Hivi wana bifu gani na Dr.Slaa jamani?

Achen hizo zitto ni mpiganaji na ni zaid ya mara moja nimemsikia hakimtaja slaa kwenye kampeni zake,na hata jana alisema serikari watakayoiunda chadema itatasimamia maendeleo endelevu ya elimu na kilimo,akaongezea tunaomba mutuunge mkono ili tuunde serikal makini,alafu awezi kuzunguka na slaa kwa kuwa hayuko kwenye ratiba naye ana ratiba yake,ndio maana chama wamempangia zitto baadhi ya majimbo na mikoa ya kupitia na kaz hiyo kaianza na huwa anamnad slaa.hiv mbona watu wengi muhimu chadema hawazunguki na slaa lakin hamuhoji,profesa Baregu ni meneja kampen lakin hayuko kwenye msafara wa slaa,Mbowe ni mwenyekiti lakin hayuko kwenye msafara,kwanini iwe kwa zitto?km ni mbunge makin mbona watu km akina Herrison Mwakyembe ni wabunge makini lakin hawako kwenye msafara wa kikwete,acheni ushabiki wa uongo,kumbuka helikopta yenyewe moja watapanda wangapi?na kingine inabid chadema ndio waseme tumempangia zitto ratiba ya kuzunguka na rais kakataa hapo ndio mutaweza kusema munayosema.lakin zitto hajapangiwa na ndio maana anaenda kwenye mikoa anayopangiwa na jimbon kwake.ccm hachen propaganda zenu munataka zitto awe bize na slaa ili mumpige bao jimbon kwake.Turud kwenye mdahalo wa jana hiv muligundua kuwa yule jamaa wa cuf alikimbia katikati ya mdahalo,ni pale zitto alivyokuwa akijibu swali kwa kuanza kuweka record sawa ambazo yule mbwana aliziongea kabda ya zitto.Bora hasingefika kuliko kukimbia.

Umimi wa Zittohauhitaji JF kuuthibitisha, kipimo kidogo ni kule tuu kutostand crticisim. Alikuwa mchangiaji mzuri tuu humu ndani, alipokwaana na macritic humu alitukimbia na kuhamia kule kwa wana bidii, huko nako yalipomtokea jamaa kajifunika kwenye ile shell yake 'mimi'.
Kwa vile yeye ndie thread starter wa hii thread sio ameiazisha ili kubadilishana mawazi nasi, bali kaileta ili kutuambia niangaieni, tumeangalia tukitegemea atakuwa nasi kwenye michango au kujibu hoja, kumbe no! Ilikua nioneneni. Sasa si mmeshaniona, inaosha!.

Zitto nakuomba come back hata kusema tuu "thanks for your observations and comments" tutatosheka, huku kukaa kimya ni dharau, kiburi, jeuri na kujisikia!
Please!.

Pasco,
Kwanza nakushukuru kwa kufuatilia mdahalo. Pia nawashukuru wana JF wengine wote. Pia nawashukuru kwa maoni yenu juu ya mdahalo huo.

1. Kwamba sikumtaja dkt. Slaa katika mdahalo - nilitaja chama changu mara nyingi sana. Suala la Reli nililijibu kwa kuonyesha kuwa CHADEMA tayari tumeshafanya kupitia hoja ya Mhe. Arfi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama. Nilipokuwa najibu suala la Kilimo nilieleza kinaga ubaga kuhusu sera ya Kilimo ya chama chetu. Mara zote nilikuwa nikisema kuwa iwapo chama chetu kikiunda serikali. Mara zote nilikuwa nikisema kuwa 'sisi tumeshafanya' na sikutamka hata mara moja 'mimi nimeshafanya'
2. tukumbuke mdahalo ulikuwa unanifanya nidefend record yangu katika utendaji wa kazi. Wenzangu watasema mengi sana kwa kuwa wana uhuru wa kusema tu. Mimi lazima nionyeshe kuwa nimetenda kama Mbunge.
3. Nimefurahi kuwa jamii imemwona mgombea wa CUF na kumtathmini. Yeye anataka kuchaguliwa kwa utajiri wake. Mimi naomba kuchaguliwa ili kutumikia watu.
Nawashukuru kwa kufuatilia

Zitto ni mbinafsi sana nakumbuka hata pale UDSM wakati tunasoma aliendesha mgomo na baadae akatusaliti wana DARUSO. He is a very strong politician na inaonyesha anakubalika sana ila team work ni muhimu sana hasa kwa yeye anayetaka kugombea uraisi mwaka 2015 kwa tikiti ya CHADEMA. Hivi wana bifu gani na Dr.Slaa jamani?

Hebu nikumbushe ni lini nilisaliti UDSM. Nikumbushe jambo moja au mgomo mmoja tu.....!

Hebu nikumbushe ni lini nilisaliti UDSM. Nikumbushe jambo moja au mgomo mmoja tu.....!

Mkuu pole na majukumu na hongera sana kwa kuyaepuka yale watu wenye upeo finyu wanataka kukupeleka (i.e. siasa za kujadili watu badala ya substance (vitu muhimu)). Ushauri wangu ni si lazima uyajibu maoni yao kwani humu JF everyone is entitle of his/her own opinion. Pia kama researcher tuna msemo unasema hivi we agree to disagree hivyo kama kuna watu watakuona wewe msaliti au uko katika mgomo waache na mtazamo wao wewe fanya kazi. ni hayo tu mkuu !!!!

Mhe Zitto mimi nakufahamu toka kibohehe sec, sina shaka wewe ni mwanamapinduzi... temtation ziko juu na zitaendelea kuwepo kwako, ila unachotakiwa kwa sasa ni kuelekeza nguvu zote ktk kukitumikia chama hasa ktk kipindi hiki ambapo chama kina hitaji ma-strategist kama wewe... duru ya pili ya kampeni ni vema mkaambatana na timu nzima ya chadema na mkatuhakikishia kuwa chadema ni wamoja na mko tayari kutuletea mabadiliko tunayoyatarajia na si kama ambayo ccm wanavyo wanadi ...Wabillah Tawfiq ... Mzawa

Zitto hongera sana kwa mmbo makuu mawili. Moja umeonyesha kuwa walikuamini mwaka 2005 na umedhihirisha kwamba wapiga kura walichoamini ndicho umekifanya. Kwa ufupi, bila kuuma maneno hata JK angefanya kama ulivyofanya wewe , naye mwaka huu asingepata taabu na ukweli ni kwamba asingehitaji kuweka mapango kila sehemu, Kiongozi akiwa madarakani matendo yake yanatakiwa kuwa ndio mabango yake; hata hivyo wapiga kura tutumie fursa hii kuona kwamba ukiona mtu ameshakuwa kiongozi halafu anaweka mabango mwngi, huyo hatufai.

Pili, mimi Zitto nakuelewa kiasi fulani. Nakumbuka tulipokuwa mlimani, ulikuwa na uwezo wa kujenga hoja vizuri sana, mimi nilikuwa kiongozi wa darasa wakati huo, pia nilikuwa naingia bungeni. Hata hivyo, nikapata fursa ya kuwa Rais wa DARUSO. Mwaka nauhifadhi kwa sasa.

Nyongeza.
Kaka yangu Zitto, kwa sasa chunguza tuhuma kwamba huenda wewe na Slaa kuna tofauti, please ondoa hilo kama lipo, ukweli unaujua wewe kaka yangu. Nchi hii tupo pabaya, tunahitaji chadema; mimi ni mpenzi wa siasa, lakini nchi hii haitupi muda wa kutosha kushiriki mambo hayo, tumebaki ku tumia ma-saa ma 4 kila siku barabarani, unarudi nyumbani umeme unakatika katika tu, bei ya vitu wote mnaona, katika yote haya, ninyi akina Zitto ambao nasema mmebahatika kuwa katika siasa kwa sasa, tunawaomba Muungane ili mtusaidiawatanzania ambao tunasumbuliwa na CCM.

Nakutakia wewe na chama chako ushindi.

Mwisho, baada ya uchaguzi, anomba muandae programme maalum ya kutafuta vijana wote waliokuwa makini maeneo mbalimabli na muone namna na kuwavuta katika kushiriki siasa hizi,ukweli ni kwamba serikali yetu inawapoteza wanaharakati mbalimbali kwa makusudi.

Ipo siku tutawasiliana zaidi baada ya uchaguzi, maana wengine kwa sasa tunatoa ushauri, lakini lazima tuingie uwanjani hatuwezi kukubali nchi iharibiwe na Mungu pengine katupa elimu na talanta za uongozi.

Kila la Kheri.

Kipindi kilikuwa kizuri sana jana na Zitto aliweza kujieleza vizuri nilichoshangaa ni yule mgombea wa NRA Khamis Fadhili Kiswaga a.k.a Ghulamali alikuwa na personal attack kwa Zitto badala ya kunadi sera za chama chake nakumbuka huyu alikuwa kada muhimu sana wa CCM pale kijijini mwandiga miaka ya nyuma my perception ni kuwa jamaa ni kibaraka au anatumiwa tu kugawa kura na sidhani kama atapata kura kwenye jimbo kwani hata influence hapo kijiji na jimboni hana .Big up Zitto unachotakiwa kufanya now Zitto najua utarudi Bungeni jitahidi kero ya maji Mwandiga uishughulikie kwani hiyo ndio ngome yako I dont know how far have u gonne kufuatilia hilo.

Back
Top Bottom