jeuri ya tajiri wa kijijini hiyo..umeiona?.......kama issue ni utajiri, basi asigombee, akawasaidie wananchi kimya kimya.huyu mgombe wa CUF anadharau sana, anasema masikini, hawezi kumsaidia masikini mwezake, anasema wampe yeye ili awasaidie
Katika kipindi cha TBC1 cha Mchakato Majimboni, mgombea Ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ametia fora na kuwapiku wagombea wenzake huku akishangiliwa na watu waliofurika kwenye ukumbi ambapo kipindi hicho kilirekodiwa na kurushwa hewani, kuanzia saa 3 usiku, Jumamosi, Oktoba 2, 2010.
Kabwe alijieleza vema kuliko kila mgombea na kudhihirisha kwamba CHADEMA bado inakubalika, na ina mipango dhahiri ya kuliendeleza jimbo hilo, mojawapo ya mipango hiyo ukiwa ni ule wa kuileta kampuni inayosimamia masuala ya reli nchini Ujerumani, kuja kusimamia uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania, kwa msaada, kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani, kwa muda wa miaka miwili.
Zitto alisema: Sio kwamba tutafanya nini, ni kwamba, tunafanya nini. Tupendi nafasi tuweze kuendelea kutekeleza mipango yetu ambayo tayari imeonekana.
CCM na vyama vingine vitapaswa kufanya KAZI YA ZIADA kumwondoa Zitto kwenye jimbo hilo! Ama kweli, ni KAZI NZITO kumwondoa ZITTO kwenye jimbo hilo!
-> Mwana wa Haki
zitto jibu maswali ya wana jf tafadhali,kukaa kwako kimya kunafanya watu wasikufikirie vizuri..
Kwa nini hauonekan kwenye kampen za dr slaa ilhal wew ni mmoja wa wa vijana wa chadema wenye ushawishi katika jamii?

Kamtaja kwa lipi? amemsifia au?

Hajamtaja hata chembe Slaa? You don't tell me...!

Ukiwa na muda fuatilia kipindi hiki leo
Ukiwa na muda fuatilia kipindi hiki leo

Alimtaja Said Arfi tu na jinsi chadema ilivyokwishaanza kushughulikia swala la TRL. Na
ona kama lengo lake pale ni kujinad tena ilitakiwa uwe mhafidhina. Naona tajiri wa CUF alimchanganya ndio maana ikabidi aongeze nguvu zake. Ngoja tusubirie siku zinavyokwenda tutathibitishawacwac wa wana JF juu ya umimi wa Zitto

Umimi wa Zittohauhitaji JF kuuthibitisha, kipimo kidogo ni kule tuu kutostand crticisim. Alikuwa mchangiaji mzuri tuu humu ndani, alipokwaana na macritic humu alitukimbia na kuhamia kule kwa wana bidii, huko nako yalipomtokea jamaa kajifunika kwenye ile shell yake 'mimi'.
Kwa vile yeye ndie thread starter wa hii thread sio ameiazisha ili kubadilishana mawazi nasi, bali kaileta ili kutuambia niangaieni, tumeangalia tukitegemea atakuwa nasi kwenye michango au kujibu hoja, kumbe no! Ilikua nioneneni. Sasa si mmeshaniona, inaosha!.
Zitto nakuomba come back hata kusema tuu "thanks for your observations and comments" tutatosheka, huku kukaa kimya ni dharau, kiburi, jeuri na kujisikia!
Please!.
Zitto ni mbinafsi sana nakumbuka hata pale UDSM wakati tunasoma aliendesha mgomo na baadae akatusaliti wana DARUSO. He is a very strong politician na inaonyesha anakubalika sana ila team work ni muhimu sana hasa kwa yeye anayetaka kugombea uraisi mwaka 2015 kwa tikiti ya CHADEMA. Hivi wana bifu gani na Dr.Slaa jamani?
Hebu nikumbushe ni lini nilisaliti UDSM. Nikumbushe jambo moja au mgomo mmoja tu.....!