Mchakato wa ajira za ualimu mwaka 2025 si wa haki, umekaa upendeleo

Umemaliza Mkuu.
 
Unataka kusema nini mkuu, usimuite mpumbavu unamtia hasira
Sasa mkuu, ht mm hua nafeli kwenye usaili ila sio kupata 0 aisee, yn miaka yote uliyosoma unapataje 0 c bora ushindwe kuendelea na usaili ila una 50%+ unaonekana haikuwa bahati yako ila ukipata 0 bc huo n upumbavu
 
Wapumbavu pekee ndio hawatokuelewa hapa.
🤝
 
Sasa kama ni swali la usaili si ushapata 0! Humu hamna lolote kazi kujifanya wakongwe wa usaili kichwani ni sifuri
Mkuu, tambua kuwa hakuna mtu anayejifanya mkongwe wa usaili humu ndani, tatizo lenu waalimu ndio mara yenu ya kwanza kufanya usaili hvy mmekutana na kitu kipya mnaona kama mnaonewa, hata sisi wa kada zingine tulipoenda usaili wa utumishi kwa mara ya kwanza tuliona kama tunaonewa kama mnavyoona nyie sasa hv, ila baada ya kujua jinsi walivyo na sisi tumebadilika na ndio sasa tunawapa ukweli wa jinsi utumishi walivyo ila sasa nyie kwakuwa mmeamua kukaza kichwa bc ht hamuelewi mnaona kama tunawakejeli.
 
Umeeleza vyema kwamba psrs wameweza kurudisha tumaini kwa watoto wa hohehahe lakini sikubaliani na wewe kwamba kozi Fulani Zina maana au waliosoma hizo za wanaoitwa 200+ walipenda, na Wala ukiajiriwa sio kwamba umemaliza mitihani yote Chini ya jua. Chunga mawazo na mwandiko wako Kila kada Ina hitajika sana sana kwenye jamii.

Sema hizo mnazokuwa Wachache ziko kwenye kipaumbele na ufadhili mkubwa wa Dunia kutokana na ajenda za mifumo inayoitawala. Usikufuru kijana.

NB. Ukatubu.
 
Hebu jibu hilo swali hapo juu wenzio wamelishindwa wakakimbia jaribu wewe ili tuone kama zimo
 
Nakubaliana na wewe na hivyo vyote ninavyo issue ni kuwa utumishi wanatakiwa wakupe mtihani kulingana na course msailiwa alizosoma

Sio fair kumuuliza msailiwa course ambazo hajasoma either subject content au core courses hasa za psychology

Mfano geogaraphy wametoa course ya guidance and councelling tena kwa ku cite na maswali kama according to Elton's theory... ambayo unahitajika kukariri argument za huyo philosopher huku hiyo course si wote wa education tunachukua hasa wa BAED. Watu wa Udom ndio huwa wanasoma iyo course

Sasa tukisema haya kuna kunguni himu kisa anaeyasema haya ni mwalimu na wameshazoea kuburuzwa na utumishi kila kitu wanapinga na kukashifu
 
Pass mark inategemea wanahitaji watu wangapi mfano walikuwa wanachukua watu mara tati ya idadi wanayohitaji wanaenda oral
 
Yaap tena nimepunguza ni miaka 35 kazini ila sio continuous unastaafu sehemu unaunga kwingine kwa mikataba ninapoandika haya ni nyani aliyekwepa mishale mingi.
Nimeona mengi na tena tusilaumu nchi yetu ni nchi nyingi tu duniani
Hata raisi akiingia madarakani wakati mwingine anaweka watu ambao anaona watamtii na anawaamini huwezi weka watu wakawa kikwazo kwako basi na makazini ni hivyo wakati mwingine
 
Ndio maana mimi kwenye kufanya usaili ili kuwa fair nilikuwa natumia computer naweka conditions flani kwenye excell yenyewe ina prune.Wanaobakia naweka vigezo vingine tena baada ya mtihani flani na prune tena hivyo hivyo hatimaye nitabaki na wachache sana.
Sasa hao wachache ndio kwenye oral niwe fair naitisha jopo la watu kumi kila mmoja anamuwekea mtu marks kwa kificho kisha tunakusanya lazima utapata the best cream
 
Pass mark inategemea wanahitaji watu wangapi mfano walikuwa wanachukua watu mara tati ya idadi wanayohitaji wanaenda oral
Unahitaji watu 900 unaita interview watu 28000 upo sawa kichwani?
 
Sasa wewe utakuwa mwalimu gani usijui mambo ya counseling and guidence hujui?Hivi unajua maana aptitude test?
 
Mwl wewe wenzio hilo swali wamepata
 
Ni kweli ila basi mchujo unatakiwa kuwa fea na watu wakilalamikia mapungufu isionekane eti kisa ni walimu hapana mnakosea sana
Lazima ujue kutofautisha kati ya mtihani na usaili!
 
Kwa hiyo kada zingine wanaofanya mtihani? Hivi utawapaje ajira walimu 200 kati ya walimu 2000 bila usahili?
 
Yanapima uelewa
Kwaiyo wewe shule hukujifunza
Newton's law of motion
Archimedes principle
Nyerere socialism
Au hujui haya ni mawazo ya watu na inatakiwa uyajue, tuone uelewa wako
Shida watu hawakuwai fanya usaili …. Ndio maana wanashangaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…