Mchakato wa kuajiriwa kocha Amunike

Mchakato wa kuajiriwa kocha Amunike

valet de chambre

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2017
Posts
1,044
Reaction score
1,112
Wakuu amani amani! Kwa wale wenye kumbukumbu naonmba kujua mchakato wote wa kuajiriwa kocha Amunike na kwamba alishindanishwa na makocha gani hadi akashinda nafasi hiyo.

Nawasilisha wakuu maana dah!
 
Nataka kujua jinsi mchakato wa kupatikana kwake ulivyokuwa hadi akapewa timu. Alkpambanishwa na nani hadi akashinda nafasi hiyo.

Shida siyo kocha, shida ni wanaofundishwa.

Unadhani ni kocha gani alipita Bongo akawapa mafanikio makubwa kupita Amunike?
 
Hoja nzuri sana sema umeileta kwa kizazi kisichopenda kudadisi kilichokaa kimipashomipasho ila ukweli ni kwamba ten percent zitaendekea kutugharimu sana kama taifa
 
Timu za kufuzu zimeongezwa toka 16 hadi 24...lile kundi maximo na poulsen wangefuzu game tatu za mwanzo
Sio kweli angalia rankings za FIFA. .huko nyuma tumewahi kupangwa na vitimu vyepesi hatukufuzu kama Msumbiji
 
Sio kweli angalia rankings za FIFA. .huko nyuma tumewahi kupangwa na vitimu vyepesi hatukufuzu kama Msumbiji
Hivi msumbiji ya wakati ule utailinganisha na msumbiji ya leo!?..msumbiji ile ilikua na wachezaji wengi wanacheza ligi bora,palikua na cape verde ya wachezaj wanaocheza portugal...lakini stars ilikua ikicheza mpira unaoeleweka,tuliifunga morocco goli tatu taifa,tukachezs vizuri dhidi ya ivory coast..sasa hili kundi timu ngumu uganda!!!
 
Eti viongozi wa TFF akiwemo katibu mkuu walienda kuhudhuria mkutano fulani wa CAF sijui ni Misri vilee! Kufika huko wakakutana na moja ya watoa mada wa ule mkutano ambaye ndiye huyu Amunike wetu!

Viongozi wetu wa soka wakapagawa na yale madini ya Amunike; baada ya kutoka kwenye kikao wakamuomba namba! Mawasiliano yalianzia pale mpaka kufikia muafaka wa kuingia mkataba wa kujiunga na Taifa Stars!

Nakumbuka nilimsikia Jemedari Said akisimulia kwenye kipindi cha Sports Am cha Bin Zubery, Azam tv.
 
kulikuwa hakuna mchakato unaoeleweka ila ni maamuzi tu ya watu wachache kiutaratibu nafasi inatangazwa, makocha wanatuma maombi baadae mchujo unafanyika kwa kuangalia sifa waliopita kwenye mchujo yanaanza mazungumzo ya mishahara kujua nani yupo nafuu lakini kwa Amunike ni kama mkurugenzi wa ufundi wa TFF alivyochaguliwa au katibu wa tff alivyochaguliwa
 
Hivi haiwezekani team ya taifa ikawa na wachezaji wote wasio kwenye vilabu vya nyumbani? Sababu naona mda mwingi wachezaji wanakuwa kwenye vilabu vyao.. Tunataka wachezaji watakao kuwa kwenye kambi mda wote
 
Back
Top Bottom