Mchakato wa kuingiza Ukraine ndani ya NATO waanza rasmi

Nato kuikubalia Ukraine, maana yake itakuwa kuingia vitani immediately. Sidhani kama kuna watu wana hiyo appetite.
 
Nchi yeyote kumegwa hata kipande cha saizi ya kiwanja cha mpira wa miguu ni dharau kubwa sembuse mini minne tena eneo kubwa na lina rasilimali ? ingekuwa miji hiyo kuchukulia sio kitu Ukraine asingehaha kupiganiwa na kutaka kuirejesha..

Hamna nchi iliyomegwa, Warusi na liinchi lao libwaku na usupapawa wao wameshindwa kupambana na kainchi kadogo jirani hapo halafu wakajitangazia kumega tena katikati ya mapambano, ni aibu sana kwa mliokua mnategemea Urusi kama supapawa wenu, hata waarabu wenu raundi hii wamekubali kwa Urusi walipigwa bao.
 
Mkuu vipi Updates za miji 4 ya Ukraine kumegwa na Urusi baada ya kura za maoni
Update zipo sana jamaa wako vitani na wakati Putini juzi anaadaa sherehe Ukrean walifanikiwa kukomboa kijiji la Lpyanski, lakini siku ya pili pia jeshi la Ukrean likasonga mbele na kukomboa kijiji cha Lyman kuelekea Donbas

Putini ana hali mbaya sana, na sasa kushambulia Russia imekuwa ni kazi rahisi wale askari wake wakihisi wamezingirwa tu wanaacha silaha mikono juu wanajisalimisha wenyewe.

On top of that, maombi rasmi ya kujiunga NATO jana yamesainiwa na Rais wa Ukrean, ni kusema kwamba ombi likikamilika jeshi la NATO litahusika fully kumchapa jamaa yako ambaye sasa anapumulia mashine, jeshi hana amepeleka askari laki tatu wa JKT baada ya miezi 7 tu.
 
Maelezo meeengi nonsense soma hapa kutoka Pentagon
White House responds to Ukraine’s NATO request

Now is not the time, says national security adviser Jake Sullivan.

View attachment 2373403
 
Nchi yeyote kumegwa hata kipande cha saizi ya kiwanja cha mpira wa miguu ni dharau kubwa sembuse mini minne tena eneo kubwa na lina rasilimali ? ingekuwa miji hiyo kuchukulia sio kitu Ukraine asingehaha kupiganiwa na kutaka kuirejesha..
Russia amefanyiwa dharau mara ngapi kwani? Si alisema Ukrean haitawezekana kujiunga na NATO? Zelensky jana kapeleka maombi rasmi, tusubiri tuone,
 
Maelezo meeengi nonsense soma hapa kutoka Pentagon
White House responds to Ukraine’s NATO request

Now is not the time, says national security adviser Jake Sullivan.

View attachment 2373403

Pentagon nakwenda kufanya nini, frontline iko Ukraine, hebu hii picha iwape aibu kidogo kwamba kainchi kadogo kamelitoza kamasi lisupapawa lote hilo....
Waarabu wa bongo mnatia huruma.



 
Angepewa credit kama angefanya chochote cha maana hapo Kyiv, limsafara lote lililiwa, halafu kataifa kadogo kama Ukraine kamemkula kichwa mpaka jeshi lake limeshindwa imebidi afuate wanywa gongo mtaani.
Huyu hata waarabu wenu kwa sasa hawamtaki...
Ushabiki mandazj hujui chochote
 
Ushabiki mandazj hujui chochote

Ha ha ha!! Hasira zote hizo, ila nawaelewa sana maana sio kwa ule mzuka mlianza nawo wa limsafara la kwenda kufunika Kyev, binafsi niliingiwa hofu kuu, ila kwa ambavyo lilipigwa na wabeba javelin hadi raha.
 
Vipi Ukraine akikubaliwa NATO?
Itakuwa piga nikupige....uwezo kwa uwezo
Sijui kama kanuni za nato zinaruhusu taifa lenye vita kujiunga, kama litaruhusiwa basi vita itabadili sura
 
mkuuu naona unazungumzia ukombozi wa vijiji viwili,

mimi nimeuliza updates za majimbo 4 ya Ukraine ambayo wakazi wake wamepiga kura na kuchagua kuwa sehemu ya Urusi.
 
Pentagon nakwenda kufanya nini, frontline iko Ukraine, hebu hii picha iwape aibu kidogo kwamba kainchi kadogo kamelitoza kamasi lisupapawa lote hilo....
Waarabu wa bongo mnatia huruma.



Ukraine ndio nchi ya pili kwa ukubwa pale ulaya ukiitoa Russia alafu unasema ka nchi kadogo[emoji23][emoji23] na kingine jana wamemkatalia live zelensky kuingia NATO wazungu wanapenda maisha wewe yani watu waiangamize miji yao kwa ajili ya Ukraine[emoji23][emoji23] Yani london,paris,berlin,warsaw na miji kwa ajili ya zelensky unaota na endlea kuota
 
Naomba putin ashindwe vibaya hii vita maana analeta economic depression na njaa duniani with his own interest.
 
mkuuu naona unazungumzia ukombozi wa vijiji viwili,

mimi nimeuliza updates za majimbo 4 ya Ukraine ambayo wakazi wake wamepiga kura na kuchagua kuwa sehemu ya Urusi.
Vijiji mkuu ndivyo vinavyotengeneza jimbo, jimbo ni eneo kubwa sana sio kam huko kwenu, Ukrean ni nchi kubwa sana eneo lake la ardhi sasa kwa vita usitegemee kwa siku1, HIMARS zinaendelea kumtesa Russia watu wako kazini ni suala la muda kila kitu kitarudi kwenye mipaka yake Ukrean
 
Huyu jamaa MK254 reasoning yake inatia shaka sijui kosoma shule zipi yaani hata vitu vidogo kwake ni shida kuelewa nimecheka sana eti anasema Ukraine kainchi kadogo..
 
Lete uthibitisho kwamba jana hiyo hiyo ombi lake limekataliwa
 
NATO walisha sema Ukraine, haiwezi ingia NATO leo au Kesho. NATO wanajua fika kuingia Ukraine NATO ni fujo kwa Ukraine. Hivyo watachelewesha hata miaka 5 mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…