Mchambuzi Amri Kiemba unamuonaje?

Mchambuzi Amri Kiemba unamuonaje?

mugah di matheo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6,307
Reaction score
12,410
Mchezaji wa zamani wa simba, yanga, kagera na stand united baada ya kustaafu kucheza amehamia kwenye Tasnia hiyo akiwa anafanyia kazi clouds media. Kipindi ni kila siku saa 3 usiku na jumapili saa 7 mchana

Wewe mdau unamuonaje Amri Kiemba?

Amefanikiwa kwa hilo?

Je, anaonyesha mapenzi na timu ipi ya kariakoo?

Ungemshauri aongeze kipi ili afanikiwe zaidi?
 
Sasa ndugu yetu Amri Kiemba, si ungetutajia na ratiba ya hicho kipindi cha michezo unacho chambua hapo Maqingu Redio ili tuwe na uhakika wa kukuangalia na kukufanyia tathmini.

Hongera sana kwa kupata hilo shavu la uchambuzi.
 
Amri Kiemba ni mchambuzi wa kweli,hasemi kwa hisia kama wengine waliopo Clouds.

Anajaribu kuusema ukweli ulivyo na mimi huwa namuelewa sana.Hana utopolo kama wenzake pale
 
chambua wa azam na yule mwenzake ndio ninaowaamini na kuwaelewa kuliko wachambuzi wote jamaa huweka ushabiki pembeni waongeapo ukweli
 
Kiemba ni bonge la mchambuzi, anazungumza vitu vya kitaalamu ambavyo mchambuzi ambaye hajacheza mpira siyo rahisi kuvifahamu. Hana mbwembwe, anachambua kwa utulivu wa hali ya juu.
Clouds wamepatia sana kuwa na huyu mwamba.
 
Kiemba ni bonge la mchambuzi, anazungumza vitu vya kitaalamu ambavyo mchambuzi ambaye hajacheza mpira siyo rahisi kuvifahamu. Hana mbwembwe, anachambua kwa utulivu wa hali ya juu.
Clouds wamepatia sana kuwa na huyu mwamba.
Yupo vizuri sana. Nipo namsikiliza hapa
 
Back
Top Bottom