Hapo ndo kazi ya mwalimu inapoonekana.
Kama mchezaji hajitumi mtie benchi weka wengine wacheze.
Kuna wachezaji pale Simba hata wakicheza pumba kila siku hawana pressure maana wana namba za kudumu (Mfano Zimbwe, Kapombe, Saido, Mzamiru et al).
Kocha hafanyi rotation ya wachezaji, kila mechi watu walewale na ameshindwa kabisa 100% kupandisha morali ya timu.
Mwanzo ALITUDANGANYA eti anapenda mchezo wa kasi na kusema akina Chama wanamchelewesha, lakini hivi ukiangalia toka aje yeye na kabla yake, kipi kimeongezeka kiuchezaji tofauti na kushuka?.
Timu inapata matokeo ya kimchezo yatokanayo na uwezo binafsi ila sio mbinu za kocha.
Hata ukiangalia timu inavyojipanga wakati wa kushambulia au kukaba ni kituko. Kuna gap kubwa sana na mashimo mengi uwanjani yanayoachwa wazi.
Simba tumezoea ball linatembea dakika 90 kwa kasi na matokeo yanapatikana. Hata likifungwa goli moja wakati ball limetembea washabiki tulikuwa tunafurahi tofauti na sasa ambapo hata tukishinda 5 bila nadhani bado hatutakuwa na furaha.