Mchambuzi maarufu wa siasa kutoka Kenya, Herman Manyora, amezua gumzo baada ya kudai kuwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, hatoweza kumaliza kipindi chake cha miaka mitano madarakani.
Akizungumza katika mahojiano na Tedd Agwa, Manyora alisema hali ya kisiasa nchini Tanzania inaashiria anguko la Chama cha Mapinduzi (CCM), akibainisha kuwa uongozi wa Rais Samia umeathiri uimara wa chama hicho tawala kwa tuhuma zote chafu dhidi ya chama hicho ambayo inaweza kugharimu muda mrefu kurejesha imani yake kwa wananchi
“Hakuna namna Samia ataweza kumaliza miaka mitano madarakani,” alisema Manyora, akisisitiza kuwa hatua na mienendo ya kisiasa ya rais huyo “imeharibu misingi ya CCM kutoka ndani.”
Manyora pia alizungumzia kukamatwa na kushtakiwa kwa kosa la uhaini kwa kiongozi wa upinzani, Tundu Lissu, ambaye alikuwa mpinzani mkuu wa Rais Samia. Hata hivyo, alisema kuwa hata kama Lissu angekuwa huru, bado ingekuwa vigumu kwake kumshinda Samia kutokana na ushawishi mkubwa wa CCM katika Siasa