Dear Wana JF!
Natumaini wote mpo poa kabisa, Na tunaendelea Sukuma Gurudumu la maendeleo ya taifa letu hili hili. Mimi nikiwa kama Mjasiliamali ambae tayari nimeshaingia katika Soko(Mapambano) nina swala nataka msaada kwa wale ambao watakuwa interested.
Mimi nina Business IDEA ambayo yatakiwa andikiwa Business Plan. Kama kuna Mtu/Watu wanataka kushare hii Idea na mimi, tukaweka team ambayo itakuwa na wataalam. Tukaandika Business Plan & Proposal nzuri, tukaomba Oppointment mahala, Nakuambia Hatuwezi kosa. Ni biashara Nzuri na inaendana kabisa na Karne hii ya Sayansi na Technolojia 100%. Cha msingi ni sisi wenyewe tu kujitoa.
Mimi kwa Ufahamu wangu mdogo tu nilionao hakuna kitu huwa nakiamini sana katika kuanzisha biashara kama Rasimali WATU, Maana bila kuwa na Watu hakuna kinachoweza fanyika, Vitu kama Fedha n.k huwa vinakuja Baadae, Mtanirekebisha kama nimekosea. So kama mtu amenielewa basi tufanye mawasiliano!
Nasema hivi wawekezaji wapo wengi tu hapa kwetu Tanzania. Kwa Mfano NSSF! wana Fedha nyingi lakini hawana hata Idea ya Biashara gani wafanye, Kila kukicha wanajenga Majengo tu na kuweka fedha katika Fixed account za Mabenki, Huku watanzania tunalilia Mitaji!
Tujipange ndugu zangu, Elimu ndio hizi tunazo! tusitegemee sana kuajiriwa!
Nakupa Hints tu ya Biashara yenyewe;
Kwa Mfano ukienda dukani nunua shati? Unauziwa mashati yote yalio Dukani? au wauziwa shati ambalo ni size yako na ambalo wewe umelipenda na ambalo linaendena na bajeti yako. Au Sio? Sasa why wao wanatuuzia vitu ambavyo hata hatuvihitaji na vingine hata huwa hatuvitumii kabisaa ila wanakupatia tu na gharama yake ipo juu.....!!!!
Sasa Tafakari.......Alafu Chukua hatua