Mchanganuo wa gharama ya kulima ekari moja ya mahindi

Pole sana,hawaweki wazi changamoto ya hali ya hewa.
Hapana, hao wanaoleta mrejesho wanatokea maeneo ambako kuna Kilimo cha mahindi ndiyo maana wanazungumza habari ya kuweka mbolea! Mavuno waliyozungumzia ni ya kawaida kabisa! Wilaya ya Tanganyika wanalima bila mbolea lakini hawakosi magunia 15-20 kwa ekari. Changamoto ya kubwa ni udhibiti wa post harvest losses, mazao mengi yanapotea wakati wa uvunaji. Unakuta mahindi yanaoza kutokana na wingi wa mvua!
 
Hujataja ghalama za Mbolea. Heka moja inahitaji wastani kilo 200 za mbolea. Mfuko wa kilo 50 unauzwa wastani 100,000 x 4 = 400,000.

Jumlisha 600,000 + 400,000 = 1000,000/= hiyo ndiyo ghalama halisi ya kuihudumia ekari moja ya zao la Mahindi.
 
Shukrani bro...barikiwa sana...
 
Ili kulima kitaalamu kwanza inatakiwa kujihakikishia upatikanaji wa maji yawe ya mvua au kumwagilia.

Pili ni ardhi inayokubali hilo zao liwe la Mahindi au lingine.

Tatu shamba lilimwe kwa Trekta kwakuwa katika ekari moja ukilima matuta ya jembe la mkono linatoa matuta 70 hadi 75 hiyo ndio mistari au matuta ya kupanda Mahindi yako.

Shamba likilimwa kwa trekta linatoa mistari 120 hadi 130 kama mistari ya kupanda Mahindi yako.

Shamba hilo likipata maji, mbolea na palizi sahihi katika muda sahihi.
Shamba la kulima kwa mkono linatoa gunia za kilo 120 kuanzia 15 hadi 25.

Shamba la kulima kwa Trekta linatoa gunia za kilo 120 kuanzia 25 hadi 35.

Hivyo Basi Kama nilivyoeleza pale juu kuwa wastani Ekari moja ya Mahindi kitaalamu kabisa inahudumiwa kwa ghalama ya Tsh 1000,000/=

Na kwa wastani Kama soko la Mahindi litakuwa la kawaida Mwenye kulima kwa jembe la mkono atatarajia kupata wastani wa shilingi 1500,000/= hadi 2,000,000/= kwa ekari moja.

Yule wa Trekta atatarajiwa kupata shilingi 2000,000/= hadi 3,000,000/= kwa ekari moja.
Shamba linatakiwa kuwa chini ya uangalizi kwa masaa 24 Kama mtoto mchanga.

Kasoro yoyote inayojitokeza inapaswa kuhudumiwa mala moja na kwa utaalamu wa kilimo.
Ni vema kulima kalibu na chanzo cha maji ili mvua ikiwa ya mashaka Basi limwagiliwe na maji yaliyokalibu.

Hivyo Mota japo ya Mchina iwe inawaka na inamafuta muda wote.

Jambo lolote likifanywa kitaalamu linaleta tija.
 
Nimenote kitu hapa
 
Mchanganuo wa kilimo cha .... Kwa heka Kulima elfu 60 mbegu kilo elfu30 yaitajika kilo 5 kupanda elfu20 kupalilia elfu 30 kuvuna elf50 ikiuza jumla unapata m19 kwa hekar moja unajua kilimo cha nn hicho tulia tunalima wachache
 
Safi hio ni specific kwa eneo gani na wilaya ipi?
hizo hesabu umepigaje hapo?
 
Mchanganuo wa kilimo cha .... Kwa heka Kulima elfu 60 mbegu kilo elfu30 yaitajika kilo 5 kupanda elfu20 kupalilia elfu 30 kuvuna elf50 ikiuza jumla unapata m19 kwa hekar moja unajua kilimo cha nn hicho tulia tunalima wachache
KILIMO cha upupu
 
Ngoja niweke kambi hapa nawaza huu mwaka ishu za kilimo nifanye,
Kuna mwenye uzoefu wa Kahama kuhusu mvua
Kahama kwa mahindi hamna Huwa yanaungua sana labda mpunga ni fresh
 
Faida ya Tsh 600000 kwa ekari igawe kwa muda uliotumia kusubiri pesa yako irudi.
Kuanzia mwezi wa kulima (mwezi wa 12 kwa Songwe) mpaka muda ambapo bei ingalau imepanda (Mwezi wa 8)
600000 / 9 = 67,000 TSH (Hii inamaanisha kila mwezi ulikuwa ukiingiza Tsh 67,000 tu ambayo haitoshi kulisha familia).

Ili ufaidike kwenye kilimo cha mahindi inabidi uingize ingalau Tsh 2500000 kwa mwezi

2500000/67,000 = 37 ekari

Inabidi ulime ingalau ekari 35 za mahindi ndo uone faida na kusomesha watoto shule nzuri!

Aksante
 
Kiufupi mbolea lazima mifuko 3 Kwa kiwango Cha chini kabisa ,dawa za Wadudu na wastani wa gharama Kwa ekari 1 ni Kati ya 650k-700k ila una guarantee ya kuanzia gunia 25 kwenda Juu.
 
Wacha kutisha watu.Ekari 10 zinakupa faida nzuri,hapo ni gunia minimum 250 *50,000=12,500,000 ambapo gharama zote sio zaidi ya 5,500,000.

Unavyolima ekari nyingi ndivyo unit cost inapungua
 
Mvua ni ya kwako? Wadudu? Palizi?
Kama unalima Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Magharibi kuanzia Kagera mvua ni uhakika haijawahi Goma hata siku Moja.

Huko kwingine Sina uzoefu ila ni tia maji tia maji.
 
Kwa haraka haraka naweza sema mikoa kama Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Songwe, Kagera, Kilimanjaro, Arusha, Tanga mvua huwa haisumbui sana
Plus Kigoma na Kusini ya Morogoro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…