Wakuu Saluti,
Ngoja niwape experience yangu ya Kilimo cha Mahindi Mkoa wa Ruvuma kwa Wilaya ya Mbinga.
1. Kukodi shamba 50,000 - 100,000 inategemea mahali na mahusiano na mwenye shamba.
2. Kulima kwa trekta 60,000, Kwa kutumia vibarua ni kadiri ya makubaliano lakini ni kuanzia 45,000 hadi 70,000
3. Mbegu inategemea na aina ya mbegu ila Mbinga maarufu ni Mbegu aina ya Tembo ya Zambia gharama ni kuanzia 15,000 hadi 20,000 kwa paketi, hapa utahitaji paketi 6.
4. Kupanda, zipo njia mbili. Kwa kutumia vibarua ambapo ni kati ya 4000 -7000 kwa kibarua au kwa kutumia mashine ya kupandia ambapo utalipa kati ya 20,000 hadi 25,000
5. Mbolea hapa utaweka mifuko 5 - 6 kwa awamu mbili (2.5 - 3 kwa awamu). Mbolea maarufu huku ni UREA 70,000/= CAN 65,000/= na SA 55,000/= kwa bei ya ruzuku. Au kama utapata mbolea aina ya YaraMila Cereals hiyo ina mchanganyo wa mbolea zote hizo tatu.
6. Kuweka mbolea, utalipa vibarua kwa kila awamu kwa gharama ya vibarua ambazo ni kati ya 4000 - 7000
7. Palizi ni 30,000 hadi 45,000 kwa hekari. Au unaweza kupiga dawa hapa gharama itategemea aina ya magugu yaliyopo shambani ndio ita-determine gharama ya dawa na bei zake.
Shida ya dawa kuna probability ya kurudia kupiga tena in case haijakubali vizuri na kama mtaalamu ameshindwa kukushauri aina ya dawa kulingana na aina ya magugu lakini pia changamoto nyingine unaweza ukaunguza mazao kunahitajika umakini wakati wa upigaji dawa.
8. Kuvuna na kukusanya mahindi utalipa vibarua in daily basis kwa rate ya 4000 hadi 7000.
9. Kupukuchua mahindi gharama ni 1000 kwa kila kiroba.
10. Matokeo kwa hekari moja kama utafuata hatua zote hizo hapo juu na ukawa haujaathirika na mvua na ardhi ni nzuri hautakosa kupata kuanzia gunia 18 hadi 33.
Gunia moja halitapungua kilo 120 hadi 135 na bei itategemea soko limekaaje. Ila kwasasa bei ni kuanzia 650 hadi 800 kwa kilo.
NB. Bado gharama za usafirishaji, ushonaji wa viroba, kupandisha na kushusha, chakula cha vibarua na gharama za kwenda na kurudi shamba hazijajumuisha.
The higher the expectations the Greater the disappointment. But all in all Mahindi kwa Ruvuma it's a hell of business na kama una mtaji wa kutosha achana na kwenda shambani kulima nenda vijijini weka mzani nunua mahindi.
I hope umepata kitu cha kujifunza.