Mchanganuo wa gharama ya kulima ekari moja ya mahindi

mkuu kg 12 za mbegu ni sawa na miche 24,000 kwny eka moja inawezekana japo wengi tupo kwny miche 17,000 kwa spacing ya 30x90cm
Kitu tunachokosea mara kwa mara ni mbolea, kama tuna ambiwa kila mche tuweke grams 5 ya kila mbole meaning 5x24,000= 120,000gm ya mbolea sawa na 120kg = sawa na mifuko miwili na nusu kwa maana hiyo kwa eka 1 utahitaji jumla mifuko 5 ya mbolea.
Hata kwa miche 17,000 bado utahitaji kilo 170 ya mbolea jumla ni karibia mifuko 3.5 Ukiachilia mbali mvua pia nadhan tunashindwa kufanya vzr kwny kilimo kwa kukosa taarifa muhimu zinazopelekea kupata mazao hafifu.
Na anza rasmi kulima mwaka huu ntajitahidi kufata maelekezo yote ya kitaalamu pamoja na kushare taarifa kwa wanavijiji lilipo shamba ili kubalance stories nitajitahidi kuweka hapa jukwaa pendwa
Karibu sana shambani.
 
Mikoa isiopata njaa na misaada ya chakula hio ndio ina mvua nyingi na mavuno mengi.
Rejea mwaka jana ni mikoa gani ilipelekewa mahindi ya bei rahisi ya serikali, hio ndio ina changamoto ya mvua ikiwemo na mkoa unsoishi wewe maana unalalamika mazao yako kukauka.
Mkoa ninaoishi mimi mwaka wa 15 sijawahi ona mahindi yamepandwa na kukauka kwa jua.
Ukisema changamoyo ya mafuriko na magonjwa nitakuelewa, mfano kyela,kilombero wao hasara kubwa ni mafuriko sio ukame. Hama uko mkuu using'nganie sehemu yenye ukame wakati kuna mikoa naji wao hawana pa kuyapeleka zaidi ya kutiritika mtoni. Njoo mkoa ninaoishi mimi mashamba bei chini mito kama yote.
Hio mito jaba Ryaja Rufiji, Rubuma,Nakafalasi,kagera nk unafikiri maji yake yabatoja wapi ?
My dear jf member, jigrafia tuliofunfishwa shike itusaidia kuijua nchi hii na kujopangia maisha.
Kuna mnyanwezi mmoja nilikutaba nae kwenye treni alisimilua kywa yeye amegama kwao urambo kaenda kilosa kutokana na changamoto za maji na masoko.
Kilosa wamechimba visima wanalima mda wote, masika na kiangazi, usizidi kupoteza mda move.

Umenipa tabu kweli kusoma andiko lako, ebu tulia usiwe na pupa andika vizuri unatuumiza macho!
 
Si edit kwa kweli. Smart keyboard very fucking. Smart keyboard ni teknolojia ya kijinga ktk kuunda maneno. Ni kuingiliana tu herufi zilizokaribu.
Mwanzoni nilidhani ubora wa simu kumbe hata samsang ni wale wale.
 
Huu hapa ni mchanganuo wa kulima ekari moja ya mahindi kwa sasa hivi
1. Kukodi shamba ekari 1 - 70,000/-
2. Kulima shamba mara 2 - 60,000/-
3. Mbegu pakiti 6 sawa kg 12 - 72,000/-
4. Kupanda mahindi - 30,000/-
5. Mbolea 2 - 140,000/-
6. Palizi 2 - 60,000/-
7. Kuweka mbolea - 30,000/-
8. Kuvuna/kupukuchua/mifuko - 100,0000/-

Jumla ya gharama huwa ni 550,000/- ~ 600,000/-

Mavuno
Mara nyingi mavuno hutegemea ubora wa ardhi na matunzo ya mazuri ya mazao, lakini mara nyingi ekari moja ya mahindi hutoa gunia 15 ~ 25, sasa ukipata kiwango cha chini gunia 15 ukauza kwa bei ya sasa 80,000/- unapata Tsh 1,200,000/- faida ya Tsh 600,000 kwa ekari.
kilimo kingekuwa Rahisi hivi kila mkulima angekuwa tajiri

kwa kilimo cha kisasa hyo pesa haitoshi
 
Ngoja niweke kambi hapa nawaza huu mwaka ishu za kilimo nifanye,
Kuna mwenye uzoefu wa Kahama kuhusu mvua
 
Kwa huku niliko, nimekodi ekari 3 Tsh 80,000/
Palizi ya kwanza kila ekari Tsh 21000 mara 3 63000

Ya pili napiga dawa ya magugu 25 kila ekari pamoja na mpigaji.

25000×3= 75000
Mbegu 30 Kg kila kg 10 ni 70000 jumla 210,000/
Kuvuna kila ekari ni 15000 mara 3 45000

Kupiga kila gunia 1000,
Watani gunia 60, so 60,000.

Mbolea mifuko 9 *70000

80000+65000+75000+210000+45000+630000
Total 115000, naongeza laki dharura. So 1,205,000.

Minimum bei ni 50k mara 60 ni 3M.

Hiki ni kilimo Cha mtandaoni tu uharisia hauko hivyo watu tumelima sana lakini hatujawahi kupata gunia 25 kwa heka
 
Wakuu Saluti,
Ngoja niwape experience yangu ya Kilimo cha Mahindi Mkoa wa Ruvuma kwa Wilaya ya Mbinga.

1. Kukodi shamba 50,000 - 100,000 inategemea mahali na mahusiano na mwenye shamba.

2. Kulima kwa trekta 60,000, Kwa kutumia vibarua ni kadiri ya makubaliano lakini ni kuanzia 45,000 hadi 70,000

3. Mbegu inategemea na aina ya mbegu ila Mbinga maarufu ni Mbegu aina ya Tembo ya Zambia gharama ni kuanzia 15,000 hadi 20,000 kwa paketi, hapa utahitaji paketi 6.

4. Kupanda, zipo njia mbili. Kwa kutumia vibarua ambapo ni kati ya 4000 -7000 kwa kibarua au kwa kutumia mashine ya kupandia ambapo utalipa kati ya 20,000 hadi 25,000

5. Mbolea hapa utaweka mifuko 5 - 6 kwa awamu mbili (2.5 - 3 kwa awamu). Mbolea maarufu huku ni UREA 70,000/= CAN 65,000/= na SA 55,000/= kwa bei ya ruzuku. Au kama utapata mbolea aina ya YaraMila Cereals hiyo ina mchanganyo wa mbolea zote hizo tatu.

6. Kuweka mbolea, utalipa vibarua kwa kila awamu kwa gharama ya vibarua ambazo ni kati ya 4000 - 7000

7. Palizi ni 30,000 hadi 45,000 kwa hekari. Au unaweza kupiga dawa hapa gharama itategemea aina ya magugu yaliyopo shambani ndio ita-determine gharama ya dawa na bei zake.

Shida ya dawa kuna probability ya kurudia kupiga tena in case haijakubali vizuri na kama mtaalamu ameshindwa kukushauri aina ya dawa kulingana na aina ya magugu lakini pia changamoto nyingine unaweza ukaunguza mazao kunahitajika umakini wakati wa upigaji dawa.

8. Kuvuna na kukusanya mahindi utalipa vibarua in daily basis kwa rate ya 4000 hadi 7000.

9. Kupukuchua mahindi gharama ni 1000 kwa kila kiroba.

10. Matokeo kwa hekari moja kama utafuata hatua zote hizo hapo juu na ukawa haujaathirika na mvua na ardhi ni nzuri hautakosa kupata kuanzia gunia 18 hadi 33.

Gunia moja halitapungua kilo 120 hadi 135 na bei itategemea soko limekaaje. Ila kwasasa bei ni kuanzia 650 hadi 800 kwa kilo.

NB. Bado gharama za usafirishaji, ushonaji wa viroba, kupandisha na kushusha, chakula cha vibarua na gharama za kwenda na kurudi shamba hazijajumuisha.

The higher the expectations the Greater the disappointment. But all in all Mahindi kwa Ruvuma it's a hell of business na kama una mtaji wa kutosha achana na kwenda shambani kulima nenda vijijini weka mzani nunua mahindi.

I hope umepata kitu cha kujifunza.
 
Ukipata nafasi utuekee na experience yako katika ununuzi wa mazao....asante
 
Huu hapa ni mchanganuo wa kulima ekari moja ya mahindi kwa sasa hivi
1. Kukodi shamba ekari 1 - 70,000/-
2. Kulima shamba mara 2 - 60,000/-
3. Mbegu pakiti 6 sawa kg 12 - 72,000/-
4. Kupanda mahindi - 30,000/-
5. Mbolea 2 - 140,000/-
6. Palizi 2 - 60,000/-
7. Kuweka mbolea - 30,000/-
8. Kuvuna/kupukuchua/mifuko - 100,0000/-

Jumla ya gharama huwa ni 550,000/- ~ 600,000/-

Mavuno
Mara nyingi mavuno hutegemea ubora wa ardhi na matunzo ya mazuri ya mazao, lakini mara nyingi ekari moja ya mahindi hutoa gunia 15 ~ 25, sasa ukipata kiwango cha chini gunia 15 ukauza kwa bei ya sasa 80,000/- unapata Tsh 1,200,000/- faida ya Tsh 600,000 kwa ekari.
Hujaweka gharama za usimamizi! gharama za kwenda shjamba na kurudi toka maandalizi hadi mavuno!

Lakini pia hujasema hayo mashamba ya kukodi yapo wapi!!
 
Huu hapa ni mchanganuo wa kulima ekari moja ya mahindi kwa sasa hivi
1. Kukodi shamba ekari 1 - 70,000/-
2. Kulima shamba mara 2 - 60,000/-
3. Mbegu pakiti 6 sawa kg 12 - 72,000/-
4. Kupanda mahindi - 30,000/-
5. Mbolea 2 - 140,000/-
6. Palizi 2 - 60,000/-
7. Kuweka mbolea - 30,000/-
8. Kuvuna/kupukuchua/mifuko - 100,0000/-

Jumla ya gharama huwa ni 550,000/- ~ 600,000/-

Mavuno
Mara nyingi mavuno hutegemea ubora wa ardhi na matunzo ya mazuri ya mazao, lakini mara nyingi ekari moja ya mahindi hutoa gunia 15 ~ 25, sasa ukipata kiwango cha chini gunia 15 ukauza kwa bei ya sasa 80,000/- unapata Tsh 1,200,000/- faida ya Tsh 600,000 kwa ekari.
🙏🙏👏
 
Back
Top Bottom