Mchanganuo wa kujenga nyumba ya vyumba vitatu na sebule

Mchanganuo wa kujenga nyumba ya vyumba vitatu na sebule

sasa binamu nami nisaidie kujua gharama za ujengaji wa nyumba vyumba 3 sebule, master, choo, jiko, yaani kiwanja kina mita 15x18
binamu mpaka kupaua au...?
nione inbox please, weka maswali yako yote
 
binamu mpaka kupaua au...?
nione inbox please, weka maswali yako yote
Ingekuwa mambo ndiyo yanaenda hivi basi JF ingeshakufa, wekeni mambo hadharani wengine wajifunze pia
 
Zumbemkuu na wadau wengine wa ujenzi:

Hii mada ya gharama za ujenzi imekuwa inakuja mara kwa mara kwenye ukumbi huu. Nami nimekuwa naifuatilia kwani ni shughuli ninayoipenda na ninajishughulisha nayo kwa muda mrefu.

Mimi ni mhandisi lakini siyo wa ujenzi, japo uchoraji na upigaji wa hesabu ndiyo shughuli yangu ya kila mara. Kwa kipindi kirefu nimekuwa natumia MS Excel kurahisisha makisio ya gharama za ujenzi. Na kwa kweli nimekuwa sichezi mbali sana na gharama halisi kwa kujenga mdogomdogo (yaani kwa kusimamia mwenyewe na mafundi wa mitaani maeneo ya Mwanza na Dar es Salaam.).

Muhimu ninajitahidi kupata ramani kamili ya nyumba ili kupata:

  1. Urefu wa kuta zote utakaosaidia kupata idadi kamili ya matofali
  2. Eneo la nyumba-sakafu (ground floor area) ili kupata gharama za sakafu, vigae, ceiling/gypsum board, idadi ya mabati nk.
  3. Eneo la kuta zote (wall area) ambalo linategemea unanyanyua kozi ngapi za matofali ili kupata idadi ya matofali, gharama za lipu, rangi nk.

Jedwali linasaidia kukokotoa idadi ya vifaa hivyo kirahisi baada ya kuweka vipimo hivyo vichache.

Kwa kutokana sasa na takwimu hizo kwa kutumia formular mbalimbali za civil engineering na uzoefu wa ujenzi, jedwali litakusaidia kupata makisio pia ya gharama kwa "automatic", yaani papo kwa papo. Fine tuning unaweza kuifanya, lakini tayari unakuwa na takwimu za kutosha hata ukimwita fundi muanze kujadiliana idadi ya vifaa vya ujenzi (matofali, ndoo za rangi, maboksi ya vigae, idadi ya mabati, gypsum board, nk) pia gharama za vifaa na gharama za ufundi kwa vile unakuwa una tatwimu zote muhimu na siyo kubishana tu na fundi.

Hili najua ni tatizo kubwa kwa watu wengi hasa wale wanaotaka kujenga nyumba kwa mara ya kwanza. Matokeo yake ni kutishika na kuacha kujenga au kupata mjanja akakuzidi akili na kuishia kununua vifaa vingi usivyohitaji na kama haupo site anaviuza! Aidha matokeo ya mkokotoo wa gharama hizi unaweza kukusaidia kupanga vizuri awamu za ujenzi kwa kulingana na uwezo wako ili ujenge nyumba yako bila taabu.

Nashukuru programu ya BURE ya Sweethome huwa hainiangushi, kwa muda wa nusu saa tu naweza kuchora ramani ya nyumba kubwa inayojitosheleza. Lakini hii ni kwa vile nimefundisha technical drawing na nimejifunza na kuitumia AutoCAD miaka ya nyuma. Hata hivyo ni programu rahisi kwa mtu yeyote kujifunza mwenyewe kama ana uelewa wa ufundi kidogo. Upungufu wake ni kutoweka paa kirahisi. Hivyo huwa nakomea kwenye kuta tu na kukweka furniture halisi kirahisi kabisa nipendavyo ili kupata feeling ya nyumba itakavyokuwa. Sweet Home 3D - Draw floor plans and arrange furniture freely

Kama una mchoro wa nyumba yako tayari, ingiza urefu wa kuta zote (ndani na nje) kwa utaratibu mzuri bila kukosea. Ni kujumlisha na kutoa tu. Kwa kurahisisha unaweza kujikumbusha hesabu za mzingo pia. Kisha kokotoa eneo la sakafu. Halafu mambo mengine ya kufanya ni kuingiza bei za ufundi/vifaa mbalimbali kulingana na eneo lako kama unaona zangu si sahihi. Jaribu kubadili takwimu kwenye maeneo MEUPE tu. Ama sivyo kama hujui kutumia Excel utaivuruga!

Nakiri kwamba haya makisio bado si kamili, kwa mfano sijaweka zege la msingi na makisio mengine yanaweza kuendelea kuboreshwa. Lakini kwa sasa nimeona nitoe mchango huu bure kwa jamii - eeh jamiiforums.

Upande wa msingi bado haujakaa vizuri na kwa kweli unategemea sura ya eneo na tabia ya ardhi unapotaka kujenga nyumba yako. Kazi hii hakikisha inafanywa kitaalamu. Kwa hiyo kwa upande wa msingi unaweza kuweka kozi 0 za msingi na hivyo kuondoa kabisa makisio ya msingi. Lakini kama unajenga msingi wa tofali tu, makisio ya matofali yanayohitajika utayapata.

Hapa nimeambatanisha:

  1. Ramani ya nyumba ikiwa na vipimo (ramani ambayo ilitolewa hapa na Zumbemkuu. Nimetumia ramani hii kugandamizia ili kuchora ramani hii(programu ya Sweet Home 3D inaruhusu jambo hili).
  2. Jedwali la MS Excel. NB: Jedwali la MS Excel ninalotoa hapa lina formular nyingi na nyingine nitazidi kuziongeza jinsi muda wangu unavyoruhusu, kwa hiyo pitia hapa kupata jedwali jipya au lililoboreshwa baada ya muda fulani.

****Nimeboresha tena awamu ya nne (Version 4)****:
- Ramani: Test house plan Vers3 - 12-2014-combined.pdf
- Jedwali_la_kukadiria_gharama_za_ujenzi_Test-House-Vers4.xlsx
Hii post imekuwa mkombozi kwangu, yaani imerahisisha maisha hususani design ya nyumba za kitanzania.Asante sana mwanabodi
 
Shukuru MUNGU wewe unaweza, sidhani kama alipenda awe too shallow like that.

Mijitu mingine hata kujielezea unashindwa.. Hebu kuwa na akili na uelezeee vizuri.. Utasaidiwaje iwapp hujiewi wewe mwenyewe... Mfyuuuuuuuu
 
Wana JF, natumai mko vizuri.

Naomba mwenye uzoefu na ujenzi anisaidie. Nitahitaji matofali mangapi ya sementi (BLOCK) ili kujenga nyumba hii hadi boma kuisha. Naomba kuwasilisha, KARIBU.
Tafuta fundi hapo mtaani fanya nao mahojiano kwa mafundi Wawili au Watatu tofauti waambie nataka makadirio ya ujenzi wa nyumba vyumba vitatu wape na sifa zingine. Mafundi ndiyo wanajua zaidi field kukoje hata kama utaenda kwa QS au ARCHTECTURE mwisho wa siku lazima atatafutwa fundi tuu (Tena kuna local fundi wametoa vitu vikali huwezi amini). Hakikisha unapata Mafundi waaminifu (unapopita hata Mtaani utaona wanajenga_chukua contact mfanye mambo). Humu watu watakupa ushauri kama ule wa kulima Matikiti kwa ekali unatoka na matikiti 2000 kila tikiki utauza kati ya 6000-8000 hahahaha!
 
Wana JF, natumai mko vizuri.

Naomba mwenye uzoefu na ujenzi anisaidie. Nitahitaji matofali mangapi ya sementi (BLOCK) ili kujenga nyumba hii hadi boma kuisha. Naomba kuwasilisha, KARIBU.
Nyumba ni ramani yenye vipimo sasa hesabu zitafanyikaje kama hakuna ramani
 
Back
Top Bottom