Kada wa CCM, Mchange Habib Mchange, amesema kuwa chama cha CHADEMA kinapaswa kuchunguzwa na vyombo vya ulinzi kuhusu tuhuma za kuhusika kwenye vurugu za Oktoba 29. Kuhusu madai ya watu kunyimwa miili ya ndugu zao waliofariki katika matukio hayo, amesema hakuna mtu aliyenyimwa mwili. Aidha, akizungumzia madai ya kaburi la halaiki katika maeneo ya Kondo, amesema hakuna ushahidi wa jambo hilo kwa kuwa alifika mwenyewe katika eneo hilo.
Ikumbukwe mnamo March 14, 2025, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Wilaya ya Kigamboni, ilimhoji mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Habibu Mchange, kufuatia tuhuma za kutaka kutoa rushwa kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wa Kata ya Tungi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chanzo cha habari, Mchange alikuwa miongoni mwa wanaotaka kutia nia ya kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kigamboni katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.