Mchango wa CHADEMA: Mawaziri Prof Kitila, Silinde, Dr Mollel, Waitara, Katambi na Gekul yule Shonza amefeli!

Mchango wa CHADEMA: Mawaziri Prof Kitila, Silinde, Dr Mollel, Waitara, Katambi na Gekul yule Shonza amefeli!

Anyway PASCHAL MAYALLA bado ana nafasi ya kuteuliwa nafasi ya Uenezi pale chamani[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Mwita Waitara na Godwin Mollel walihama CCM kwenda ChADEMA kisha wakarejea kwao hawezi kuwa zao la CHADEMA
 
Kiukweli Chadema wana mchango wa kutosha katika serikali yetu na hasa katika level ya uwaziri.

Mawaziri wafuatao wamewahi kutumika pale Ufipa katika level tofauti za uongozi kwa nyakati tofauti tofauti.

1. Prof Kitila Mkumbo

2. Mh Pauline Gekui

3. Mh Patrobas Katambi

4. Dr Godwin Mollel

5. Mh Mwita Waitara

6 Mh David Silinde

Ni vema vijana wa CCM mnapoibeza Chadema msisahau huu mchango wao mkubwa kwenye utumishi wa Umma.

Nasisitiza; Maendeleo hayana vyama!
Naona vipenyo watupu
 
Katika baraza la mawaziri lililotangazwa leo , wahamiaji kutoka upinzani wameula huku wafia chama kindakindaki Wakiendelea Kusugua benchi . Waliokuwa wapinzani na wamepata uteuzi ni Mwita Waitara , Pauline Gekul , David Silinde , Protobas Katambi huku wafia chama kina Pascal Njaa , Johnthebabtist , Etwege ,Mama D , Kawe Alumni licha ya kukesha mtandaoni lakini wanaendelea kusugua benchi sijui mpaka lini?
Hao huwa wanapata posho ya buku Saba,polepole akiamka vizuri anawapa hata teni!
 
Real is Real.

Dr. Chamuriho na Dr. Gwajima utendaji wao umewabeba. Leo hii wamebeba uwaziri kirahisi tuu.

Nyie mnapambana kutumia nguvu kumpamba mkuu ili mpate uteuzi kama akina Kigwa pambaneni na hali zenu.
Analia huko Twitter kama alizaliwa na waziri. Kuroga ni janga kubwa. Muulizieni Mshana😂😂😂😀
 
Mwita Waitara na Godwin Mollel walihama CCM kwenda ChADEMA kisha wakarejea kwao hawezi kuwa zao la CHADEMA
Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, Waitara alikuwa Chadema tangu akiwa UDSM kabla ya kuhamia CCM kipindi cha JK na baadae akarudi Chadema kisha CCM tena, hivyo akiitwa 'zao' la Chadema nadhani bado ni sahihi.
 
Katika baraza la mawaziri lililotangazwa leo , wahamiaji kutoka upinzani wameula huku wafia chama kindakindaki Wakiendelea Kusugua benchi . Waliokuwa wapinzani na wamepata uteuzi ni Mwita Waitara , Pauline Gekul , David Silinde , Protobas Katambi huku wafia chama kina Pascal Njaa , Johnthebabtist , Etwege ,Mama D , Kawe Alumni licha ya kukesha mtandaoni lakini wanaendelea kusugua benchi sijui mpaka lini?
Mkuu, hivi walipokuwa wanatangaza majina ya walioteuliwa walikuwa wanatangaza na ID zao za hapa JF 🤔
 
Chadema nayo iliwachukua hao watu kutoka NCCR Mageuzi mfano Tundu Lissu
 
Back
Top Bottom