Mchango wa CHADEMA: Mawaziri Prof Kitila, Silinde, Dr Mollel, Waitara, Katambi na Gekul yule Shonza amefeli!

Mchango wa CHADEMA: Mawaziri Prof Kitila, Silinde, Dr Mollel, Waitara, Katambi na Gekul yule Shonza amefeli!

Sisi tumeridhika kuwa wapiga debe au siyo bwasheh acha tuendele kuwa wapiga debe tu😂

Ova
Hahahaaaa....... Mgawanyo wa shughuli bwashee.

Wote hatuwezi kuwa mawaziri ndio maana tunatest mitambo mipya akina Gekui, Katambi na Silinde!
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, Waitara alikuwa Chadema tangu akiwa UDSM kabla ya kuhamia CCM kipindi cha JK na baadae akarudi Chadema kisha CCM tena, hivyo akiitwa 'zao' la Chadema nadhani bado ni sahihi.
Waitara alikuwa mpishi wa Nchimbi pale UVCCM!
 
Pamoja na kupewa uwaziri lakini hakika silinde hana amani kwa moyo wake hata kidogo
 
Cdm Ni chama chenye watu makini Sana. Mh rais kadhibitisha Hilo kwa hizi teuzi. Hongera mbowe, hongera cdm.
 
Kiukweli Chadema wana mchango wa kutosha katika serikali yetu na hasa katika level ya uwaziri.

Mawaziri wafuatao wamewahi kutumika pale Ufipa katika level tofauti za uongozi kwa nyakati tofauti tofauti.

1. Prof Kitila Mkumbo

2. Mh Pauline Gekui

3. Mh Patrobas Katambi

4. Dr Godwin Mollel

5. Mh Mwita Waitara

6 Mh David Silinde

Ni vema vijana wa CCM mnapoibeza Chadema msisahau huu mchango wao mkubwa kwenye utumishi wa Umma.

Nasisitiza; Maendeleo hayana vyama!
Bado wengine siku zijazo kina mdee matiko maana mnashindwa watumia vizuri muuende serikali yenu
 
Pascal mayala anaendelea kukomaa akitumia kale kamsemo kanakosema "MTAFUTAJI HACHOKI" 😆😆😆😆😆😆
 
Katika baraza la mawaziri lililotangazwa leo , wahamiaji kutoka upinzani wameula huku wafia chama kindakindaki Wakiendelea Kusugua benchi . Waliokuwa wapinzani na wamepata uteuzi ni Mwita Waitara , Pauline Gekul , David Silinde , Protobas Katambi huku wafia chama kina Pascal Njaa , Johnthebabtist , Etwege ,Mama D , Kawe Alumni licha ya kukesha mtandaoni lakini wanaendelea kusugua benchi sijui mpaka lini?
Watasugua bench hadi makalio yaote sugu kudadadeq
 
Pongezi kwa wote walioteuliwa. Nafikiri ile dhana ya kuwatia moyo wanaofanya jambo la kishujaa imetumika.

Hakika ukimaliza kazi kinachobaki ni kuvishwa taji.
 
Back
Top Bottom