Escrowseal1
JF-Expert Member
- Dec 17, 2014
- 4,618
- 4,605
Preamble : jamaa mmoja ughaibuni alikamatwa na polisi akisingiziwa na mkewe kuwa kampiga. Pamoja na kusingiziwa polisi na mwendesha mashtaka walihakikisha anapelekwa mahakamani japo hakuna ushahidi. Wakati aki deal na polisi kuhusu kesi walimwambia kuwa hata kama hakuna ushahidi ni lazima apelekwe mahakamani kwa kuwa kuna Domestic violence ndani yake. In real sense kesi zisizo na ushahidi huwa zinaishia njiani kwa no evidence .
Ester Matiko.
Akiwa Bungeni anajikita kuonyesha madhira wanayoyopitia wananchi wake wanaoishi karibu na hifadhi.
a) Yanatokea mauaji ya binadamu
b) Wapo waliopata vilema
C) Inataifishwa mifugo
d) Mifugo inapigwa risasi
e) Wanawake wanabakwa
Kwa kutoa ushahidi anataja tarehe 11/3 . Anakitaja kitongoji cha Germany kijiji cha machochwe ambako askari 5 walikiingilia na kumpiga risasi kijana Julius Nyaisuka Muhono. Umri miaka 21. Esta anataja muda kuwa ilikuwa saa 3:30.
Kwa mara nyingine Esta anaendelea kwa kumtaja Julius Mwita Mmari alikamatwa akichunga hifadhini na mama yake maseke alifika kambini akaamriwa kutoa fedha ili apewe kijana wake na baadae hakupewa kijana wake hadi leo hakaonekana.
Serikali.
Dakika ya tano kwenye clip niliyoiona naibu waziri anasimama na kutoa ufafanuzi kuwa sample ya damu iliyochukuliwa kwenye eneo la tukio baada ya kupelekwa kwa mwanasheria haikuthibitika kuwa ni ya binadamu na kujigamba kuwa awamu hii suala la maisha ya binadamu hawalichukulii ki mzaha mzaha.
Naibu spika.
Kama dakika ya saba hivi baada ya naibu waziri naibu spika anatoa tamko kwa Esta kuwa anapoleta taarifa kama hizi hasa kwa uzoefu wake awe makini kwa kuwa na uthibitisho ili kuepuka yeye ama wananchi wake kuingia kwenye matatizo anajigamba kuwa amefanya makusudi kuipa nafasi serikali ya kumjibu Esta.
Esta Matiko.
Ni baada ya majibu ya serikali na nyongeza ya naibu spika dada anaeonyesha kujiamini na kuwa na uhakika na anachokisema anaripuka bungeni kuongeza data za matukio. Its very very touching . Esta kwa uchungu mkubwa anatoa data nyingine.
a)20/12/2022 maaskari waliwakamata kuwatocha vijana 2 na kuwapeleka kwenye mto wenye mamba. Inasemekana kuna mabaki mengi ya nguo za binadamu wanaouawa na hawa watu wa higadhi. Vijana hao Waliokolewa na watoto ( i dont know how )Kijana yuko tayari kuongea na mamlaka. Taarifa iko kwa katibu mkuu , waziri wake no action todate baada ya miezi 3.
b. Eneo la Tuhanche na Goronga wameuawa watu 11
C) Nyanungu watu 6 wameuawa but yet no
action from authority.
Esta anaendelea kwa uchungu mkubwa sana ku demand hata kama wamewauwa kama majambazi they still need their bodies wazikwe kwa heshima ya kabila lao la wakurya.
Esta kwa uchungu usio na kifani na kwa hisia kali anamalizia kwa kusema .
Mimi ni mwanamke mkiniulia mwanangu na nikilia kila siku ,Mama anaweza akafanya Royal tour na mambo mengi kuukuza italii lakini laana ya machozi yangu kama mama haitaweza kuwa bure.
Mara chief whip anasimama na kuomba mwongozo in very rational way baada ya kuona Esta hatishwi na bla bla za kumfanya anyamaze ama aogope na naibu spika anasikika akiungana na chief whip japo naweza kusema ni unafiki wa kiwango cha standard gauge railway .
My take . Katika preamble nimeonyesha jinsi serikali huko duniani zinazojitambua zinavyoweka red lines kwenye mambo ya msingi hata kama hakuna ushahidi kwa kesi ya kusingiziwa kupigwa mwendesha mashtaka na polisi watakung’ang’ania kama kupe why? Kesi ina harufu ya domestic violence . Kama nchi ni mambo gani kati ya mfano mauaji , rushwa , ubakaji matumizi mabovu ya ofisi tunayoweza kusema naam as a nation hakuna wa ku cross line .
Naibu spika yupo kwenye kiti kwa niaba ya wananchi lakini ukimwamngalia hakuna doubt kuwa amejishonea joho la uchawa wa serikali hana habari kwa nini yupo pale .
Kwa machungu na tone ya Esta mbele ya kiongozi anaewakilisha wananchi there is no way on earth kama anajitambua anaweza ku side upande wa serikali na kujaribu ku discourage mwakilishi wa wananchi wake.
Esta ametaja majina ya waathirika , tarehe ya matukio , vijiji na vitongoji, saa ya baadhi ya matukio , kijana alie tayari kutoa ushahidi kwa vyombo vya habari , viongozi waliofika eneo la tukio akiwemo mkuu wa wilaya . Ametaja jina la mama wa kijana aliepotezwa pamoja na majina ya vijana wadogo waliouwawa . Yet mwakishi mkuu wa wananchi anamtishia kuingia kwenye matatizo baada tu ya naibu waziri kusema ETI mwanasheria mkuu alisema hakuna ushahidi wa moja kwa moja kama damu iliyokutwa eneo la tukio ni ya binadamu . Mwanasheria kutoa hiyo statement kunaondoaje malalamiko ya watu wanaoshuhudia ndugu zao wakiuawa kila kukicha ?
Ni maabara ya kichochoro gani inayoshindwa kuthibitisha DNA za binadamu wakati inao uwezo wa kuthibitisha DNA ya faru John . Kama si ya binadamu ninya mnyama gani huyo? Nchi hii nzuri tumetupiwa jini gani ?
All those solid evidence huyu naibu waziri na naibu spika walitaka Esta awe mkemia mkuu ndo waamini anachokisema pmoja na ushahidi wote alioutaja na majina?
Okey. Naibu waziri kasema damu haikuwa na ushahidi kuwa ilikuwa ya binadamu . Naibu spika kampa warning Esta kuwa na ushahidi na mambo anayoyaleta . Ghafla chief whip anatuliza mawimbi kuwa serikali imepata nyaraka na inafanyia kazi ghafla bin vuuu naibu spika anarukia ushauri wa chief whip kuwa serikali ifanyie kazi na ilete majibu wakati alipokuwa anamuonya Esta hakuona umuhimu wa kuiagiza serikali kufanya hivyo.
1.kwa mujibu wa chief whip Je serikali ilikuwa kazini kati ya muda aliowasilisha nyaraka kwa naibu spika na muda anaoongea chief whip ? Ni wakati gani huo chief whip alimaanisha kuwa serikali inaganyia kazi?
2.Kama si 1 hapo juu serkali iliendelea na kazi wakati damu haina ushahidi kuwa ni ya pimbi ama binadamu kwa mujibu wa naibu waziri?
3. Nani anatakiwa kuiagiza serikali spika wa bunge ama chief whip.
4. Okey are these names mentioned by Ester non existing humans ? Serikali si ina record ua watu wake ? Kama damu si ya binadamu na binadamu wamepotea katika mazingira hayo ni nini imefanya ama kutokuwa damu ya binadamu kunaondoa crime ua watu wake kupotea .?
Kuna mambo yanafanywa na viongozi wanaopaswa kutuongoza inadhihirisha kabisa kuwa tunaongozwa na mamlaka zinazotoka mahaka fulani ambako siko tunakokutaja kila siku mamlaka zinakotoka. Na si ajabu ndo kinachosababisha vicious cycle tunayoiona.
As a nation kuna mambo tunahitaji tuweke mguu chini na ku draw line . Hakuna shaka nchi inalia kila mahala tuachane uongozi wa kiujanja ujanja .
Kila mmoja anaweza kuzungusha usukani wa meli lakini inahitaji nahodha kuitoa meli kutoka kwenye bandari moja hadi nyingine by bishop Mpemba.
Mungu awabariki .
View: https://youtu.be/Gu05nRi5DLk?si=ctEtAppY30ZWW6Fp