SoC01 Mchango wa Jamii katika kuboresha Elimu Tanzania

SoC01 Mchango wa Jamii katika kuboresha Elimu Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Semu Msongole

Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
16
Reaction score
421
Katika taifa letu la Tanzania, watanzania tumejijengea utaratibu wa kushirikiana katika maswala mbalimbali ndani ya jamii zetu kama kuchangiana harusi, kutoa rambi rambi kwenye misiba na kujenga makanisa pamoja na misikiti. Haya yote yanafanyika na yanafanikiwa kutokana na nguvu ya umoja na mshikamano iliyopo katika jamii zetu.

Nguvu hii hii tunayoitumia huku kwenye maswala mengine ya kijamii tukiielekezea kwenye kuboresha elimu na kusomesha wanafunzi waliopo katika jamii zetu tutafika mbali kama taifa. Kuna changamoto nyingi sana katika sekta ya elimu baadhi zikiwa ni changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na chuo kikuu, vitabu vya kusomea mashuleni, usafiri wa wanafunzi na hulka ya kusoma au kwenda shule.

Changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na vyuo vikuu

Kwa kupitia dini zetu na kwa uhamasijaji wa viongozi wa dini zetu tunaweza tukashirikiana katika kusaidia wale wanafunzi ambao tunasali nao katika makanisa na misikiti yetu, wanafunzi hawa wanaweza kuwa wadogo zetu, majirani zetu, wanakwaya wetu, vijana wetu makanisani na wanajumuiya wenzetu. Kama tunaweza kuchangishana katika ujenzi wa makanisa, kurekodi video na audio za kwaya zetu, sherehe mbalimbali za kidini basi hili nalo pia linawezekana.

Kama kila kanisa na msikiti wakiamua kusomesha wale wanafunzi ambao ni waumini wao tu naamini kuwa hakutakuwa tena na wanafunzi watakaoshindwa kwenda kusoma kwa kukosa ada. Kihesabu zaidi ni kwamba kanisa moja likiwa na wanafunzi watano wanaotarajia kwenda sekondari (A level) ambako ada ni 70,000/= Tsh ukijumlisha na michango ya shule inafika 120,000/= Tsh kwa mwanafunzi mmoja wakiwa watano jumla inakuwa 600,000/= Tsh kwa miaka yote miwili inakuwa ni 1,200,000/= Tsh kwa kushirikiana hivi na kufanikisha jambo hili kanisa linakuwa limeokoa maisha ya vijana hawa na kuwapa nafasi ya kufanikiwa kielimu.

Changamoto ya vitabu vya kusoma mashuleni

Katika swala la vitabu vya kusomea mashuleni wazazi na jamii kwa ujumla tumekuwa tukiilaumu serikali kwa kutonunua na kupeleka vitabu vya masomo mashuleni tunasahau kuwa hata sisi binafsi kama jamii tunao uwezo wa kufanikisha hili swala kwa urahisi sana. Katika shule zetu huwa kuna wanafunzi wanaotoka katika familia zenye hali tofauti ya kiuchumi, kama mzazi unauwezo wa kumnunulia mtoto wako simu ya laki 3 basi unaouwezo wa kununua vitabu 20 vya 15,000/=Tsh.

Sawa unaweza usipongezwe wala kushukuriwa kama utakavyotarajia lakini fahamu kuwa kuna maisha ya mwanafunzi mmoja au wawili hapo shuleni utakuwa umeyaokoa cha muhimu ni kuzingatia umuhimu wa msaada utakao toa katika shule anayosoma mwanao au hata mtoto wa jirani yako, wakifanya hivi wazazi watano kutakuwa na vitabu 100 ikiendelea kwa miaka miwili au mitatu hiyo shule haitakuwa tena na shida ya vitabu na kama jamii mnakuwa mmechangia kuleta maendeleo ya kielimu.

Changamoto ya usafiri kwa wanafunzi

Tumekuwa tukishuhudia kila siku namna ambavyo wanafunzi huwa wanateseka katika swala la usafiri wa kwenda shule na kurudi nyumbani. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kama tukishirikiana kwa pamoja wazazi na walezi wa hawa wanafunzi au watoto wetu wanaopata shida hii ya usafiri. Kama wazazi wakikubaliana na madereva hata watano tu wa daladala ambao watakuwa wanawabeba wanafunzi hao kwenda shule na kurudi nyumbani bila kuharibu safari zao za kawaida yaani kama ni gari ya gongo la mboto ibebe wanafunzi wanaoelekea huko huko.

Pia njia nyingine ni ya wazazi kuongea na uongozi wa miji waweke utaratibu kuwa kila daladala litumie safari yake moja ya siku kubeba wanafunzi yaani ikipakia wanafunzi tupu asubuhi basi ikifika jioni muda wanatoka shule hatawajibika yeye kuwabeba tena hao wanafunzi watabebwa na daladala nyingine ambayo haikuwapakia asubuhi, kwa taratibu kama hizi tutakuwa tumeboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi.

Changamoto ya hulka ya kusoma au kwenda shule

Wanafunzi wengi siku hizi hawapendi kusoma na hawapendi zaidi kwenda shule hii inaweza kuwa inasababishwa na ukali wa walimu mashuleni lakini pia husababishwa na ukosefu wa dira ya kielimu kwa wanafunzi. Hapa Tanzania mwanafunzi anasoma darasa la kwanza hadi kidato cha nne na msomi pekee anayemfahamu ni mwalimu wake tu basi hali hii hupelekea wanafunzi wengi kuichukia elimu na kuona hakuna maana ya kusoma. Kama jamii tunaweza kutatua changamoto hii na kubadilisha fikra za wanafunzi kwa kuwa mabalozi wa taaluma zetu kutembelea shule na kuongea na wanafunzi wajue kuwa taaluma zipo nyingi na zinahitaji ufaulu wa masomo gani ili uweze kusomea.

Kama wewe ni daktari, mwanasheria, manager, mwandishi wa habari, engineer ukipata muda tembelea shule yeyote iwe ya serikali au ya binafsi uongee na kupiga stori na wanafunzi waruhusu wakuulize maswali mbalimbali kuhusu taaluma yako, waeleze changamoto ulizopitia katika safari yako ya kielimu wajulishe faida ya kuwa na taaluma kama yako. Wanafunzi wengi siku hizi wamekuwa wakitamani kuwa wasanii wa mziki au waigizaji (sio kwamba ni kitu kibaya) hii ni kwasababu hao ndo watu wanaoona wana mafanikio katika jamii lakini mwanafunzi huyo huyo akijua kuwa ukiwa manager wa Vodacom, CRDB bank au kampuni kubwa kubwa familia yako inakuwa na bima ya kutibiwa hadi nje za nchi, unapewa gari la kazi, unalipiwa nyumba unayokaa ukitaka unasomeshwa na kampuni na vingine vingi tu watoto wetu wakijua haya hawatakuwa tena na wasiwasi na maisha yao ya kielimu watasoma tena kwa bidii mpaka na wao wayafikie mafanikio ya kiwango hicho.

Kwa kumalizia naomba kusema kuwa tukishirikiana kama jamii tunaweza kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya elimu Tanzania, sio lazima tusubirie serikali itufanyie kila kitu mtu binafsi kwa kwenda tu shule na kupiga stori na wanafunzi kuhusu kazi yako inatosha kuleta mabadiliko makubwa sana ya kifikra kwa wanafunzi na kuwafanya waongeze bidii katika masomo yao. Pamoja Tunaweza!​
 
Upvote 422
Ina maana akili zangu zimeisha kabisa, hebu shoot hapo pa kupiga kura unitumie, poor me
 
Katika taifa letu la Tanzania, watanzania tumejijengea utaratibu wa kushirikiana katika maswala mbalimbali ndani ya jamii zetu kama kuchangiana harusi, kutoa rambi rambi kwenye misiba na kujenga makanisa pamoja na misikiti. Haya yote yanafanyika na yanafanikiwa kutokana na nguvu ya umoja na mshikamano iliyopo katika jamii zetu.

Nguvu hii hii tunayoitumia huku kwenye maswala mengine ya kijamii tukiielekezea kwenye kuboresha elimu na kusomesha wanafunzi waliopo katika jamii zetu tutafika mbali kama taifa. Kuna changamoto nyingi sana katika sekta ya elimu baadhi zikiwa ni changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na chuo kikuu, vitabu vya kusomea mashuleni, usafiri wa wanafunzi na hulka ya kusoma au kwenda shule.

Changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na vyuo vikuu
Kwa kupitia dini zetu na kwa uhamasijaji wa viongozi wa dini zetu tunaweza tukashirikiana katika kusaidia wale wanafunzi ambao tunasali nao katika makanisa na misikiti yetu, wanafunzi hawa wanaweza kuwa wadogo zetu, majirani zetu, wanakwaya wetu, vijana wetu makanisani na wanajumuiya wenzetu. Kama tunaweza kuchangishana katika ujenzi wa makanisa, kurekodi video na audio za kwaya zetu, sherehe mbalimbali za kidini basi hili nalo pia linawezekana. Kama kila kanisa na msikiti wakiamua kusomesha wale wanafunzi ambao ni waumini wao tu naamini kuwa hakutakuwa tena na wanafunzi watakaoshindwa kwenda kusoma kwa kukosa ada. Kihesabu zaidi ni kwamba kanisa moja likiwa na wanafunzi watano wanaotarajia kwenda sekondari (A level) ambako ada ni 70,000/= Tsh ukijumlisha na michango ya shule inafika 120,000/= Tsh kwa mwanafunzi mmoja wakiwa watano jumla inakuwa 600,000/= Tsh kwa miaka yote miwili inakuwa ni 1,200,000/= Tsh kwa kushirikiana hivi na kufanikisha jambo hili kanisa linakuwa limeokoa maisha ya vijana hawa na kuwapa nafasi ya kufanikiwa kielimu.

Changamoto ya vitabu vya kusoma mashuleni
Katika swala la vitabu vya kusomea mashuleni wazazi na jamii kwa ujumla tumekuwa tukiilaumu serikali kwa kutonunua na kupeleka vitabu vya masomo mashuleni tunasahau kuwa hata sisi binafsi kama jamii tunao uwezo wa kufanikisha hili swala kwa urahisi sana. Katika shule zetu huwa kuna wanafunzi wanaotoka katika familia zenye hali tofauti ya kiuchumi, kama mzazi unauwezo wa kumnunulia mtoto wako simu ya laki 3 basi unaouwezo wa kununua vitabu 20 vya 15,000/=Tsh. Sawa unaweza usipongezwe wala kushukuriwa kama utakavyotarajia lakini fahamu kuwa kuna maisha ya mwanafunzi mmoja au wawili hapo shuleni utakuwa umeyaokoa cha muhimu ni kuzingatia umuhimu wa msaada utakao toa katika shule anayosoma mwanao au hata mtoto wa jirani yako, wakifanya hivi wazazi watano kutakuwa na vitabu 100 ikiendelea kwa miaka miwili au mitatu hiyo shule haitakuwa tena na shida ya vitabu na kama jamii mnakuwa mmechangia kuleta maendeleo ya kielimu.

Changamoto ya usafiri kwa wanafunzi
Tumekuwa tukishuhudia kila siku namna ambavyo wanafunzi huwa wanateseka katika swala la usafiri wa kwenda shule na kurudi nyumbani. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kama tukishirikiana kwa pamoja wazazi na walezi wa hawa wanafunzi au watoto wetu wanaopata shida hii ya usafiri. Kama wazazi wakikubaliana na madereva hata watano tu wa daladala ambao watakuwa wanawabeba wanafunzi hao kwenda shule na kurudi nyumbani bila kuharibu safari zao za kawaida yaani kama ni gari ya gongo la mboto ibebe wanafunzi wanaoelekea huko huko. Pia njia nyingine ni ya wazazi kuongea na uongozi wa miji waweke utaratibu kuwa kila daladala litumie safari yake moja ya siku kubeba wanafunzi yaani ikipakia wanafunzi tupu asubuhi basi ikifika jioni muda wanatoka shule hatawajibika yeye kuwabeba tena hao wanafunzi watabebwa na daladala nyingine ambayo haikuwapakia asubuhi, kwa taratibu kama hizi tutakuwa tumeboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi.

Changamoto ya hulka ya kusoma au kwenda shule
Wanafunzi wengi siku hizi hawapendi kusoma na hawapendi zaidi kwenda shule hii inaweza kuwa inasababishwa na ukali wa walimu mashuleni lakini pia husababishwa na ukosefu wa dira ya kielimu kwa wanafunzi. Hapa Tanzania mwanafunzi anasoma darasa la kwanza hadi kidato cha nne na msomi pekee anayemfahamu ni mwalimu wake tu basi hali hii hupelekea wanafunzi wengi kuichukia elimu na kuona hakuna maana ya kusoma. Kama jamii tunaweza kutatua changamoto hii na kubadilisha fikra za wanafunzi kwa kuwa mabalozi wa taaluma zetu kutembelea shule na kuongea na wanafunzi wajue kuwa taaluma zipo nyingi na zinahitaji ufaulu wa masomo gani ili uweze kusomea. Kama wewe ni daktari, mwanasheria, manager, mwandishi wa habari, engineer ukipata muda tembelea shule yeyote iwe ya serikali au ya binafsi uongee na kupiga stori na wanafunzi waruhusu wakuulize maswali mbalimbali kuhusu taaluma yako, waeleze changamoto ulizopitia katika safari yako ya kielimu wajulishe faida ya kuwa na taaluma kama yako. Wanafunzi wengi siku hizi wamekuwa wakitamani kuwa wasanii wa mziki au waigizaji (sio kwamba ni kitu kibaya) hii ni kwasababu hao ndo watu wanaoona wana mafanikio katika jamii lakini mwanafunzi huyo huyo akijua kuwa ukiwa manager wa Vodacom, CRDB bank au kampuni kubwa kubwa familia yako inakuwa na bima ya kutibiwa hadi nje za nchi, unapewa gari la kazi, unalipiwa nyumba unayokaa ukitaka unasomeshwa na kampuni na vingine vingi tu watoto wetu wakijua haya hawatakuwa tena na wasiwasi na maisha yao ya kielimu watasoma tena kwa bidii mpaka na wao wayafikie mafanikio ya kiwango hicho.

Kwa kumalizia naomba kusema kuwa tukishirikiana kama jamii tunaweza kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya elimu Tanzania, sio lazima tusubirie serikali itufanyie kila kitu mtu binafsi kwa kwenda tu shule na kupiga stori na wanafunzi kuhusu kazi yako inatosha kuleta mabadiliko makubwa sana ya kifikra kwa wanafunzi na kuwafanya waongeze bidii katika masomo yao. Pamoja Tunaweza!​
All the best mkuu
 
Upo sahihi lakini ayo yote yanashindikana kutokana na ubinafsi wetu na mitazamo yetu tuliojiwekea juu ya swala la elimu
 
Waliosoma wanateseka mitaani kutafuta ajira na kazi morali yakuchangishana ili wakasome wengine itatoka wapi sasa Mkuu?.

Kadiri siku zinavyozidi kwenda elimu ya shule inaonekana ni upotevu wa pesa na muda, kuna athari kubwa sana kijamii wasomi kukosa kazi na ajira.

Hapa watakuja watu watasema wasomi wajiajiri, ila ukweli ni kuwa sio kila msomi anao uwezo wa kujiajiri, kujiajiri ni zaidi ya hapo, ni biashara na si kila msomi ana umahiri wa kufanya biashara.

Wasomi waajiriwe maana kuajiriwa sio dhambi. Ikiwezekana serikali ishushe umri wa kustaafu kwa baadhi ya kada ili kuruhusu kizazi kipya na ubunifu mpya kwenye hizo kada, au la fao la kujitoa liwepo, mtu aamue kujitoa utumishi wa umma muda wowote.

Sekta binafsi ipewe nguvu

Mwisho na kwa ulazima fedha za mikopo kwa vijana ya halmashauri zitolewe hata kwa kijana mmoja mmoja, isiwe lazima wawe kikundi

Alafu kusiwe na urasimu kuzipata hizo fedha. Wapo vijana mbali na kujiunga vikundi na kukidhi vigezo fedha hawajapata au wanazungushwa zungushwa.
 
Natumia simu sijaona hizo namba ningekupigia kura sorry
 
Chief naomba upokee mchango wangu kama itakupendeza.
1. Kuhusu vitabu.
Naunga mkono suala la taasisi za kidini kuchangia vitabu na vifaa mbalimbali vya kujifunzia. Sababu zangu ni:-
A. Kuwezesha watoto wa kaya zenye kipato cha chini kupata huduma sawa na wengine bila matabaka.
B. Kuongeza ushawishi wa watoto kutamani kujifunza kwa bidii kwa kuona nyuma yao kuna kundi kubwa na muhimu katika jamii likiwatakia mafanikio.
Aidha kuwe na muda wa kuwatambua(to acknowledge them) kama wafadhili wa Elimu.
2. Kuhusu Usafiri.
Kama magari binafsi yanaweza kukitolea kupeleka watu kwenye mikutano ya siasa na makongamano mbalimbali, sidhani kama itashindikana kusaidia kuandaa vijana kwa ajili ya taifa la kesho.
Taratibu zinaweza kuwekwa ili aidha:-
A. Kuchangia gharama za mafuta AU
B. Kuwafanyia service kwa viwango maalumu na gharama kulingana na standards zilizowekwa AU.
C. Kuwachangia sehem ya gharama za uendeshaji kulingana na km & idadi ya wanafunzi wanaosafirisha. Gharama hizi zinaweza kulipwa kwa mwezi au kila baada ya kipindi fulani.
Hapa hata tozo hazitalalamikiwa sana😂 ili mradi tu usimamizi uwe mzuri.
Note: Hii itasaidia kuboresha huduma ya usafirishaji wanafunzi ukiwemo usalama wa vyombo na abiria.
Tahadhali. Ikitumika vibaya inakuwa fursa kwa watendaji wa serikali wasio waaminifu.

3. Kuhusu Ada.
Naona changamoto katika hili kuchangisha ada kupitia makanisa na madhehebu mengine ya dini. Ingawa ni rahisi kupata wafadhili kutoka makanisani na misikitini.
Jamii zetu zimejengeka katika fikra za utegemezi. Hivyo kuchangisha pesa zinazotambulika kwenda kumnufaisha mtu anayefahamika an identified individua kutafanya baadhi ya wazazi kutotimiza wajibu wao kwa watoto kwa viwango stahiki huku wakielekeza matumaini yao kwa taasisi za kidini.

Hongera kwa andiko zuri.
 
Jamii yetu inahitaji fikra chanya kama hizi. Zinatufundisha kuwajibika kwa wenzetu hasa wenye uhitaji bila kubaguana kwa misingi yoyote.
Zinatufundisha kuiandaa kesho ya vijana wetu kabla hatujachelewa.
 
1. Kwenye KILA MITA 1 YA UMEME iongezwe tozo ya Tsh. 300 au zaidi kila mwezi kugharamia miundombinu ya Elimu., hasa ya Pri + Sec. Hali ni mbaya wandugu. The situation is so terrible. Kuna baadhi ya shule ufundishaji hufanywa kana kwamba watu wapo kwenye kongamano.
2. Yafanyike mageuzi makubwa kwenye Elimu yatakayowezesha Elimu ya Kujitegemea. Hii itatia morali wanafunzi kukaza kwenye Elimu.
 
Changamoto kubwa zaidi ya elimu ni kwa wanufaika wenyewe wa elimu ambao pamoja na kupata msoto wa kusotea elimu wanajikuta wanaingia kwenye msoto mwingine wa mtaani kwa kukosa ajira wakati walitegemea kuwa baada ya msoto wa elimu watalia kivulini.
 
Katika taifa letu la Tanzania, watanzania tumejijengea utaratibu wa kushirikiana katika maswala mbalimbali ndani ya jamii zetu kama kuchangiana harusi, kutoa rambi rambi kwenye misiba na kujenga makanisa pamoja na misikiti. Haya yote yanafanyika na yanafanikiwa kutokana na nguvu ya umoja na mshikamano iliyopo katika jamii zetu.

Nguvu hii hii tunayoitumia huku kwenye maswala mengine ya kijamii tukiielekezea kwenye kuboresha elimu na kusomesha wanafunzi waliopo katika jamii zetu tutafika mbali kama taifa. Kuna changamoto nyingi sana katika sekta ya elimu baadhi zikiwa ni changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na chuo kikuu, vitabu vya kusomea mashuleni, usafiri wa wanafunzi na hulka ya kusoma au kwenda shule.

Changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na vyuo vikuu

Kwa kupitia dini zetu na kwa uhamasijaji wa viongozi wa dini zetu tunaweza tukashirikiana katika kusaidia wale wanafunzi ambao tunasali nao katika makanisa na misikiti yetu, wanafunzi hawa wanaweza kuwa wadogo zetu, majirani zetu, wanakwaya wetu, vijana wetu makanisani na wanajumuiya wenzetu. Kama tunaweza kuchangishana katika ujenzi wa makanisa, kurekodi video na audio za kwaya zetu, sherehe mbalimbali za kidini basi hili nalo pia linawezekana.

Kama kila kanisa na msikiti wakiamua kusomesha wale wanafunzi ambao ni waumini wao tu naamini kuwa hakutakuwa tena na wanafunzi watakaoshindwa kwenda kusoma kwa kukosa ada. Kihesabu zaidi ni kwamba kanisa moja likiwa na wanafunzi watano wanaotarajia kwenda sekondari (A level) ambako ada ni 70,000/= Tsh ukijumlisha na michango ya shule inafika 120,000/= Tsh kwa mwanafunzi mmoja wakiwa watano jumla inakuwa 600,000/= Tsh kwa miaka yote miwili inakuwa ni 1,200,000/= Tsh kwa kushirikiana hivi na kufanikisha jambo hili kanisa linakuwa limeokoa maisha ya vijana hawa na kuwapa nafasi ya kufanikiwa kielimu.

Changamoto ya vitabu vya kusoma mashuleni

Katika swala la vitabu vya kusomea mashuleni wazazi na jamii kwa ujumla tumekuwa tukiilaumu serikali kwa kutonunua na kupeleka vitabu vya masomo mashuleni tunasahau kuwa hata sisi binafsi kama jamii tunao uwezo wa kufanikisha hili swala kwa urahisi sana. Katika shule zetu huwa kuna wanafunzi wanaotoka katika familia zenye hali tofauti ya kiuchumi, kama mzazi unauwezo wa kumnunulia mtoto wako simu ya laki 3 basi unaouwezo wa kununua vitabu 20 vya 15,000/=Tsh.

Sawa unaweza usipongezwe wala kushukuriwa kama utakavyotarajia lakini fahamu kuwa kuna maisha ya mwanafunzi mmoja au wawili hapo shuleni utakuwa umeyaokoa cha muhimu ni kuzingatia umuhimu wa msaada utakao toa katika shule anayosoma mwanao au hata mtoto wa jirani yako, wakifanya hivi wazazi watano kutakuwa na vitabu 100 ikiendelea kwa miaka miwili au mitatu hiyo shule haitakuwa tena na shida ya vitabu na kama jamii mnakuwa mmechangia kuleta maendeleo ya kielimu.

Changamoto ya usafiri kwa wanafunzi

Tumekuwa tukishuhudia kila siku namna ambavyo wanafunzi huwa wanateseka katika swala la usafiri wa kwenda shule na kurudi nyumbani. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kama tukishirikiana kwa pamoja wazazi na walezi wa hawa wanafunzi au watoto wetu wanaopata shida hii ya usafiri. Kama wazazi wakikubaliana na madereva hata watano tu wa daladala ambao watakuwa wanawabeba wanafunzi hao kwenda shule na kurudi nyumbani bila kuharibu safari zao za kawaida yaani kama ni gari ya gongo la mboto ibebe wanafunzi wanaoelekea huko huko.

Pia njia nyingine ni ya wazazi kuongea na uongozi wa miji waweke utaratibu kuwa kila daladala litumie safari yake moja ya siku kubeba wanafunzi yaani ikipakia wanafunzi tupu asubuhi basi ikifika jioni muda wanatoka shule hatawajibika yeye kuwabeba tena hao wanafunzi watabebwa na daladala nyingine ambayo haikuwapakia asubuhi, kwa taratibu kama hizi tutakuwa tumeboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi.

Changamoto ya hulka ya kusoma au kwenda shule

Wanafunzi wengi siku hizi hawapendi kusoma na hawapendi zaidi kwenda shule hii inaweza kuwa inasababishwa na ukali wa walimu mashuleni lakini pia husababishwa na ukosefu wa dira ya kielimu kwa wanafunzi. Hapa Tanzania mwanafunzi anasoma darasa la kwanza hadi kidato cha nne na msomi pekee anayemfahamu ni mwalimu wake tu basi hali hii hupelekea wanafunzi wengi kuichukia elimu na kuona hakuna maana ya kusoma. Kama jamii tunaweza kutatua changamoto hii na kubadilisha fikra za wanafunzi kwa kuwa mabalozi wa taaluma zetu kutembelea shule na kuongea na wanafunzi wajue kuwa taaluma zipo nyingi na zinahitaji ufaulu wa masomo gani ili uweze kusomea.

Kama wewe ni daktari, mwanasheria, manager, mwandishi wa habari, engineer ukipata muda tembelea shule yeyote iwe ya serikali au ya binafsi uongee na kupiga stori na wanafunzi waruhusu wakuulize maswali mbalimbali kuhusu taaluma yako, waeleze changamoto ulizopitia katika safari yako ya kielimu wajulishe faida ya kuwa na taaluma kama yako. Wanafunzi wengi siku hizi wamekuwa wakitamani kuwa wasanii wa mziki au waigizaji (sio kwamba ni kitu kibaya) hii ni kwasababu hao ndo watu wanaoona wana mafanikio katika jamii lakini mwanafunzi huyo huyo akijua kuwa ukiwa manager wa Vodacom, CRDB bank au kampuni kubwa kubwa familia yako inakuwa na bima ya kutibiwa hadi nje za nchi, unapewa gari la kazi, unalipiwa nyumba unayokaa ukitaka unasomeshwa na kampuni na vingine vingi tu watoto wetu wakijua haya hawatakuwa tena na wasiwasi na maisha yao ya kielimu watasoma tena kwa bidii mpaka na wao wayafikie mafanikio ya kiwango hicho.

Kwa kumalizia naomba kusema kuwa tukishirikiana kama jamii tunaweza kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya elimu Tanzania, sio lazima tusubirie serikali itufanyie kila kitu mtu binafsi kwa kwenda tu shule na kupiga stori na wanafunzi kuhusu kazi yako inatosha kuleta mabadiliko makubwa sana ya kifikra kwa wanafunzi na kuwafanya waongeze bidii katika masomo yao. Pamoja Tunaweza!​
Ok
 
Ndg Semu Msongole umetoa mchango mzuri wa mawazo hapa, hongera. Hii nayo ni aina ya sadaka kwa jamii na umetumia karama yako
Mungu aliyo kujalia vizuri kwa kutoa mawazo na wako members wengi hapa jF wamejitolea kufanya hivyo. Haijalishi mawazo yao yatachukuliwa na wanaotuongoza wakayafanyia kazi au yata puuzwa lakini ninacho amini Mungu atawalipa kwasababu waliwasha taa zao na hawakuziweka chini ya uvungu bali waliizweka juu ya meza au stuli ziangaze na mwanga wake uwe faida kwa wengine.

Nikirudi kwenye hii maada ya uboreshaji Elimu.
Kuhusu ada ni kweli taasisi za kidini zinaweza kuwa na mchango mzuri wakiamua na wakaweka utatatibu ulio wazi wa kufanya hii michango/sadaka ya elimu matokeo yake yawe yanaonekana kwa wadau. Kanisa Katoliki limefanikiwa kwa kiasi kikubwa na shule zao ni bora na zakupigiwa mfano. Nisichokuwa na hakika nacho sijui wamao utaratibu gani wa kuwagundua wenye uhitaji huu na kuwasaidia?

Makanisa mengine yanajitahidi na wana hizi sadaka za elimu lakini unakuta shule zao ubora hauko. Jinsi wanavyowapata wanafunzi wakuwasaidia hakuna uwazi sana sana wanafunzi wanao faidi ni watoto wa viongozi wa ngazi mbalimbali za dhehebu husika tu wala si watoto wa waumini wengine wa kawaida wenye huo uhitaji katika dhehebu hilo. Na mbaya zaidi kunakuwa na matumizi ya sadaka hizi yasiyo bariki. Kuweza kuliweka sawa hili ni kuzitumia sadaka hizi kwa kuacha zisimamiwe na uongozi wa kanisa zilipotolewa. Kamavzimetolewa na kaniza x la dhehebu y. Uongozi wa kanisa x ndio utambue nani walio na uhitaji huo kati ya waumini wenzao na kama hamna utoke uende uangalie nani walio na uhitaji huo nje. Ikiwemo jamii inayo wa zunguka au kaniza z la sehemu nyingine ma la hilo hil dhehebu y. Ila sadaka hizi zikiachiwa zizimamiwe na uongozi wa juu wa dhehebu y ni ngumu kuona matokeo yake na kuwaguza waumini mmoja mmoja kuona wao ni sehemu ya wito na utumishi huo.

Pia wako watu walio someshwa kwa michango ya wana vijiji wenzao na ndugu zao ni kiasi cha serekali kuwakumbusha inaowaongoza kwamba wakati mwengine wana wajibu huo. Na waliosomeshwa na ndugu zao wawe waungwana basi angalau ku appriciate.

Kuhusu usafiri kwa mijini kweli wanafunzi wanateseka sana. Serikali imekosa ubunifu. Kuwa na mradi maalumu wa mabasi ya wanafunzi ingekuwa ni suluhisho. Wakati wa saa za kwenda na kutoka shule yanabeba wanafunzi tu ambalo ndio jukumu lake muhimu. Wskati amvao ni nje ya hapo wanabeba abiria wa kawsida ili waweze kujiendesha na serikali isichukue kodi hata senti moja labda payee ya waajiriwa wa huu mradi.

Hili ka mradi wa mabasi kama ni gumu. Serikali ione ni jinsi gani itaweka utaratibu mzuri wa kuingia na wafanyabiashara baadhi na watakao penda wenye mabasi ya biashara za daladala. Na ni rahisi tu unakubaliana nao unawapa incentives flani flani watakazoridhika nazo na unawakea utaratibu wa kuwasimimia wa kubeba wanafunzi wakilipwa kwa malipo ya hizo incentives. Kwa mfano wasilipe kodi na tozo zinazoendana na biashara ya daladaka.

Kwa vijijini ni kuongeza shule zilizo karibu na wanapoushi watu wananafunzi wasitembee umbak mrefu kufuata shule.

Hili la wanafunzi kutoenda shule ni kutafuta vitu vitakavyo wafutia huko mashuleni vishinde vya huko mtaani. Lakini uwepo utaratibu wa kuwawajibisha wazazi na walezi kusimamia watoto wao ili kugakikisha wanafika mashuleni.
 
Serikali inatakiwa iangalie na walimu wa kuwaajiri, Kuna baadhi ya walimu shida ndiyo zimewapeleka na si wito wala kipawa Cha kufundisha Sana Sana shule za kata ndiyo Kuna uozo huu, siyo Siri serikali ilizipuuza shule za kata hatimae zikawa zinajikotroo
Hatimae walimu walijikatia tamaa wakazivuruga hizo shule

Me nimiongoni mwa waliosoma shule za kata kwa Madudu niliyoyaona hakika Elimu yetu itazidi kudidimia, pia wanafunzi inatakiwa wajitambue hasa pale wanapoona haki Elimu inayumba wasisite kupaza sauti.

Media zinabidi ziandae mijadala hasa ikiwalenga wanafunzi kuweza kueleza changamoto zilizopo na jinsi ya kuzitatua.

Ahasante
 
Asante sana Kwa maoni yako hata mimi ninakubaliana na wewe kuhusu hili swala la walimu kutofanya kazi kwa wito na matokeo yake kuzidi kuididimiza elimu nchini kikubwa hapa cha kuzingatia ni kubadilisha mtazamo wa jamii zetu. Kila mtu katika jamii yetu anatakiwa afuatilie kwa kina muenendo wa elimu inayotolewa mashuleni na vile vile kutoa msaada wa aina yeyote ile ili kuboresha huduma za masomo mashuleni.
Nakumbuka Enzi za mkapa watu tulikuwa tunapewa daftari Bure kuonyesha serikali ilikuwa serious na Elimu, hii leo hizo huduma ni
destroyed.
 
Back
Top Bottom