SoC01 Mchango wa Jamii katika kuboresha Elimu Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Semu Msongole

Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
16
Reaction score
421
Katika taifa letu la Tanzania, watanzania tumejijengea utaratibu wa kushirikiana katika maswala mbalimbali ndani ya jamii zetu kama kuchangiana harusi, kutoa rambi rambi kwenye misiba na kujenga makanisa pamoja na misikiti. Haya yote yanafanyika na yanafanikiwa kutokana na nguvu ya umoja na mshikamano iliyopo katika jamii zetu.

Nguvu hii hii tunayoitumia huku kwenye maswala mengine ya kijamii tukiielekezea kwenye kuboresha elimu na kusomesha wanafunzi waliopo katika jamii zetu tutafika mbali kama taifa. Kuna changamoto nyingi sana katika sekta ya elimu baadhi zikiwa ni changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na chuo kikuu, vitabu vya kusomea mashuleni, usafiri wa wanafunzi na hulka ya kusoma au kwenda shule.

Changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na vyuo vikuu

Kwa kupitia dini zetu na kwa uhamasijaji wa viongozi wa dini zetu tunaweza tukashirikiana katika kusaidia wale wanafunzi ambao tunasali nao katika makanisa na misikiti yetu, wanafunzi hawa wanaweza kuwa wadogo zetu, majirani zetu, wanakwaya wetu, vijana wetu makanisani na wanajumuiya wenzetu. Kama tunaweza kuchangishana katika ujenzi wa makanisa, kurekodi video na audio za kwaya zetu, sherehe mbalimbali za kidini basi hili nalo pia linawezekana.

Kama kila kanisa na msikiti wakiamua kusomesha wale wanafunzi ambao ni waumini wao tu naamini kuwa hakutakuwa tena na wanafunzi watakaoshindwa kwenda kusoma kwa kukosa ada. Kihesabu zaidi ni kwamba kanisa moja likiwa na wanafunzi watano wanaotarajia kwenda sekondari (A level) ambako ada ni 70,000/= Tsh ukijumlisha na michango ya shule inafika 120,000/= Tsh kwa mwanafunzi mmoja wakiwa watano jumla inakuwa 600,000/= Tsh kwa miaka yote miwili inakuwa ni 1,200,000/= Tsh kwa kushirikiana hivi na kufanikisha jambo hili kanisa linakuwa limeokoa maisha ya vijana hawa na kuwapa nafasi ya kufanikiwa kielimu.

Changamoto ya vitabu vya kusoma mashuleni

Katika swala la vitabu vya kusomea mashuleni wazazi na jamii kwa ujumla tumekuwa tukiilaumu serikali kwa kutonunua na kupeleka vitabu vya masomo mashuleni tunasahau kuwa hata sisi binafsi kama jamii tunao uwezo wa kufanikisha hili swala kwa urahisi sana. Katika shule zetu huwa kuna wanafunzi wanaotoka katika familia zenye hali tofauti ya kiuchumi, kama mzazi unauwezo wa kumnunulia mtoto wako simu ya laki 3 basi unaouwezo wa kununua vitabu 20 vya 15,000/=Tsh.

Sawa unaweza usipongezwe wala kushukuriwa kama utakavyotarajia lakini fahamu kuwa kuna maisha ya mwanafunzi mmoja au wawili hapo shuleni utakuwa umeyaokoa cha muhimu ni kuzingatia umuhimu wa msaada utakao toa katika shule anayosoma mwanao au hata mtoto wa jirani yako, wakifanya hivi wazazi watano kutakuwa na vitabu 100 ikiendelea kwa miaka miwili au mitatu hiyo shule haitakuwa tena na shida ya vitabu na kama jamii mnakuwa mmechangia kuleta maendeleo ya kielimu.

Changamoto ya usafiri kwa wanafunzi

Tumekuwa tukishuhudia kila siku namna ambavyo wanafunzi huwa wanateseka katika swala la usafiri wa kwenda shule na kurudi nyumbani. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kama tukishirikiana kwa pamoja wazazi na walezi wa hawa wanafunzi au watoto wetu wanaopata shida hii ya usafiri. Kama wazazi wakikubaliana na madereva hata watano tu wa daladala ambao watakuwa wanawabeba wanafunzi hao kwenda shule na kurudi nyumbani bila kuharibu safari zao za kawaida yaani kama ni gari ya gongo la mboto ibebe wanafunzi wanaoelekea huko huko.

Pia njia nyingine ni ya wazazi kuongea na uongozi wa miji waweke utaratibu kuwa kila daladala litumie safari yake moja ya siku kubeba wanafunzi yaani ikipakia wanafunzi tupu asubuhi basi ikifika jioni muda wanatoka shule hatawajibika yeye kuwabeba tena hao wanafunzi watabebwa na daladala nyingine ambayo haikuwapakia asubuhi, kwa taratibu kama hizi tutakuwa tumeboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi.

Changamoto ya hulka ya kusoma au kwenda shule

Wanafunzi wengi siku hizi hawapendi kusoma na hawapendi zaidi kwenda shule hii inaweza kuwa inasababishwa na ukali wa walimu mashuleni lakini pia husababishwa na ukosefu wa dira ya kielimu kwa wanafunzi. Hapa Tanzania mwanafunzi anasoma darasa la kwanza hadi kidato cha nne na msomi pekee anayemfahamu ni mwalimu wake tu basi hali hii hupelekea wanafunzi wengi kuichukia elimu na kuona hakuna maana ya kusoma. Kama jamii tunaweza kutatua changamoto hii na kubadilisha fikra za wanafunzi kwa kuwa mabalozi wa taaluma zetu kutembelea shule na kuongea na wanafunzi wajue kuwa taaluma zipo nyingi na zinahitaji ufaulu wa masomo gani ili uweze kusomea.

Kama wewe ni daktari, mwanasheria, manager, mwandishi wa habari, engineer ukipata muda tembelea shule yeyote iwe ya serikali au ya binafsi uongee na kupiga stori na wanafunzi waruhusu wakuulize maswali mbalimbali kuhusu taaluma yako, waeleze changamoto ulizopitia katika safari yako ya kielimu wajulishe faida ya kuwa na taaluma kama yako. Wanafunzi wengi siku hizi wamekuwa wakitamani kuwa wasanii wa mziki au waigizaji (sio kwamba ni kitu kibaya) hii ni kwasababu hao ndo watu wanaoona wana mafanikio katika jamii lakini mwanafunzi huyo huyo akijua kuwa ukiwa manager wa Vodacom, CRDB bank au kampuni kubwa kubwa familia yako inakuwa na bima ya kutibiwa hadi nje za nchi, unapewa gari la kazi, unalipiwa nyumba unayokaa ukitaka unasomeshwa na kampuni na vingine vingi tu watoto wetu wakijua haya hawatakuwa tena na wasiwasi na maisha yao ya kielimu watasoma tena kwa bidii mpaka na wao wayafikie mafanikio ya kiwango hicho.

Kwa kumalizia naomba kusema kuwa tukishirikiana kama jamii tunaweza kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya elimu Tanzania, sio lazima tusubirie serikali itufanyie kila kitu mtu binafsi kwa kwenda tu shule na kupiga stori na wanafunzi kuhusu kazi yako inatosha kuleta mabadiliko makubwa sana ya kifikra kwa wanafunzi na kuwafanya waongeze bidii katika masomo yao. Pamoja Tunaweza!​
 
Upvote 422

Thread yako ni nzuri ila hajagusa maeneo mengi muhimu.

Kwa mitazamo wangu ungegusia pia lugha ya kufundishwa na Vocational training. Kwenye vocational training Tanzania imejitahidi sana probably is one of the best. Hii simaanishi kuwa our vocational training is the best.

Kwenye lugha ya kufundishwa ndiyo our biggest challenge. Kama watu wetu wangeweza kufundishwa kwa lugha moja ambayo kwa mitazamo wangu ni Kingereza ingewasaidia sana.

Hii ni kwa sababu moja. Ingewasaidia kuelewa wanachojifuza na kuachana na kukariri. Pia kwa wale wanaotakiwa kujipendekeza au kupata uelewa zaidi kwenye fani zao lugha ingewasaidia zaidi maana siyo rahisi kufanya hivyo kwa kutumia kiswahili. Mfano mdogo tu, fundi wa gari amekutana na small fault kwenye gari, let say BMW, kama hajui kingereza jawezibkugoogle na kupata solution kirahisi kwa tatizo ambalo halijui wakati matatizo kama hayo watu wa nakutana nayo kila siku na wanatoa solution zake kwenye mtandao.
 
Asante sana kwa maoni yako kwa kweli hapo kwenye lugha ya kufundishia hata mimi nakubaliana na wewe kwamba ingetumika tu lugha moja ambayo ni kiingereza maana kimsingi haileti maana kama mtu utasoma sekondari, advance na chuo kwa kiingereza kwa nini shule ya msingi usome kiswahili where is the logic in this ? kwakweli wizara ya elimu inatakiwa ilione hili swala na kulirekebisha ili kukuza na kuboresha elimu ya Tanzania. Asante sana kwa Ushirikiano wako 🙏
Serikali inaogopa kufanya hivyo kwa Sasa kwa sababu nyingi ambazo nyingine ni za kisiasa. Hakuna anayetaka kufunga Paka kengere.

Ila hilo linawezeka hata kama ni kwa kuanza kufundishwa kingereza kwa kiswahili kwa kuwa walimu wengi hawajui kingereza. Ila hilo la kubadili lugha limefanikiwa kwenye nchi kama Namibia ( kutoka Afrikaans to English), Mozambique na Rwanda pia wanaonekana kufanikiwa. Ni decision tu ndiyo inatukwamisha.
 
Kwa hatima ya elimu Tanzania mabadiriko yanahitajika sana sana. Lakini nafikiri kuna kundi furani la watu linafaidika sana na mfumo huu wa elimu ulivyo.

Kufanikisha hili tunapaswa pia kubadiri mitazamo ya watu ikiwa pamoja na imani na itikadi zetu, pia utayari wa watu mazingira ya uhiari wa watu.

Sylabus ni msingi mkubwa sana kwa wananchi maana ndio inayotengeneza aina ya watu fulani katika eneo fulani na maendeleo ya vitu na mindset za watu.

Hii itasaidia sana kubadirisha ethics za watu na viongozi, japo kubadili mfumo huu ni kazi kubwa na itachukua muda kidogo lakini ikifanikiwa mfumo unabadilika mazima.
 
Kabisa yaani kuna mambo mengi sana ya kuzingatia tunapozungumzia swala la kuipa elimu kipaumbele la kwanza likiwa ni sisi wenyewe wananchi unakuta mzazi anaitwa kwenye kikao shuleni haendi matokeo yake walimu na wenyewe wanakosa watu wa kuwahoji kuhusu ufundishaji wao au adhabu zinazotolewa mashuleni na kupelekea kudumaa kwa elimu kwa wanafunzi wetu. Ukifuatilia vizuri utagundua kuwa tofauti kubwa iliyopo kati ya wanafunzi wanaosoma shule za kulipia na wanaosoma shule za serikali kwenye upande wa ufaulu wa mtoto swala huwa sio mzazi analipia kiasi gani mtoto asome shule hiyo swala ni je mzazi anafuatilia kiasi gani maendeleo ya mwanae huko shuleni? Tukiwa wafuatiliaji kwenye elimu za watoto wetu walimu pamoja na wanafunzi wanalazimika kuwajibika ili kuwe na matokeo mazuri.
Nahisi mjadara wa Rais mstaafu Hayatty Benjamin Mkapa ungefanyika ungeleta chachu Ktk Elimu
 
Katika taifa letu la Tanzania, watanzania tumejijengea utaratibu wa kushirikiana katika maswala mbalimbali ndani ya jamii zetu kama kuchangiana harusi, kutoa rambi rambi kwenye misiba na kujenga makanisa pamoja na misikiti. Haya yote yanafanyika na yanafanikiwa kutokana na nguvu ya umoja na mshikamano iliyopo katika jamii zetu.

Nguvu hii hii tunayoitumia huku kwenye maswala mengine ya kijamii tukiielekezea kwenye kuboresha elimu na kusomesha wanafunzi waliopo katika jamii zetu tutafika mbali kama taifa. Kuna changamoto nyingi sana katika sekta ya elimu baadhi zikiwa ni changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na chuo kikuu, vitabu vya kusomea mashuleni, usafiri wa wanafunzi na hulka ya kusoma au kwenda shule.

Changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na vyuo vikuu

Kwa kupitia dini zetu na kwa uhamasijaji wa viongozi wa dini zetu tunaweza tukashirikiana katika kusaidia wale wanafunzi ambao tunasali nao katika makanisa na misikiti yetu, wanafunzi hawa wanaweza kuwa wadogo zetu, majirani zetu, wanakwaya wetu, vijana wetu makanisani na wanajumuiya wenzetu. Kama tunaweza kuchangishana katika ujenzi wa makanisa, kurekodi video na audio za kwaya zetu, sherehe mbalimbali za kidini basi hili nalo pia linawezekana.

Kama kila kanisa na msikiti wakiamua kusomesha wale wanafunzi ambao ni waumini wao tu naamini kuwa hakutakuwa tena na wanafunzi watakaoshindwa kwenda kusoma kwa kukosa ada. Kihesabu zaidi ni kwamba kanisa moja likiwa na wanafunzi watano wanaotarajia kwenda sekondari (A level) ambako ada ni 70,000/= Tsh ukijumlisha na michango ya shule inafika 120,000/= Tsh kwa mwanafunzi mmoja wakiwa watano jumla inakuwa 600,000/= Tsh kwa miaka yote miwili inakuwa ni 1,200,000/= Tsh kwa kushirikiana hivi na kufanikisha jambo hili kanisa linakuwa limeokoa maisha ya vijana hawa na kuwapa nafasi ya kufanikiwa kielimu.

Changamoto ya vitabu vya kusoma mashuleni

Katika swala la vitabu vya kusomea mashuleni wazazi na jamii kwa ujumla tumekuwa tukiilaumu serikali kwa kutonunua na kupeleka vitabu vya masomo mashuleni tunasahau kuwa hata sisi binafsi kama jamii tunao uwezo wa kufanikisha hili swala kwa urahisi sana. Katika shule zetu huwa kuna wanafunzi wanaotoka katika familia zenye hali tofauti ya kiuchumi, kama mzazi unauwezo wa kumnunulia mtoto wako simu ya laki 3 basi unaouwezo wa kununua vitabu 20 vya 15,000/=Tsh.

Sawa unaweza usipongezwe wala kushukuriwa kama utakavyotarajia lakini fahamu kuwa kuna maisha ya mwanafunzi mmoja au wawili hapo shuleni utakuwa umeyaokoa cha muhimu ni kuzingatia umuhimu wa msaada utakao toa katika shule anayosoma mwanao au hata mtoto wa jirani yako, wakifanya hivi wazazi watano kutakuwa na vitabu 100 ikiendelea kwa miaka miwili au mitatu hiyo shule haitakuwa tena na shida ya vitabu na kama jamii mnakuwa mmechangia kuleta maendeleo ya kielimu.

Changamoto ya usafiri kwa wanafunzi

Tumekuwa tukishuhudia kila siku namna ambavyo wanafunzi huwa wanateseka katika swala la usafiri wa kwenda shule na kurudi nyumbani. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kama tukishirikiana kwa pamoja wazazi na walezi wa hawa wanafunzi au watoto wetu wanaopata shida hii ya usafiri. Kama wazazi wakikubaliana na madereva hata watano tu wa daladala ambao watakuwa wanawabeba wanafunzi hao kwenda shule na kurudi nyumbani bila kuharibu safari zao za kawaida yaani kama ni gari ya gongo la mboto ibebe wanafunzi wanaoelekea huko huko.

Pia njia nyingine ni ya wazazi kuongea na uongozi wa miji waweke utaratibu kuwa kila daladala litumie safari yake moja ya siku kubeba wanafunzi yaani ikipakia wanafunzi tupu asubuhi basi ikifika jioni muda wanatoka shule hatawajibika yeye kuwabeba tena hao wanafunzi watabebwa na daladala nyingine ambayo haikuwapakia asubuhi, kwa taratibu kama hizi tutakuwa tumeboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi.

Changamoto ya hulka ya kusoma au kwenda shule

Wanafunzi wengi siku hizi hawapendi kusoma na hawapendi zaidi kwenda shule hii inaweza kuwa inasababishwa na ukali wa walimu mashuleni lakini pia husababishwa na ukosefu wa dira ya kielimu kwa wanafunzi. Hapa Tanzania mwanafunzi anasoma darasa la kwanza hadi kidato cha nne na msomi pekee anayemfahamu ni mwalimu wake tu basi hali hii hupelekea wanafunzi wengi kuichukia elimu na kuona hakuna maana ya kusoma. Kama jamii tunaweza kutatua changamoto hii na kubadilisha fikra za wanafunzi kwa kuwa mabalozi wa taaluma zetu kutembelea shule na kuongea na wanafunzi wajue kuwa taaluma zipo nyingi na zinahitaji ufaulu wa masomo gani ili uweze kusomea.

Kama wewe ni daktari, mwanasheria, manager, mwandishi wa habari, engineer ukipata muda tembelea shule yeyote iwe ya serikali au ya binafsi uongee na kupiga stori na wanafunzi waruhusu wakuulize maswali mbalimbali kuhusu taaluma yako, waeleze changamoto ulizopitia katika safari yako ya kielimu wajulishe faida ya kuwa na taaluma kama yako. Wanafunzi wengi siku hizi wamekuwa wakitamani kuwa wasanii wa mziki au waigizaji (sio kwamba ni kitu kibaya) hii ni kwasababu hao ndo watu wanaoona wana mafanikio katika jamii lakini mwanafunzi huyo huyo akijua kuwa ukiwa manager wa Vodacom, CRDB bank au kampuni kubwa kubwa familia yako inakuwa na bima ya kutibiwa hadi nje za nchi, unapewa gari la kazi, unalipiwa nyumba unayokaa ukitaka unasomeshwa na kampuni na vingine vingi tu watoto wetu wakijua haya hawatakuwa tena na wasiwasi na maisha yao ya kielimu watasoma tena kwa bidii mpaka na wao wayafikie mafanikio ya kiwango hicho.

Kwa kumalizia naomba kusema kuwa tukishirikiana kama jamii tunaweza kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya elimu Tanzania, sio lazima tusubirie serikali itufanyie kila kitu mtu binafsi kwa kwenda tu shule na kupiga stori na wanafunzi kuhusu kazi yako inatosha kuleta mabadiliko makubwa sana ya kifikra kwa wanafunzi na kuwafanya waongeze bidii katika masomo yao. Pamoja Tunaweza!​
Mkuu Kwanza nikupongeze kwa andiko zuri Sana, ninayo mambo kadhaa..

Mosi, wanafuzi uliowataget Ni wa level ipi?? Maana ikiwa Ni wa primary hadi o-level Basi andiko lako lisahihishe liwiane na mapendekezo..

Pili, kwa kuzingatia kuchangiwa makanisani, huoni kwamba wazaz watakuwa na uzembe wakutokuwajibika?? Au unamaana kwa wale wazazi wanaoshindwa ndipo harambee itolewe??

Tatu, zingatia mazingira ya kijografia, na hali ya hewa, je usafri wa dar utakuwa sawa na wa mwz?? (Ulizingatia swali no 1)

Nne, mwisho eleza uzoefu wako binafsi, ukizingatia maelezo hayo, je unaushuhuda wako binafsi kwa elim ya tz kuwa umeyaishi uliyoyaeleza??

Mkuu nakuja kupiga kura kwako nikipata mrejesho wa maswali hayo kila raheri mkuu
 
Asante sana kwa kusoma makala yangu na kuhusu hayo maswali uliyoniuliza naomba nikujibu kama ifuatavyo

1. Wanafunzi niliowatarget ni wa kuanzia O-level mpaka Advanced secondary ila kwa waliopo O-level kwavile sasa hivi Tanzania elimu ni bure kuanzia shule za msingi mpaka O-level basi swala la ada nililolizungumzia linawagusa wanafunzi wa Advance secondary ila kwa upande wa usafiri hiyo inagusa wanafunzi wote kwa ujumla kuanzia shule ya msingi kwenda hadi Advance sekondari.

2. Kuhusu kuchangiwa ada makanisani au msikitini nilielezea hilo kwasababu kutokana na ukaribu ambao watu tunakuwaga nao ndani ya dini zetu kama wakristo tuna hadi jumuiya za nyumba kwa nyumba, tuna mazoezi ya kwaya, fellowship haya mambo yote yanatujengea ukaribu na waumini wenzetu kana kwamba kipato chako kinakuwa sio siri tena kwa waumini wenzako maana kwa mijumuiko mnayofanya pamoja wanaona kabisa hali yako halisi ya maisha hata bila kuwaambia kwa hiyo kwa kutumuia ukaribu huu huu hawa watu wanaokufahamu zaidi unaosali nao wanaweza wakawa mashaidi kanisani unapoenda kuomba msaada kwamba hauna hela ya kumpeleka mtoto shule wanajua unasema ukweli na hata wasipokuamini watakuja tu kumuona kuwa huyo mtoto kweli hakwenda shule pale wanapokuja jumuiya nyumbani kwako. Na pia katika swala la uzembe kwa wazazi ni kuweka tu utaratibu maalum kanisani kuwa kama hatuwapi hela hawa wenye shida basi angalau tuwakopeshe bila riba au kama kiwango ni kikubwa sana unachoomba waseme kuwa tunakupa hela yote sasa hivi ila utarudisha nusu ili wenzako pia wanufaike na mrejesho wako hapo kila mtu anakuwa na amani na anachokifanya.

3. Kwenye mazingira ya usafiri kusema ukweli mimi nilikuwa na elezea kwa upande wa Dar es salaam maana ndo nilipo na ndo ninapoiona hiyo shida sijajua kuhusu mikoa mingine kama wanatatizo la usafiri kwa wanafunzi kama ilivyo kwa Dar.

4. Tukija kwenye swala zima la uzoefu wangu binafsi ni kweli kabisa mimi nimeyapitia hayo yote niliyoyaelezea kuanzia changamoto ya ada kwenda kusoma advance nilikuwa nahangaika sana kuikamilisha hiyo ada namshukuru Mungu ndugu zangu walijitahidi sana kunichangia mpaka nikaweza kumaliza shule na pia kwenye usafiri napo hiyo changamoto nayo niliipata maana O-level niliyosoma ilikuwa mbali na nyumbani hivyo nilikuwa nalazimika kupanda gari moja kwenda shule, japokuwa sikuwa naenda mbali sana kama wanafunzi wengine lakini bado kwa huo umbali mfupi tu wa gari moja bado nilikuwa nasumbuka kupata usafiri nilichokuwa nafanya mimi ni kudamka saa 11 mpaka inafika saa 12 kamili mi nakuwa tayari nipo shule na jioni nilikuwa nabaki kujisomea shule mpaka saa 11 tena jioni ndo naondoka nilikuwa nafanya hivyo ili kukwepa ule muda ambao wanafunzi wengi ndo huwa wanakuwa stendi wakisubiri usafiri. Na pia tukija kwenye swala zima la hulka ya kusoma mimi binafsi nimesoma kuanzia form 1 hadi form 4 sijawahi kuonana na mwanafunzi wa Advance hata nilikuwa sijui wanafananaje sasa hiyo ilikuwa inaninyima raha maana nilikuwa nikiwaza kwamba kama wapo wachache kiasi hiki mpaka sikutani nao ovyo ntatoboa kweli form 4?

Nimalizie tu kwa kusema kuwa safari ya Elimu kwa Tanzania ina changamoto nyingi sana kwa wanafunzi kiasi kwamba wanaofanikiwa kuivuka hiyo hatua hawatamani kabisa hata kurudi nyuma na kuwapa moyo wadogo zao unakuta mtu akirudi shule aliyosoma ni kwaajili tu ya kufuata cheti chake tu basi hata ongea na walimu waliomfundisha wala wanafunzi aliowakuta wakisoma kama yeye kipindi akiwa shule naamini kuwa tukibadilika na kuzingatia haya niliyoyaelezea kwenye makala hii tunaweza kuongeza ubora katika elimu ya Tanzania. Asante sana kwa ushirikiano wako naomba kuwasilisha [emoji120]
Unakula yangu mkuu, kimsingi nlitaka tu kupima uwezo wako wakujib, mapungufu kadhaa nliyoyaona yakiboreshwa na kuweka Kama andiko la tz nzima bandiko hli litakuwa na maana Sana, yaan Kama jamii ikiamua tu kila harus watoe 10% ya michango ya harusi katika mfuko wa elim ya mtoto alieko upande wa kike/kiume au 10% ya mahali, hakuna mtt atakae kwama kwenda shule, hicho Ni chanzo kizr mno,

Tatzo tu mpka elim kubwa itumike kuibadili jamii na njia ya Kwanza ya kabadilika Ni kuanza na Mimi.
 
Suala la elimu ni complex sana, limegawanyika sehemu nyingi na serikali binafsi haiwezi kutoa kila kitu kwa ubora hitajika.

Tunaona siku hizi kuna elimu bure lakini kiwango vha ubora wa elimu inayotolewa ni kibovu kisichowarudhisha wengi, licha ya serikali kuwataka wapeleke watoto wao kwenye public schools bado inakuwa bora kwa mzazi mwenye uwezo apeleke mtoto wake private akapate elimu bora.

Hapa nachojifunza ni kwamba, serikali ilegeze masharti kwa shule binafsi kwa vifaa ili elimu itayotolewa huko ipunguzwe bei (ada), kwa kufanya hivi taifa litakuwa na kizazi kilichoelimika kwa quality education.

Lakini pia serikali itapunguziwa mzigo wa watoto wengi kwenda kwenye shule zake, hivyo itaweza kugawanya resources chache ilizonazo kuwapa wale watakaokuwepo mashuleni (public schools).
 
Hapa kusema ukweli sikubaliani na wewe serikali ikizipa shule binafsi kipaumbele zaidi ya hiki kilichopo sasa hivi basi kutakuwa hamna maana ya kusoma kabisa shule za serikali maana watakuwa wanatunga sheria kulingana na matokeo wanayoyaona na matokeo watakayokuwa wanayaona ni ya shule binafsi kitu ambacho kitawaumiza na kuwakandamiza zaidi wanafunzi waliosoma shule za serikali.
Utakuwa hujanielewa, shule binafsi zisipewe kipaumbele, nachotaka zipunguziwe gharama za uendeshaji ikiwemo kodi na serikali ili waweze kutoa elimu zao kwa gharama nafuu hivyo kuipunguzia serikali mzigo wa kupokea wanafunzi wengi ambao hushindwa kuwa accomodate.

Kama darasa moja lina wanafunzi zaidi ya mia moja mwalimu ataweza vipi kuwa handle hao wote na kufuatilia maendeleo yao darasani? hili pekee linachangia kupunguza ufaulu kwenye shule za serikali sababu mwalimu anaelemewa na rundo la wanafunzi.

Lakini pia, tatizo la ukosefu au upungufu wa walimu, hapa napo kama serikali itafanya kwa kuiwezesha sekta binafsi kujiendesha bila gharama za ziada, waweze kuwatumia walimu wachache walionao hasa wa sayansi kwenye shule zake, na kuendelea kuajiri wengine taratibu wakati ambapo shule binafsi zitakuwa zimejisogeza kwa kuchukua wanafunzi ambao watakuta tayari kuna walimu wa sayansi kwenye shule zao.
 
Kwa hatima ya elimu Tanzania mabadiriko yanahitajika sana sana. Lakini nafikiri kuna kundi furani la watu linafaidika sana na mfumo huu wa elimu ulivyo.

Kufanikisha hili tunapaswa pia kubadiri mitazamo ya watu ikiwa pamoja na imani na itikadi zetu, pia utayari wa watu mazingira ya uhiari wa watu.

Sylabus ni msingi mkubwa sana kwa wananchi maana ndio inayotengeneza aina ya watu fulani katika eneo fulani na maendeleo ya vitu na mindset za watu.

Hii itasaidia sana kubadirisha ethics za watu na viongozi, japo kubadili mfumo huu ni kazi kubwa na itachukua muda kidogo lakini ikifanikiwa mfumo unabadilika mazima.
Asante sana kwa maoni yako Nashkuru 🙏
 
Karibu katika mjadala huu tuanze kwa kuongelea uzoefu wako binafsi wa changamoto hizi zilizoelezewa na namna ambavyo unaweza kuchangia maendeleo ya jamii inayokuzungua baada ya kusoma na kuelewa makala hii.
 
Yakifanyiwa kazi haya kwa hakika tutapiga hatua sana katika taaluma
Kabisa yaani maana wasomi wakiwa wengi nchini maana yake zile taaluma ambazo zilikuwa na uhaba wa wafanyakazi kama madaktari idadi itaongezeka kitu ambacho kitachochea maendeleo ya sekta zingine na nchi kwa ujumla.
 
Umewaza vizuri sana siyo kila mara kutegemea wafadhili kutoka nnje wenye masharti hii nndo maana ya ukombozi wa elimu
Kabisa yaani mi naamini kuwa tukiamua wote katika jamii zetu kuipa elimu kipaumbele zaidi ya mambo yote tutaikomboa nchi yetu ndani ya hata miaka 20 maana tutakuwa na wasomi wa kutosha na hiyo itapelekea kuongeza nguvu kazi ya taifa na kupelekea kukua kiuchumi.
 
Back
Top Bottom