Mchango wa sherehe ya kumaliza Masters itakayofanyika ukumbini. Nini maoni yako kuhusu uchangishaji wa sherehe za namna hii?

Ulofa unakusumbua yaani mchango wa elfu 50 unaandika maneno yote hayo ungeambiwa mchango milioni si ungejinyonga

Kemea Pepo la umaskini likutoke kwa Jina la Yesu
A Fool and his Money, are Soon Parted....

Unadhani wenye pesa wakizitoa willy nilly bado wangekuwa nazo ? Bora nitoe milioni moja kwa vitu constructive (kumpa hata mtu asiye na chakula) kuliko sumni kwa vitu visivyo tija....
 
Hatari, nliwah mkopesha mtu aongezee katka mahari yake, akaingia mitini na pesa yangu. Ngawa na ndoa haikudumu
 
Hajatajwa mtu hapa ndugu. Kumdhalilisha mtu ni kumtaja au kuweka picha yake hapa.
 
Hizi ni sherehe za ovyo kabisa. Mwache asherekee yeye mwenyewe pamoja na familia yake asituchoshe na michango isiyokuwa na kichwa wlaa miguu.
 
Mwambie hasisumbue watu, graduation huwa haichangiwi.
 
Kwenu ndiko graduation huwa haichangiwi kwetu huwa tunachangia

Utoe tu kadi isirudi tu
Unajionaje kuchangisha sherehe za namna hiyo ikiwemo birthday. Kwa nini kama kama unazipenda sana hizo sherehe, why usijipange mwenyewe then ukafanya ukaribisho tu kwa watu kuhudhuria, ili atayepata nafasi afike atayekosa basi. Kuliko ukose hiyo michango kwa watu wasioona umuhimu wa vitu hivyo then ukabak kuwachukia bure, kumbe sherehe zenyewe za kidwanzi.
 
Sherehe mtu hula na wakwao watu hawakosekani hata uchangishe mchango wa ngoma za kutoa mwali, kigodoro,kibati ,kangamoko au mdundiko nk wako wenyewe ambao shughuli ni watu na watu ndio wenyewe hao na watachanga hata zaidi ya pesa ya kwenye kadi utashangaa tu watu kibao utabaki domo wazi na ubahili wako na roho mbaya kuwa Sherehe ya mtu isifanikiwe

Utashangaa watu wanaserebuka kwa furaha na Wimbo wa Jogoo kichwani mgumu kumvalisha kilemba hakikai
 
huenda ikawa kweli sikupingi. watz na mshikamano wapi na wapi. sisi kunafikiana.
 
Money is the source of many evils!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…