Mchapakazi kijana Waziri Hussein Bashe, historia ya ushupavu Tanzania itamkumbuka

Mchapakazi kijana Waziri Hussein Bashe, historia ya ushupavu Tanzania itamkumbuka

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ataandikwa kwenye kumbukumbu za historia za viongozi shupavu wa nchi hii kwa namna alivyothubutu kuchochea mageuzi na mabadiliko katika kilimo kwa bajeti ndogo tu.

Kipindi hiki cha mavuno ya mazao mbalimbali nchini, kinadhihirisha uthubutu, nia na dhamira yake njema ya kuchochea na kuleta mageuzi katika kilimo Tanzania ili kiwe chenye tija na matokeo mazuri zaidi ya haya ya sasa hakuna tena uhaba wa malighafi za viwandani zitokanazo na kilimo.

Katika kipindi kifupi sana cha uongozi wake mamilioni ya vijana wamevutiwa na kujiajiri kwenye sekta hii muhimu ya kilimo na kupunguza tatizo la ajira nchini. Hii imeongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa kiasi kikubwa na kusaidia kupunguza na kudhibiti mfumuko wa bei kwenye mazao ya chakula.

Matokeo yake hakuna kitisho cha njaa tena Tanzania, licha ya mvua za mwaka huu kutokua nzuri sana zilizozidi matarajio na kuathiri baadhi ya mazao kiasi. hata hivyo hali ya mavuno ni nzuri mno ukilinganisha na wakati mwingine.

Ndugu zangu mnyonge mnyonge Lakini haki yake mpeni, waziri wa kilimo Hussein Bashe anapiga kazi sana shambani aise.

Upatikanaji wa pembejeo za kisasa za kilimo, mbolea na madawa ya wadau, elimu ya kilimo cha kisasa, mbegu bora na za kisasa za mazao mbalimbali, pamoja na soko la uhakika la mazao mbalimbali ya biashara na bei nzuri za uhakika.

Kiongozi huyu Jasiri amefanya kilimo kiendelee kua ni fursa muhimu ya ajira ya kudumu na ya uhakika inayoongoza kwa kuvutia vijana wengi zaidi nchini. Kongole nyingi sana kwa vijana kuchangamkia fursa hii muhimu ya ajira.

Mpaka sasa mageuzi haya ya kilimo yanayosimamiwa na kupangwa na kijana huyu hodari, mchapakazi asie choka wala kukata tamaa, yanapunguza hali ya umaskini wa kipato na chakula kwa waTanzania kwa kiwango kikubwa sana na hivyo kuboresha na kuinua hali ya maisha ya waTanzania.

Licha ya setbacks, chuki na uzushi dhidi ya waziri huyo shupavu, kutoka kwa watu wasio itakia mema Tanzania, Waziri Husseni Bashe alisimama kidete na waTanzania na kwa umakini mkubwa sana kuchukua hatua muhimu na kuingilia kati tatizo la upungufu wa sukari lililotokea huko nyuma, baada ya viwanda kusitisha uzalishaji wa bidhaa hiyo muhimu kutokana na mvua nyingi sana kuathiri wa zao hilo.

Alichukua hatua madhubuti za makusudi kwa mujibu wa sheria na hali ya dharura ya uhitaji wa sukari wakati huo, ambazo zimeacha historia ya kipekee sana kwa vijana kuiga mfano wake wa uthubutu, wanapopewa dhamana na fursa ya kuongoza umma..

Historia ya watu hodari shupavu, madhubuti na wenye uthubutu itakukumbuka daima ndugu waziri..
Hongera sana watu wa Jimbo la Nzega Mjini, mna kiongozi makini lakini pia ni mtu na nusu 🐒

Well done waziri, comrade Husseni Bashe.

God bless you gentleman 🙏
 
Huwa nikiona andiko refu kama hili kutoka kwa Pro CCM najuaga Tu ni pumba tupu always!
unaelewa nchi hii ina changamoto kadha kubwa mtambuka tunazopambana nazo kwa nguvu sana kila siku kuzitokomeza 🐒

@umaskini wa fikra
@umaskini wa kipato

na miongoni mwa sababu zinazochangia changamoto hizo ni pamoja na uvivu na hivi sasa kuna hii ya mihemko isiyo na tija...

nadhan huna sababu yoyote kuexpress aina ya uvivu ulio nao humu jukwaani, kwamba wewe kusoma paragraphs mbili tu jasho linakutoka mbaya sana 🤣

huwezi kua na fikra mpya,uelewa na ufahamu wa mambo mengi kwa kuendekeza aina hiyo uvivu, daima hitimisho la hoja usizo elewa itakua ni kwa mihemko, ghadhabu na hasira tu 🐒
 
ID za kimkakati...yaani ni uchawa mwanzo mwisho
Ngoja nami niandae andiko la kumsifu Luaga Mpina
anahusika na nini huyo muungwana ulomtaja 🐒

mie namzungumzia mageuzi aloleta waziri kijana mchapakazi hodari Hussein Bashe kwenye sekta ya kilimo 🐒
 
Hizi ID mnazoanzishia nyimbo za kusifu na kuabudu it will reach a time mtazikimbia na kuzionea haya kama umejinyea, miaka hii ni ya machawa kama wewe do it to the fullest, kama una familia sijui unafundisha Nini watoto wako nyumbani, shame on you
 
"Utii ukizidi unakuwa UOGA. Uoga huzaa
UNAFIKI na KUJIPENDEKEZA mwisho wake ni
MAUTI"

Julius K. Nyerere,
Rais wa kwanza wa Tanzania.
katika nyakati hizi mihemko ni kiwango cha juu sana cha kukosa fikra mpya na uelekeo lakini ni dalili ya kukata tamaa kabisaa 🐒

hata hivyo,
kwenye sekta ya kilimo waziri Husseni Bashe amebadili kabisa fikra na mtindo wa kilimo cha Tanzania,
Anastahili pongezi anastahili kuungwa mkono na kila mTanzania 🐒
 
Back
Top Bottom