Mchapakazi kijana Waziri Hussein Bashe, historia ya ushupavu Tanzania itamkumbuka

Mwamba atakumbukwa na vizazi vijavyo na siyo majangili ya CCM
sure,
Atakumbukwa sana kwa kubuni tuhuma za uzushi na uongo, jeuri, kiburi na hasira za kutemwa kwenye baraza la mawaziri 🀣

zaidi sana atakumbukwa kwa kutumia rula kupima size ya ukubwa wa samaki waliorostiwa vizuri sana kwa nazi aise 🀣

achilia mbali kwa kuchoma nyavu za wavuja jasho, kutaifisha ng'ombe mbuzi na kondoo za watu, mbaya zaidi kuangamiza mamilioni ya vifaranga vya kuku bila kujali hasara watakazopata wafanyibiashara wale πŸ’

atakumbukwa sana kwa mengi kwakweli πŸ’
 
Msomali ametoa rushwa CCM nzima mmemkubali kama DP World
 
Msomali ametoa rushwa CCM nzima mmemkubali kama DP World
Waziri wa kilimo Husseni Bashe, atawekwa kwenye vitabu vya kumbukumbu Kwa namna alivyo buni mipango ya kuleta mageuzi na Mapinduzi kwenye sekta muhimu sana ya kilimo,

leo hii mtu alie lima ekari 10, itamlazimu atumie siku si chini ya 10 kuvuna shamba lake tofauti na huko nyuma shamba la ekari 10 unavuna kwa siku moja au mbili tu 🀣
 
UWT sijui kama nyie ni wazima kichwani
 
Bashe muoga hana ujasiri wowote, ameshindwa kujitokeza hadharani kujibu tuhuma dhidi yake, badala yake anatetewa na kamati ya bunge.

Hafai.
 
"WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA NEW HABARI (2006) LTD WATOA SIKU 14 KWA MFANYABIASHARA ROSTAM AZIZ KULIPA MAFAO YAO

Na swalehe kasimu Dar es Salaam.

WAFANYAKAZI zaidi ya 200, Waliokuwa wakifanyakazi katika kampuni ya New Habari (2006) Ltd, wametoa siku 14 kwa Mmiliki wa Kampuni hiyo, Mfanyabiashara na Bilionea Rostam Aziz awe amepeleka fedha za mafao katika mifuko ya Hifadhi ya Jamii ikiwemo NSSF na PSSSF kiasi cha zaidi ya Bilioni 3.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo Februari 3. 2022, Katibu wa waliokuwa wafanyakazi wa New Habari (2006) Ltd, Arodia Peter alisema licha ya kusubiria kwa muda mrefu taratibu za kisheria dhidi ya mfanyabiashara huyo pamoja na Mbunge wa Nzega Mjini ambaye pia ni Waziri wa Kilimo
Hussein Bashe kushindwa kuwasilisha mafao yao kwenye mifuko licha ya kuwakata michango kwa miaka zaidi ya 10.

"Walikuwa wanatukata mishahara yetu kila mwezi pamoja na michango ya mwajiri kwa mujibu wa sheria kwa zaidi ya miaka 10.

Licha ya kuhoji, Mwajili alituhaminisha kuwa anapeleka makato yetu katika mifuko husika...

Lakini tunashangaa Watendaji wa mifuko hiyo kutochukua hatua yoyote kwa mwajiri kwa zaidi ya miaka 10 tofauti na sheria ya mifuko hiyo unayoelekeza." Alisema Arodia.

Na kuongeza kuwa;
"Tunapenda kufikisha taarifa na kilio chetu kwa Rais Samia Suluhu Hassan juu ya madhila yanayotupata na yanayoendelea dhidi ya Rostam Aziz na Afisa Mtendaji Mkuu, Mbunge na Waziri wa kilimo Hussein Bashe kwani wameshindwa kabisa kutupelekea mafao yetu katika mifuko ya Hifadhi ya Jamii." alisema Arodia.

Rostam Aziz na Hussein Bashe walituondoa kazini Mei 31 mwaka 2019 bila kutulipa stahiki za mafao yetu kwa mifuko ya NSSF na PSSSF kwa mujibu wa Sheria.

Ambapo alifafanua kuwa; Mtendaji mkuu Hussein Bashe, aliwaondoa kazini kwa lazima wafanyakazi wote bila kutangaza kwa umma sababu ya kufanya hivyo kama sheria inavyotaka.

Kwa upande wake Mshauri katika kikao hicho waliokuwa wafanyakazi wa New Habari (2006), Mzee Balinagwe Mwambungu alitoa kilio chake kwa wadaiwa hao Rostam Aziz na Hussein Bashe, kuwa kwa sasa wanaishi kwa mateso huku pesa zao zikiwa zipo kwa wadaiwa.

"Wapo wenzetu wametangulia mbele za haki na familia zao tuonao hapa wakidai malipo ya wapendwa wao.

Waliotangulia mbele za haki ni pamoja na: Aliyekiwa Mhariri Kanda ya Kaskazini, Elia Mbonea, Mhariri wa Maudhui ya Habari wa kampumi, Mwalimu Chrysotom Rweyemamu, Mhariri wa Habari wa gazeti la Rai, Innocent Mnyuku, Mhariri wa Makala wa gazeti la Rai, Mayege Mayege, Mhariri wa michezo, Asha Muhaji.

Pia wengine Afisa Utawala Msaidizi, Benjamin Mhina pamoja na Katibu Muhtasi Roida Kiverege. Hawa wote wametangulia mbele za haki na bado wanadai mafao yao kupitia kwa familia zao ambazo zinaishi kwa shida" alisema Mzee Mwambungu.

Hata hivyo kwa kauli moja wawakilishi hao wametangaza kufanya maandamano ya amani yasiyokuwa na ukomo nyumbani kwa Rostam Aziz na ofisini kwake, na pia maandamano hayo ya amani kwa Hussein Bashe na ofisini kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii.

Wafanyakazi hao zaidi ya 200 ni pamoja kutoka Tanzania nzima wakiweno Waandishi wa habari ambao ndo kundi kubwa, watu wa IT, Madereva, Walinzi, wafagiaji, mafundi mitambo na wengine wengi."

Mwisho.
Nimekopy na kupaste kutoka gazeti la mwananchi.

Huyu Msomali ni tapeli wa muda mrefu.
Huyu pia ni mmoja wapo wa wale wahamiaji haramu ambao aliwasema CDF kwamba walioteuliwa kwenye nafasi nyet serikalini.
Huyu mtu hafai kabisa kuwa kiongozi kwa kuwa sio Raia wa Nchi hii
 
Bashe muoga hana ujasiri wowote, ameshindwa kujitokeza hadharani kujibu tuhuma dhidi yake, badala yake anatetewa na kamati ya bunge.

Hafai.
inaweza ikawa ni kwasababu huna shamba ndio maana unaweza muona waziri wa kilimo mchapakazi hodari Hussein Bashe kwa sura hiyo πŸ’

lakini ungekua na kaplot ka shamba hata hekta 5 za mahindi, hungeweza kudhubutu kulaumu hayo unayolaumu, mambo ni mazuri eti kwenye mavuno gentleman πŸ’

anaweza kua mbaya mitandaoni lakini huku mashambani unaweza kupigwa makofi ukimdharau ndugu waziri comrade Husseni Bashe πŸ’
 
haya ya kibinafsi na yaliyo mahakamani nadhani watashughulika nayo katika sura hiyo ya kiraia na kibinafsi.

Nadhani hayana uhusiano na ile bidii ambayo ako nayo huyu kijana Husseni Bashe kwenye sekta ya kilimo ..

hata muwekezaji Rostam nae ni mzoefu kwenye kudeal na mambo haya na nadhani wataketi chini na kuona ikiwa pana ukweli ama ni kutoeleweka kwa sheria tu, wawekane sawa mambo yaishe πŸ’
 
Hasafishiki kwa huu upuuzi uliouleta hapa, pathetic,iko siku,jinai haifi
 
Hasafishiki kwa huu upuuzi uliouleta hapa, pathetic,iko siku,jinai haifi
tuliza ghadhabu gentleman,

mihemko ni kwenye mitandao tu,
field waziri Hussein Bashe ni king of farmers in agricultural activities πŸ’
 
HUYU NI MKIMBIZI NA FISADI
 
Wajinga mpo wengi lakini taratibu mtakwisha
 
Wajinga mpo wengi lakini taratibu mtakwisha
mihemko ni aina mpya ya umaskini wa fikra, ni uraibu na utumwa mbaya sana. ukweli utabaki kua mchungu na tutaendelea kusema kwa nguvu zote πŸ’
 
1. Utawala wa Nyerere ulisifika sana na nchi ikajengwa
2. Mzee Mwinyi alifanya aliyoyafanya.... Loliondo ikaenda
3. Mkapa akafanya mageuzi makubwa
4. Akaingia Kikwete... Dunia nzima inajua kilichotokea... Na Gesi ikaenda
5. JPM... Nchi ikajengwa mpaka Dunia ikatikisika. Wanyonge wakaheshimika
6. Dk Samia Suluhu Hassan.... Kazi inaendelea Kwa Kasi na viwango vya aina yake. Dunia imesimama. Rasilimali za Taifa zipo salama kabisa.

Jioni njema
 
maoni na mtazamo binafsi juu ya jambo au mambo kadha wa kadha ni haki na uhuru wako ila si lazima au muhimu yakubalike πŸ’

waziri mchapakazi hodari Hussein Bashe kwa wakulima Lazima tuseme asanti sana,
ametufikia kwa pembejeo za kilimo za kisasa, mbegu bora, mbolea, madawa ya wadudu, mikopo benki, masoko ya bidhaa za mazao na bei nzuri n.k

waTanzania kwasasa ni kushindilia maugali haswa uhakika wa usalama wa chakula ni mkuu,
Heko waziri Bashe πŸ’
 
Hili nalo limekaa kinafiki sana sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…